Utabiri: Simba kubeba taji la Kombe la Shirikisho barani Afrika 2021/22

Kwenye timu zote 16 unaleta timu moja tu ndio ujue ni jinsi gani ilivyo ngumu kufanya hivyo na ndio maana unaona pamoja na dharau zako zote kwa simba ila ndio timu pekee kundi D kupata point ugenini sio Asec Mimosas wala Barkane
Ume badili gia ulisema hakuna team iliyo pata point ugenini nmekuonyesha jamaa wametwanga mtu sita unageuza mkia
 
Orlando Pirates, Pyramids,Berkana,Tp Mazdmbe,Al Masry, sawa mchambuzi mtachukua Ubingwa.
Simba wanaweza kuteswa na TP Mazembe pekee kwenye michuano hii wakiwa sawa kwa kila idara.

Ila mechi ya Berkane ilituexpose weakness zetu kwenye aerial balls na set pieces ikiwemo kuwa na squad ambayo kama wachezaji wako wawili tu wakipata shida the whole squad inakuwa in shambles.
 
sawa mtabeba ubingwa, tuko tunalisubiri ilo kombe
 
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022

Simba imeonekana kuwa bora sana kwenye mechi 3 hizi za mwanzo ambapo imekuwa timu pekee katika kundi D kupata walau point ugenini na hii inatoa ishara kubwa kuwa huenda simba akamaliza kundi hili akiwa kileleni na kutinga hatua ya robo fainali

Kwa namna nilivyoziangalia timu shiriki za michuano hii ni wazi simba ana nafasi kubwa si ya kupita tu hatua ya robo fainali bali hata nusu fainal hali itakayopelekea kuingia fainali ya michuano hii na kubeba taji hilo kwa mara yao ya kwanza.

Simba kiuchezaji ina imarika kila siku benchi la ufundi linafanya kazi kubwa sana hivyo mpira watakaoucheza robo na nusu fainali utawashtua watanzania wengi hasa waliodhani labda simba imeshuka makali yake.

Tuendelee kusubiri muda lakini kwa zaidi ya 90% simba anaenda fainali ya hii michuano na kwa 60% atabeba hii ndoo kwa mara ya kwanza na kusimika rasmi ubabe barani afrika huku tukilielekea kombe la klabu bingwa barani afrika msimu unaofuata

View attachment 2135697
View attachment 2135698
View attachment 2135699
KAKA UMEWAONA VIGOGO LAKINI? MAZEMBE, ORLANDO PIRATES,AL MASRY, PYRAMIDS,AL ITTIHAD?
 
Simba mwaka huu wangefika mbali sana kwenye Shirikisho lakini kitachakachowaangusha ni safu yao ya ushambuliaji. Hata kama watavuka hatua hii ya makundi bado kuendelea mbele zaidi itakuwa ngumu sana. Na hii hata kwenye NBC ligi imeshawagharimu na itaendelea kuwagharimu sana na pia itamrahisishia sana Yanga kubeba ndoo kilaini. Na huu ni ukweli mchungu ambao wanasimba wengi hawataki kuukubali mpaka sasa lakini ndio uhalisia wenyewe.

Kwa mtu aliyeitazama mechi ya juzi na Berekane kwa umakini ni lazima atakuwa ameona jinsi fowadi ya Simba inavyotaabika. Boko hata kukaa na mpira dakika moja wenzake wafike hawezi na akituliza mpira "control" chumba na sebule. Anapigiwa pasi beki wa Berekane anatoka nyuma yake anawahi mpira kabla yeye haujamfikia. Mugalu naye amekuwa na majeruhi ya mara kwa mara na hata akiwa mzima anakosa magoli ya wazi kabisa. Kagere ndiyo hivyo tena hatabiriki leo anacheza vizuri anafunga mechi ijayo anazurura tu uwanjani mpaka mpira unaisha.

Iwapo Simba ingekuwa na fowadi imara hata ile mechi ya Gendamarie wangeshinda ugenini na si kupata sare. Kwa hili Simba wapate funzo na waanze maandalizi mapema kwa kuanza kutafuta washambuliaji kwa ajili ya msimu ujao. Na wanatakiwa wafanye maamuzi magumu kweli kweli kuhusiana na safu yao ya ushambualiaji.
Ndoo atayobeba yanga ina thamani kuliko ile ya kutinga robo fainali kombe la shirikisho Afrika?
 
