singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WANASIASA nchini Uswisi wamepitisha sheria ya kuwalipa fidia waliokuwa watoto waliotumikishwa kazi ngumu wajulikanao kama Verdingkinder.
Chini ya sheria ambazo zilikuwapo hadi miaka ya 1980, maafisa waliwachukua watoto kutoka familia masikini, yatima, watoto waliozaliwa nje ya ndoa, ambao wazazi wao walikuwa walevi au walitengana na kuwalazimisha kufanya kazi ngumu za sulubu.
Katika jitihada za kujaribu kukabili moja ya doa kubwa katika historia ya Uswisi, juzi Bunge liliidhinisha fidia kwa maelfu ya watu ambao walitenganishwa na familia zao wakiwa watoto.
Serikali ina mipango ya kutumia Faranga milioni 308 za Uswisi kuwalipa fidia kati ya waathirika 12,000 hadi 15,000 ambao bado wako hai.
Kila mmoja atapokea kati ya Faranga 20,000 hadi 25,000. Faranga moja ya Uswisi ni sawa na Sh 2,270 za Tanzania.
Maoni yangu
hii isiishie kwa raia waliopo uswisi tu pekee yake, Mabeberu walitesa mababu zetu kwa kuwafanya watumwa katika nchi zao, ifikie hatua nchi zote zilizoshiriki biashara ya watumwa kuanzia muuzaji na mnunuzi wazilipe fidia nchi za afrika zilizoathirika na biashara hiyo utumwa.
Kuna haja kwa AU kwa pamoja itoe tamko la kuzitaka nchi zilizohusika na biashara hiyo kulizipa nchi waathirika na kulisimamia vema suala hilo