Usumbufu TRA bandarini, tunaweza kufanya nini?

Kagalala

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
2,403
1,132
Ndugu wana JF, kama kuna kitu ambacho kweli ninachngia sana kurudisha maendeleo ya Tanzania nyuma ni usumbufu na utirtimba uliopo hapo TRA (Customs). Ukitaka kujua kwamba Tanzania tutachukua miaka mingi kuendelea jaribu kuingiza bidhaa kutoka nje kupitia bandari ya Dar es Salaam. Kwa kweli hawa jamaa wanaohusika na kutoa mizigo bandarini ni wasumbufu na wanakatisha tamaa kwa mtu anayejaribu kujikwamua na maisha duni. Kwa wastani kuanzia siku meli inaingia mpaka upate kutoa container lako ni week tatu nazaidi.
Sisi kama wananchi na wafanya biasharawadogo wadogo tunaweza kufanya nini kurekebisha hali hii. Naomba maoni yenu.
 
umenikumbusha kuna jamaa aliagiza CAT Excavator halafu THA wakapoteza funguo zake...kazi kweli kweli
 
Nilikuwa najua watu wakiagiza magari wako radhi kupitia Bandari ya Kisumu, ili waingilie Sirari mpaka Mwanza, kuliko huu ujinga wa TRA..., lakini ukisema TRA pekee unawaonea.., bongo sekta zote zimeoza.., kuanzia juu mpaka chini, hii nchi ilishakosa DIRA kuanzia zamani ni mpaka sasa tumeshapotea na hatujui ni wapi tunakwenda
 
Kweli kabisa tatizo la hii nchi ni kwamba tulowapa madaraka ya kusimamia mambo yetu wamekuwa goigoi na hawajui wanatakiwa kufanya nini.... nadhani umefika muda sasa tuwapumzishe na tubadili hii system ya kizembe!!!:twitch:
 
Nilikuwa najua watu wakiagiza magari wako radhi kupitia Bandari ya Kisumu, ili waingilie Sirari mpaka Mwanza, kuliko huu ujinga wa TRA..., lakini ukisema TRA pekee unawaonea.., bongo sekta zote zimeoza.., kuanzia juu mpaka chini, hii nchi ilishakosa DIRA kuanzia zamani ni mpaka sasa tumeshapotea na hatujui ni wapi tunakwenda

I just hate dealing with any Govt official!!!
 
Nilimsikia mtaalamu mmoja akiongea pahali fulani akisema bandari za tanzania zingeweza kuendesha serikali ya tanzania bila ya kuomba msaada nchi za nje! Bandari tu! Lakini tatizo zinaendeshwa kisiasa mno! Akasema mtwara ina kina kirefu cha kuweza kutia nanga meli zote kubwa duniani. Ina kina cha asili. Naomba kusahihishwa.
 
Tumezungukwa na Land Locked Countries, nchi zote kama Rwanda, Burundi, Zambia n.k. tungeweza kupata pesa kutoka kwao kila wakileta mizigo.., Sasa iwapo Mtanzania mwenyewe wa Mwanza yupo radhi achukulie mizigo yake Kisumu..., Unategemea hawa majirani zetu watakubaliana na huu Upuuzi.

Lazima tukubaliane kuna tatizo kubwa sana na vichwa vyetu watanzania
 
Umewahi kujiuliza, hizo bandari zingekuwa zinamilikiwa na Wazungu hata kwa miaka 20 tu, zingekuwaje? Mimi naamini zingekuwa nzuri zaidi na huduma bora. Ni kweli tuna matatizo fulani.
 
Nilishawahi kuongea na mtu kutoka Canada alisema yaani maliasili za kanda ya ziwa tu.., zingeweza kulisha Tanzania nzima, yaani kwakweli ni aibu kuona jinsi tunavyoteseka bila sababu... Tena sometimes inabidi tuwashuru wakoloni sababu bila wao hata hizo reli huenda zingekuwa hazipo...

"In abundace of Water A Fool is Thirsty" Bob Marley
 
I like the quote from Robert Marley...,
and then I'm disappointed...
Katika Africa hakuna nchi iliyozungukwa na maji kama Tanzania., Rivers by its boarders, Freshwater lakes, ocean...
Halafu watu bado wananunua maji kwenye vidumu...
 
Hivi hiyo TRA ina viongozi kweli?? na kama yupo anaitwa nani!? hii kitu ni kero sana! wana nikera wana nikera wana nikera! i hate to say that!na wamenipa hasara sana pale Bandarini Dar! what a bunch of crappy service providers. Every time when i think or hear about TRA i feel so ashamed of being a Tanzanian.
 
