Ustaarabu katika jukwaa hili ni muhimu

marveljt

JF-Expert Member
Jan 11, 2017
1,503
1,479
Wakati mwingine siyo lazima wote tuchangie kila mada. Unakuta mada ya mwanaume anatafuta mpenzi/ mchumba au mwanamke anatafuta mchumba na katika bandiko lake ameweka umri na vigezo. Wewe unajijua hukakidhi na pia amesema mwenye vigezo aende pm inakuwaje wewe unaanza kumponda huyo mtu? Je,wewe uko katika mpangilio wake wa maisha? Hata kama amekuja na miaka 35 kila mmoja anampangilio na maisha yake. Tuweke ustaarabu mbele ili kuweka heshima ya jukwaa. Hata kama tunatumia id fake ila ujinga wetu tuufiche
 
Back
Top Bottom