Gwele
JF-Expert Member
- Jun 7, 2016
- 2,296
- 2,854
- Thread starter
- #21
Mada yote inazungumzia simba na Caf confederation cup wewe unakuja kucomment unaitaja Yanga hivi simba anashindana na Yanga kweli kwenye hilo kombe au ni wewe uelewa wako wa mada umekuwa mdogo mkuuSimba mwaka huu wangefika mbali sana kwenye Shirikisho lakini kitachakachowaangusha ni safu yao ya ushambuliaji. Hata kama watavuka hatua hii ya makundi bado kuendelea mbele zaidi itakuwa ngumu sana. Na hii hata kwenye NBC ligi imeshawagharimu na itaendelea kuwagharimu sana na pia itamrahisishia sana Yanga kubeba ndoo kilaini. Na huu ni ukweli mchungu ambao wanasimba wengi hawataki kuukubali mpaka sasa lakini ndio uhalisia wenyewe.
Kwa mtu aliyeitazama mechi ya juzi na Berekane kwa umakini ni lazima atakuwa ameona jinsi fowadi ya Simba inavyotaabika. Boko hata kukaa na mpira dakika moja wenzake wafike hawezi na akituliza mpira "control" chumba na sebule. Anapigiwa pasi beki wa Berekane anatoka nyuma yake anawahi mpira kabla yeye haujamfikia. Mugalu naye amekuwa na majeruhi ya mara kwa mara na hata akiwa mzima anakosa magoli ya wazi kabisa. Kagere ndiyo hivyo tena hatabiriki leo anacheza vizuri anafunga mechi ijayo anazurura tu uwanjani mpaka mpira unaisha.
Iwapo Simba ingekuwa na fowadi imara hata ile mechi ya Gendamarie wangeshinda ugenini na si kupata sare. Kwa hili Simba wapate funzo na waanze maandalizi mapema kwa kuanza kutafuta washambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. Na wanatakiwa wafanye maamuzi magumu kweli kweli kuhusiana na safu yao ya ushambualiaji.
Hebu tuchangie kulingana na mada iliyopo mezani sio mahaba yako niue kwa klabu yako