Nilikuwa najua watu wakiagiza magari wako radhi kupitia Bandari ya Kisumu, ili waingilie Sirari mpaka Mwanza, kuliko huu ujinga wa TRA..., lakini ukisema TRA pekee unawaonea.., bongo sekta zote zimeoza.., kuanzia juu mpaka chini, hii nchi ilishakosa DIRA kuanzia zamani ni mpaka sasa tumeshapotea na hatujui ni wapi tunakwenda
Mimi siju hata ni seme nini, natamani kutoa machozi kabisa.Jamani hivi ni nani aliyeturoga wa TZ!!!.
 
Hivi hiyo TRA ina viongozi kweli?? na kama yupo anaitwa nani!? hii kitu ni kero sana! wana nikera wana nikera wana nikera! i hate to say that!na wamenipa hasara sana pale Bandarini Dar! what a bunch of crappy service providers. Every time when i think or hear about TRA i feel so ashamed of being a Tanzanian.
mombasa bandari is the best, better! hawana usumbufu as longer as ur papers are correct! mimi huwa Bandari ya dar siitrumii tena, wamoeza oza wote! wanatia kichefuchefu! wamerudisha sana maendeleo ya nchi yetu since we have no kiongozi.
 
Nilikuwa najua watu wakiagiza magari wako radhi kupitia Bandari ya Kisumu, ili waingilie Sirari mpaka Mwanza, kuliko huu ujinga wa TRA..., lakini ukisema TRA pekee unawaonea.., bongo sekta zote zimeoza.., kuanzia juu mpaka chini, hii nchi ilishakosa DIRA kuanzia zamani ni mpaka sasa tumeshapotea na hatujui ni wapi tunakwenda

Bandari ya Kisumu mmmhh hii imekaaje lakini jamani? ama ulimaanisha Mombasa?
 
Tatizo siyo bandari ya Dar-es-salaam,kazi ya Bandari ni Kupakua na kupakia mizigo.
Tatizo lipo TRA ktk kukadiria kodi ya mteja.hakuna formula maalum.nimeagiza gari mbili zote zinafanana mwaka,model ,uzito etc.zimekuja na meli tofauti kwa kupishana miezi 2,ya kwanza kodi nililipia milioni 3.4 ,ya pili nikabadirisha Agent(msichana this time),kodi ikashuka kuwa milioni 2.6. tofauti ya laki 800,000/- ,
hapo ni dhahiri kuwa TRA hamna forumula wala utaratibu wa kueleweka.
TRA wanasababisha msongamano wa mizigo bandarini,kuchelewesha wateja kutoa mizigo,kupandisha kodi kiholelela (wanaita Uplifting).

Solution:
kushinikiza wabunge kuwa reli ifanye kazi kwa kutoa mizigo yote bandarini na kuipeleka kisarawe,hapo kuwe na yard kubwa -Dry port.then maafisa wa TRA wawe wanafanyia kazi huko huko,hapo tutaondoa msongamano bandarini,
2.Jinsi ya kukokotoa kodi iwe bayana.
3.mizigo ya wafanya biashara itenganishwe na mizigo ya mtu binafsi(personal effects)kwani wengi wa wanao pigwa kodi za ajabu ajabu ni watu binafsi,wafanya biashara huwa hawasumbuliwi na TRA kabisa.
 
Ninakuunga mkono kabisa bwana newmazalendo.
Huku ulaya mostly tunalipia kodi au ushuru kwenye internett au unaletewa bili nyumbani baada ya kuwapigia simu wahusika na kuwaelezea dhumuni lako. so simple kwani kila kitu kinajulikana bei yake, au asilima yake. Kama ulivyo sema hakuna formula. Ilitakiwa bidhaa ziwekwe kwa categories. na ikiwezekana ziandikwe kwenye webside ya TRA, kama utaleta gari utalipia vipi na kiasi gani, kama ni electronics, vifaa vya ujenzi, cosmetics, Ina maana kabla huja tuma kitu umesha jua bei ya kulipia.
Sasa suali bado liko pale pale, tufanye nini.
Watu wa TRA hawapendi kusika maoni kama haya. Kukisha kua na utaratibu mzuri inamaanisha hao TRA hawata pata mlo. Maana hapa kuna TRA, na kuna serekali na kuna wabunge wanao husika. Wote hao wana kula pammoja. Kwahiyo lazima wafanya biashara watafute mbinu sasa hivi. Tutumie sana internett kuweza kupata ideas, nafikiri kila mtu akitoa maoni ipo siku tutapa ufumbuzi.
Kwa kweli inatia aibu tanzania.
 
Ninakuunga mkono kabisa bwana newmazalendo.
Huku ulaya mostly tunalipia kodi au ushuru kwenye internett

Mkuu ukilinganisha na Ulaya utafanya watu wadhani kwamba hii issue ni complicated..., Hapo Kenya tu hakuna huu upuuzi kama wa hapa kwetu
 
Back
Top Bottom