Kulingana na ubora walio uonyesha klabu ya simba katika mechi hizi 3 za hatua ya makundi ya Caf confederation cup ni wazi vigogo hawa wa soka la afrika huenda wakaenda kutwaa taji hilo kubwa afrika msimu huu 2021/2022

Simba imeonekana kuwa bora sana kwenye mechi 3 hizi za mwanzo ambapo imekuwa timu pekee katika kundi D kupata walau point ugenini na hii inatoa ishara kubwa kuwa huenda simba akamaliza kundi hili akiwa kileleni na kutinga hatua ya robo fainali

Kwa namna nilivyoziangalia timu shiriki za michuano hii ni wazi simba ana nafasi kubwa si ya kupita tu hatua ya robo fainali bali hata nusu fainal hali itakayopelekea kuingia fainali ya michuano hii na kubeba taji hilo kwa mara yao ya kwanza.

Simba kiuchezaji ina imarika kila siku benchi la ufundi linafanya kazi kubwa sana hivyo mpira watakaoucheza robo na nusu fainali utawashtua watanzania wengi hasa waliodhani labda simba imeshuka makali yake.

Tuendelee kusubiri muda lakini kwa zaidi ya 90% simba anaenda fainali ya hii michuano na kwa 60% atabeba hii ndoo kwa mara ya kwanza na kusimika rasmi ubabe barani afrika huku tukilielekea kombe la klabu bingwa barani afrika msimu unaofuata

View attachment 2135697
View attachment 2135698
View attachment 2135699
Ile Kauli ya yule Mtaalam wa Afya ya Akili aliyosema kuwa kwa sasa Wagonjwa wa Akili na Vichaa ( Psychopath Case ) inaongezeka kwa Kasi nchini Tanzania hata Mimi kupitia Uzi huu ( Mada hii ) naanza Kumuelewa na Kuiamini 100% pia.
 
Mbona sikuelewi tena mkuu

Wewe ni shabiki wa simba kweli?
 
We dogo shida yako ni kujifanya unajua kila kitu, nadhani ufukara unakutesa.
 
We dogo shida yako ni kujifanya unajua kila kitu, nadhani ufukara unakutesa.
Majibu yako....

1. Kuhusu kujifanya Kwangu kuwa najua Mambo nengi au nina Akili tafadhali peleka upesi Malalamiko yako kwa Mwenyezi Mungu ya kwanini amenibariki Mimi hivi na Wewe akakuacha na huo Upumbavu, Wivu na Chuki dhidi yangu.

2. Kuhusu Mimi kuwa Fukara ( Masikini ) nakukubalia tena kwa 100% na wala hujakosea. Yawezekana Wewe ni Mgeni nami hapa Jamiiforums kwani mara kwa mara nimeshaweka wazi kuwa Mimi GENTAMYCINE ni Mtu Masikini kuliko Members wote hapa na wala sina mbele wala nyuma japo bado naendelea Kupambana na sijakata Tamaa nikiamini kuwa Siku moja isiyo na Jina Mungu huyo huyo aliyekupa Wewe Utajiri mpaka Unatudharau wengine kwa Kutuita Mafukara ndiyo huyo huyo atanibariki Mimi kwa Utajiri na mara zote nimekuwa nikisema kuwa nikibarikiwa huo Utajiri basi nataka niwe nasaidia Watu mbalimbali wenye Shida, Dhiki na Matatizo kwani hata Mimi nimeyapitia na ninayaishi kwa sasa hayo Maisha.

Mwisho nakuacha na hili Swali Kwako na kwa niaba ya Wapumbavu Wenzako wote hapa kuwa hivi baada ya kujua Mimi GENTAMYCINE najifanya Nina Akili, nataka Sifa na mkinituhumu na Mambo mengine kibao tu ni kwanini bado mnaendelea Kusoma Mada zangu Kutwa mnapo Log In tu hapa Jamiiforums? Kwani Members ambao mnawapenda na wanaandika yale muyatakayo hawapo au wameisha? Huwa nawalazimisha mnisome na mnifuatilie 24/7 hapa?

Mimi ndiyo GENTAMYCINE kudadadeki.
 
Mbona sikuelewi tena mkuu

Wewe ni shabiki wa simba kweli?
Kwahiyo uthibitisho wangu Kwako wa Mimi kuwa mwana Simba SC ni kuwa Mnafiki kama Wewe ( Nyie ) na Kusifia Upuuzi na kuwa Wapumbavu kama mlivyo wengi Wenu?
 
Simba imekuwa bora au Manula kawa bora? Mechi ya USGN simba walikuwa wanafungwa goli 2+ mechi dhidi ya Berkane walikuwa wafungwe 5+ ila Manula kafanya kazi ya ziada kusahisha makosa yaliyofanywa na wachezaji wake. Bado timu inafanya makosa mengi mno, spidi hakuna, mpira wa counter attack ni moja ya weakness ya Simba.

Unaposema timu bora umeitumia gizezo gani kuipima kwa performance au umepima kwa matokeoa?

Je kama umetumia muda wako kufatilia timu zote zinashiriki michuano hii mechi zao ili kuweza kujua uwezo wao?
Kazi ya kipa ni nini?
 
Back
Top Bottom