Utabiri: Simba kubeba taji la Kombe la Shirikisho barani Afrika 2021/22

Gwele

JF-Expert Member
Jun 7, 2016
2,242
2,772
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022

Simba imeonekana kuwa bora sana kwenye mechi 3 hizi za mwanzo ambapo imekuwa timu pekee katika kundi D kupata walau point ugenini na hii inatoa ishara kubwa kuwa huenda simba akamaliza kundi hili akiwa kileleni na kutinga hatua ya robo fainali

Kwa namna nilivyoziangalia timu shiriki za michuano hii ni wazi simba ana nafasi kubwa si ya kupita tu hatua ya robo fainali bali hata nusu fainal hali itakayopelekea kuingia fainali ya michuano hii na kubeba taji hilo kwa mara yao ya kwanza.

Simba kiuchezaji ina imarika kila siku benchi la ufundi linafanya kazi kubwa sana hivyo mpira watakaoucheza robo na nusu fainali utawashtua watanzania wengi hasa waliodhani labda simba imeshuka makali yake.

Tuendelee kusubiri muda lakini kwa zaidi ya 90% simba anaenda fainali ya hii michuano na kwa 60% atabeba hii ndoo kwa mara ya kwanza na kusimika rasmi ubabe barani afrika huku tukilielekea kombe la klabu bingwa barani afrika msimu unaofuata

simbasctanzania-post-2022_02_21_09_44.jpg

simbasctanzania-post-2022_02_21_09_44-1.jpg

FB_IMG_1646168130524.jpg
 
Simba imekuwa bora au Manula kawa bora? Mechi ya USGN simba walikuwa wanafungwa goli 2+ mechi dhidi ya Berkane walikuwa wafungwe 5+ ila Manula kafanya kazi ya ziada kusahisha makosa yaliyofanywa na wachezaji wake. Bado timu inafanya makosa mengi mno, spidi hakuna, mpira wa counter attack ni moja ya weakness ya Simba.

Unaposema timu bora umeitumia gizezo gani kuipima kwa performance au umepima kwa matokeoa?

Je kama umetumia muda wako kufatilia timu zote zinashiriki michuano hii mechi zao ili kuweza kujua uwezo wao?
 
Simba mwaka huu wangefika mbali sana kwenye Shirikisho lakini kitachakachowaangusha ni safu yao ya ushambuliaji. Hata kama watavuka hatua hii ya makundi bado kuendelea mbele zaidi itakuwa ngumu sana. Na hii hata kwenye NBC ligi imeshawagharimu na itaendelea kuwagharimu sana na pia itamrahisishia sana Yanga kubeba ndoo kilaini. Na huu ni ukweli mchungu ambao wanasimba wengi hawataki kuukubali mpaka sasa lakini ndio uhalisia wenyewe.

Kwa mtu aliyeitazama mechi ya juzi na Berekane kwa umakini ni lazima atakuwa ameona jinsi fowadi ya Simba inavyotaabika. Boko hata kukaa na mpira dakika moja wenzake wafike hawezi na akituliza mpira "control" chumba na sebule. Anapigiwa pasi beki wa Berekane anatoka nyuma yake anawahi mpira kabla yeye haujamfikia. Mugalu naye amekuwa na majeruhi ya mara kwa mara na hata akiwa mzima anakosa magoli ya wazi kabisa. Kagere ndiyo hivyo tena hatabiriki leo anacheza vizuri anafunga mechi ijayo anazurura tu uwanjani mpaka mpira unaisha.

Iwapo Simba ingekuwa na fowadi imara hata ile mechi ya Gendamarie wangeshinda ugenini na si kupata sare. Kwa hili Simba wapate funzo na waanze maandalizi mapema kwa kuanza kutafuta washambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. Na wanatakiwa wafanye maamuzi magumu kweli kweli kuhusiana na safu yao ya ushambualiaji.
 
Simba imekuwa bora au Manula kawa bora? Mechi ya USGN simba walikuwa wanafungwa goli 2+ mechi dhidi ya Berkane walikuwa wafungwe 5+ ila Manula kafanya kazi ya ziada kusahisha makosa yaliyofanywa na wachezaji wake...
Hivi nyie viumbe akili zenu zikoje? Inaamana Manula anacheza Ndanda FC na siyo Simba SC? Kwanini mafaniko ya golikipa yabaguliwe ilhali yeye ndo muundo wa wachezaji 11.

Kwahivyo kama Sakho akifunga mabao matatu, utakuja kusema Simba SC siyo bora ila Sakho ndo bora..!

Unajua maana ya Team Work?
 
Kwa hiyo huyo Manula ni yanga.
Simba imekuwa bora au Manula kawa bora? Mechi ya USGN simba walikuwa wanafungwa goli 2+ mechi dhidi ya Berkane walikuwa wafungwe 5+ ila Manula kafanya kazi ya ziada kusahisha makosa yaliyofanywa na wachezaji wake...
 
Hivi nyie viumbe akili zenu zikoje? Inaamana Manula anacheza Ndanda FC na siyo Simba SC? Kwanini mafaniko ya golikipa yabaguliwe ilhali yeye ndo muundo wa wachezaji 11...

