Utabiri: Maono na mwenendo wa yatakayo tokea mwaka 2018 tukumbushane tukio moja moja kila litakapojiri

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Habari heri ya mwaka mpya wanajamii

Kuna mambo ambayo yatatokea mwaka 2018,
1.Safari ya Kwanza ya nje ya bara la Africa ya mheshimiwa Magufuli,
2. Watu wa karibu wa Magufuli watamwangusha kiutendaji, wale aliowa amini wataonekana katika kashfa ambazo si rahis kuzimezea
3. Miez minne ya mwanzo itakuwa migumu mnoo, lakin kuanzia mwezi wa tano Magufuli atalegeza Sana maana malengo yake yatakuwa yamekaribia kukamilika ya kuinyoosha Tanzania,
4. Mwaka 2018 ni Neema Kwa bwana Khamis Kagasheki, Mrisho Gambo, Makongoro Nyerere, Nape Nnauye,
Lakin pia unaweza kuwa mbaya Kwa Paul makonda, Na bwana Nyalandu, Edward Lowassa,

5. Kunaweza kutokea msiba wa mtu mkubwa serikalini au aliyewahi kuwa mkubwa serikalini au mke wa aliyewahi kuwa mkubwa serikalini,

6. Kutakuwepo uhusiano mzuri na mataifa ya Africa kusini, Canada na kwingineko lakin Rwanda tunaweza ingia nao msuko suko mkubwa

7. Miradi mikubwa itaanza na wawekezaji watakuja Kwa wingi mwaka huu na watakubaliana na serikali katika masharti,

8. Kudhoofika Kwa vyama vya upinzani vya siasa, hata CCM itadhoofika Kwa kuwa na na nidhamu ya Unafiki juu ya mwenyekiti wao, hatapata washauri wazuri, maana wanamuogopa, Ila cha kusikitisha Zaid tutaipoteza nguvu ya Chadema,

9. Vyombo vya habari vitatiwa msuko suko Sana na vitaandika Kwa nidham ya uoga,

10. Kuna watu maarufu watastaafu siasa na kuenda kupumzika kama kina Bernard na wengine kina Mwandosya,

11. Uteuzi utaegemea Zaid jeshi

12. Tanzania itatuhumiwa kurejesha hatua za maendeleo ya shirikisho la Africa mashariki, Kwa kukosa itiyari wa maamuzi muhimu,

13. Pole Sana Diamond Platinum kwa mwaka 2018 , si mwaka wako,

14. Nilitaka kuzungumza juu ya Ben saanane Ila sisemi Jambo, Ila 2018 itasema,

15. Pole Sana mbowe mambo si mazuri kwako mwaka huu, kuna watakaokupinga ndani ya chama,

We mwanafalsafa unaona nini??
 
OK Mimi tunguli zangu zinaonyesha yafuatayo
. Lissu atarejea Bongo akiwa Salama na Bunge litajifanya kumuonea huruma na kumjali
- Serikali itajifanya kumaliza kesi feki dhidi ya Lissu
- Watu Watapata ujasiri zaidi wa kusema wazi wazi na Sio Kwa kificho tena
- Vifo vingi Sana vya akina Mama Wajawazito, TB na Ukimwi vitaongezeka saaana na taarifa sahihi hazitapatikana kwa kuogopa kuchukuliwa hatua
- Kutapatikana Upinzani wa kweli, WA wazi na WA watu wasio waoga.
- Bunge kwa kutumia wingi WA CCM watapitisha kipengele cha kuongeza ukomo wa Urais, hoja itapelekwa na Kikundi cha Wana CCM maslahi
- Wakurugenzi na Ma-DC wengi watafukuzwa kazi kwa kisingizio cha kushindwa kumudu kasi ya Nanihii
- Mchakato wa Katiba Mpya utazikwa rasmi
- Wawekezaji ambao ni Potential watazidi kuondoka na kubaki Wachina
- Viwango vya Elimu vitazidi kushuka
- Watu watazidi kufungwa kwa kesi hewa na maiti zitazidi kuokotwa bila maelezo
- Jeshi la Polisi litazidi kudhoofu kuliko nyakati zozote zile
 
nasubiri kushuhudia........................................................................................
 
Miezi mitatu ya mwanzo kutakua na Reshuffle ya baraza LA mawaziri..

-Wakuu Wa mikoa maarufu Wa tatu wataondolewa

- Wateule wake waliokua kambi tofauti wakati Wa uvhaguzi Wa ndani Wa ccm atawafuta rasmi kazi
 
Kumbe
 
OK Mimi tunguli zangu zinaonyesha yafuatayo
. Lissu atarejea Bongo akiwa Salama na Bunge litajifanya kumuonea huruma na kumjali
- Serikali itajifanya kumaliza kesi feki dhidi ya Lissu
- Watu Watapata ujasiri zaidi wa kusema wazi wazi na Sio Kwa kificho tena
- Vifo vingi Sana vya akina Mama Wajawazito, TB na Ukimwi vitaongezeka saaana na taarifa sahihi hazitapatikana kwa kuogopa kuchukuliwa hatua
- Kutapatikana Upinzani wa kweli, WA wazi na WA watu wasio waoga.
- Bunge kwa kutumia wingi WA CCM watapitisha kipengele cha kuongeza ukomo wa Urais, hoja itapelekwa na Kikundi cha Wana CCM maslahi
- Wakurugenzi na Ma-DC wengi watafukuzwa kazi kwa kisingizio cha kushindwa kumudu kasi ya Nanihii
- Mchakato wa Katiba Mpya utazikwa rasmi
- Wawekezaji ambao ni Potential watazidi kuondoka na kubaki Wachina
- Viwango vya Elimu vitazidi kushuka
- Watu watazidi kufungwa kwa kesi hewa na maiti zitazidi kuokotwa bila maelezo
- Jeshi la Polisi litazidi kudhoofu kuliko nyakati zozote zile
Hahaha tunguli zako balaa
 
1.Wakuu wa Wilaya kubadilishwa,
2.Wakurugenzi wa Halmashauri kubadilishwa, ili kulenga uchaguzi 2019,na 2020.
 
BREAKING NEWS: Mke wa Kingunge afariki Dunia

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

[HASHTAG]#Kujipatia[/HASHTAG] Taarifa, Makala mbalimbali ,,Fanya Hivi ,,[HASHTAG]#Nifollow[/HASHTAG] ktk Ukurasa Wangu wa Facebook au Nitumie ombi la Urafiki.
 
Tutaona mengi mwaka huu

Back
Top Bottom