Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,439
Swaiba yangu alifikiria sana katika kuwekeza vitega uchumi. Yeye aliamua kujikita kwenye real estate. Huko nako aliwaza jinsi ya kupata kodi bila ya usumbufu hasa kwa usawa huu.
Aliamua kuwa na nyumba mbili si mbali sana na mji za kupangisha vyumba. Badala ya kuweka vyumba sita “I face you face me”yeye aliweka vyumba vinne vyenye chumba na sebule kwa bei ya 150,000 kwa mwezi.
Nyuma aliweka jiko la wote kila mtu alikua na meza yenye kabati lenye kufuli hivyo unaweza kununua jiko la gesi na ukafungia mtungi wako kabatini.
Vyoo viwili Indian toilets pamoja na vyumba viwili vya bafu ili iwe rahisi kwa wanao kwenda kazini asubuhi. Pia alitoa vyumba viwili uani kwa kodi ya 50,000 kila kimoja.
Kwa maji ya chooni alikinga maji ya mvua kwenye simtank, pia alipata maji ya DAWSCO.
Matatizo yanakuja kwenye vyoo kuziba, kila Akiita fundi kuzibua wanatoa vipande vya gazeti na sanitary towels.
Yaani amechoka kutoa elimu kwa wapangaji. Wengi wao hujitetea kuwa ni wageni wao. Sasa hata toilet paper au maji wanashindwa kutumia.
Uzuri wake ana uhakika wa 700,000 kila mwezi ila tabia za watu wengi ni shida kazi controll.