barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,945
That's coincidence.....haya mambo ya kutokuwa wawazi ktk mapenzi,mkiwa kitandani ni kama mnasali rozari na wife...hakuna uwazi,humwambii mkeo nini akufanyie,matokeo yake unachoweza kukipata kwa mkeo waenda kughalamia nje na kuhatarisha ndoa yako.
Hii imemtokea jamaa yangu,weekend kachomoka home,kaaga anaenda vikao vya harusi...kumbe mgongo unamuwasha anataka akafanyiwe massage,sasa bila kujua kuwa jirani na hiyo massage Parlour ni saloon mkewe hupenda kwenda kujipendezesha
Kidume kaenda,huku nyuma mke akang'oa nanga saloon...mke kufika maeneo anaona gari la mumewe limeegeshwa,mama akatia nanga kujua kulikoni...sbb ni mitaa yake ya saloon,tayari mama akawa na story na jinsi wanaume za watu huingia ktk parlour hiyo na kufanyiwa vituko baada ya massage na kula tunda...Huwa ndo story za hiyo saloon...kila mara akienda saloon huwashudia waume wa wengine na wasio waume wakitoka ndani kupata huduma ya viungo na extra
Mama akakaa zaidi ya masaa mawili....mara mume huyo katoka mwepesiii...timbwili la kufa mtu,mke mtu anapiga mayowe kuwa hajawahi kuombwa kutoa huduma ya massage akakataa,iweje mumewe akawavulie nguo wengine wakati mke yupo?...Mpaka sasa nyumbani hapakaliki,jamaa kaja kwangu anajutia kuwa wife kachachamaa hatari,hakuna amani mana wife amehitimisha kuwa jamaa ni mnunuaji".....ni timbwili ndani ya nyumba,ruba kaingia bwawani...