Uso kwa uso na Jambazi Sugu

Uso kwa uso na Jambazi Sugu

Jana mida ya saa 4 usiku wakati najiandaa kulala nikiwa katika wilaya ya Ngara katika baa moja ambayo pia ina nyumba ya kulala wageni niliingia chumbani kulala (Nipo hapa Kibiashara) saa 11 alfajiri ya leo niliamka ili kuwahi usafiri wa kwenda mpakani mwa Rwanda ambako huwa napeleka mchele kuwauzia wafanyabiashara wa Kigali, ile gest haipo self contained, kwa hiyo nilipoamka ilinipasa kwenda toilet kwanza, nilipotoka toilet mwili ulishikwa ganzi nilipomuona mwanaume mwenye miraba minne akiwa na bunduki ya kivita ambayo sikuweza kuitambua kama ni AK 47 au SMG.

Alikuwa akiikagua, aliponiona akahamaki na kuiweka ndani ya mfuko wa gunia huku akisema, ''Dogo nimekuona tangu jana baa unaonekana kiherehere sana, sasa ole wako uropoke Police kuwa eti umeniona na hii kitu, nitakuchinja njiani, we si Unaenda Rwanda? Utaona sasa''.

Siyo siri niliogopa kupindukia, na kweli jana pale baa nilimuona yule njemba wakati nikiwa na wenzangu na wengi pale walijua kuwa tunaenda wapi.

Kwa tabia za Police wa kibongo, siwezi kutoa taarifa, liwalo na liwe.
mlilalal room moja? manake unasema room ni self contained na ulipotoka chooni ukakutana naye...??????
 
Sasa mbona umeshatoa taarifa kwa police? au unadhani police hawapo humu?
 
Unajua maana na matumizi ya maneno 'jambazi sugu'?
 
Next time ukioniona sema shikamoo kaka jambazi kisha sepa kabla sijaitika, sawa?
 
Back
Top Bottom