Umefikiria kishabiki sana na hukutumia akili kufikiria. Manula anapofanya saving nyungi maaanake hiyo inatakiwa kuwa signal kwa kocha kuona kuna tatizo mahali hasa kwenye safu yake ya ulinzi.

Manula sio malaika ni binadamu siku akiwa hayupo mchezoni itakuwaje? Au unafikiri ansuwezo wa kusahisha kila kosa? Saa zingine muwe mnawaza kimichezo sio kiushabiki.
 
Umefikiria kishabiki sana na hukutumia akili kufikiria. Manula anapofanya saving nyungi maaanake hiyo inatakiwa kuwa signal kwa kocha kuona kuna tatizo mahali hasa kwenye safu yake ya ulinzi. Manula sio malaika ni binadamu siku akiwa hayupo mchezoni itakuwaje? Au unafikiri ansuwezo wa kusahisha kila kosa? Saa zingine muwe mnawaza kimichezo sio kiushabiki.
Jibu nilivyokuuliza huwezi kaa kimya usilete maalezo yaliyokorogeka hapa

Nini maana ya Team Work?
 
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022...
Pale unapoota saa mbili asubuhi 🤡 uko zako USA halafu unakula bugger White House na Joe Biden.
 
Kweli huu utabiri . Yaan kama TMA wangekuwa na utabiri kama huu tusingewaamini hata kido....
Yaan mkae mkijua kuwa Yanga anahitaji kushinda match 10 tu kati ya hz 14 zilizobaki na hyo itategemeana na Matokeo ya Mikia kama Kolos wakipoteza point kidogo tu basi fahamu match hazitakuwa 10 tena zitakuwa pungufu ya hzo. Sasa hyo nguvu ya kukaa na kutabiri kuwa Simba anaweza kuwa bingwa unajitolea wapi..?

Duuuuh mnasikitisha sana
 
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022

Simba imeonekana kuwa bora sana kwenye mechi 3 hizi za mwanzo ambapo imekuwa timu pekee katika kundi D kupata walau point ugenini na hii inatoa ishara kubwa kuwa huenda simba akamaliza kundi hili akiwa kileleni na kutinga hatua ya robo fainali

Kwa namna nilivyoziangalia timu shiriki za michuano hii ni wazi simba ana nafasi kubwa si ya kupita tu hatua ya robo fainali bali hata nusu fainal hali itakayopelekea kuingia fainali ya michuano hii na kubeba taji hilo kwa mara yao ya kwanza.

Simba kiuchezaji ina imarika kila siku benchi la ufundi linafanya kazi kubwa sana hivyo mpira watakaoucheza robo na nusu fainali utawashtua watanzania wengi hasa waliodhani labda simba imeshuka makali yake.

Tuendelee kusubiri muda lakini kwa zaidi ya 90% simba anaenda fainali ya hii michuano na kwa 60% atabeba hii ndoo kwa mara ya kwanza na kusimika rasmi ubabe barani afrika huku tukilielekea kombe la klabu bingwa barani afrika msimu unaofuata

View attachment 2135697
View attachment 2135698
View attachment 2135699
Naomba unitabilie na mimi unaonekana upo vizuri hio sector
 
Simba mwaka huu wangefika mbali sana kwenye Shirikisho lakini kitachakachowaangusha ni safu yao ya ushambuliaji. Hata kama watavuka hatua hii ya makundi bado kuendelea mbele zaidi itakuwa ngumu sana. Na hii hata kwenye NBC ligi imeshawagharimu na itaendelea kuwagharimu sana na pia itamrahisishia sana Yanga kubeba ndoo kilaini. Na huu ni ukweli mchungu ambao wanasimba wengi hawataki kuukubali mpaka sasa lakini ndio uhalisia wenyewe.

Kwa mtu aliyeitazama mechi ya juzi na Berekane kwa umakini ni lazima atakuwa ameona jinsi fowadi ya Simba inavyotaabika. Boko hata kukaa na mpira dakika moja wenzake wafike hawezi na akituliza mpira "control" chumba na sebule. Anapigiwa pasi beki wa Berekane anatoka nyuma yake anawahi mpira kabla yeye haujamfikia. Mugalu naye amekuwa na majeruhi ya mara kwa mara na hata akiwa mzima anakosa magoli ya wazi kabisa. Kagere ndiyo hivyo tena hatabiriki leo anacheza vizuri anafunga mechi ijayo anazurura tu uwanjani mpaka mpira unaisha.

Iwapo Simba ingekuwa na fowadi imara hata ile mechi ya Gendamarie wangeshinda ugenini na si kupata sare. Kwa hili Simba wapate funzo na waanze maandalizi mapema kwa kuanza kutafuta washambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. Na wanatakiwa wafanye maamuzi magumu kweli kweli kuhusiana na safu yao ya ushambualiaji.
Nitajie hizo timu kwenye kombe hili la shirikisho ambazo zina forward imara kiasi kwamba hata ugenini wanabeba tu point 3 zote kama wapo kwao
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom