Uso kwa uso na Jambazi Sugu

Uso kwa uso na Jambazi Sugu

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,550
Jana mida ya saa 4 usiku wakati najiandaa kulala nikiwa katika wilaya ya Ngara katika baa moja ambayo pia ina nyumba ya kulala wageni niliingia chumbani kulala (Nipo hapa Kibiashara) saa 11 alfajiri ya leo niliamka ili kuwahi usafiri wa kwenda mpakani mwa Rwanda ambako huwa napeleka mchele kuwauzia wafanyabiashara wa Kigali, ile gest haipo self contained, kwa hiyo nilipoamka ilinipasa kwenda toilet kwanza, nilipotoka toilet mwili ulishikwa ganzi nilipomuona mwanaume mwenye miraba minne akiwa na bunduki ya kivita ambayo sikuweza kuitambua kama ni AK 47 au SMG.

Alikuwa akiikagua, aliponiona akahamaki na kuiweka ndani ya mfuko wa gunia huku akisema, ''Dogo nimekuona tangu jana baa unaonekana kiherehere sana, sasa ole wako uropoke Police kuwa eti umeniona na hii kitu, nitakuchinja njiani, we si Unaenda Rwanda? Utaona sasa''.

Siyo siri niliogopa kupindukia, na kweli jana pale baa nilimuona yule njemba wakati nikiwa na wenzangu na wengi pale walijua kuwa tunaenda wapi.

Kwa tabia za Police wa kibongo, siwezi kutoa taarifa, liwalo na liwe.
 
Nani ambaye huwa yuko kusaidia polisi wa bongo kwa upelelezi ili uswekwe ndani. Heri ujinyamazie
 
Hadithi yako nzuri ila panga maneno weka koma na stop sijui ulikwenda shule


swissme
 
Wewe ni mtunzi mzuri sana, unaonaje ukiomba Column kwenye gazeti lolote la udaku? Utatengeneza pesa nyingi
 
Jana mida ya saa 4 usiku wakati najiandaa kulala nikiwa ktk wilaya ya Ngara ktk baa moja ambayo pia ina nyumba ya kulala wageni niliingia chumbani kulala (Nipo hapa Kibiashara) saa 11 alfajiri ya leo niliamka ili kuwahi usafiri wa kwenda mpakani mwa Rwanda ambako huwa napeleka mchele kuwauzia wafanyabiashara wa Kigali,ile gest haipo self contained,kwa hiyo nilipoamka ilinipasa kwenda toilet kwanza,nilipotoka toilet mwili ulishikwa ganzi nilipomuona mwanaume mwenye miraba minne akiwa na bunduki ya kivita ambayo sikuweza kuitambua kama ni AK 47 au SMG,alikuwa akiikagua,aliponiona akahamaki na kuiweka ndani ya mfuko wa gunia huku akisema😀ogo nimekuona tangu jana baa unaonekana kiherehere sana,sasa ole wako uropoke Police kuwa eti umeniona na hii kitu,nitakuchinja njiani,we si Unaenda Rwanda? Utaona sasa.Siyo siri niliogopa kupindukia,na kweli jana pale baa nilimuona yule njemba wakati nikiwa na wenzangu na wengi pale walijua kuwa tunaenda wapi,kwa tabia za Police wa kibongo,siwezi kutoa taarifa,liwalo na liwe.
Mbona umeropoka, jamaa yuko humu JF,atakumaliza.
 
Hata mi nimeogopa maana NGARA kuna silaha nyigi sana na wezi ni wengi si mchezo
Sema hawa watoto wa humu jf kula kulala hawawezi kukuamini
 
Ulijuaje kama ni jambazi sugu na siyo kaka jambazi wa kawaida?
 
Maeneo mengi yaanayopakana na nchi jirani sio salama. Ndio maana kuna muda ukifika huwezi kuvuka barabarani kizuizi cha Polisi kwa kuwa hali ya usalama hairidhishi.
 
Ulijuaje kama ni jambazi sugu na siyo kaka jambazi wa kawaida?

Hii issue serious, usilete jokes za jitoto, silaha haramu zinauzwa burundi kama njugu. Zimetapakaa ngara. Hili tukio litakuwa la kweli
 
Ngara isikieni humu kwenye JF, sifikirii wala kutamani kurudi tena kule! Huyu mnaweza kusema anazungumza hadithi, sisi tulioneshwa mitutu ya bunduki tukiwa grocery na tukaambiwa tukae kimya!
 
Jana mida ya saa 4 usiku wakati najiandaa kulala nikiwa katika wilaya ya Ngara katika baa moja ambayo pia ina nyumba ya kulala wageni niliingia chumbani kulala (Nipo hapa Kibiashara) saa 11 alfajiri ya leo niliamka ili kuwahi usafiri wa kwenda mpakani mwa Rwanda ambako huwa napeleka mchele kuwauzia wafanyabiashara wa Kigali, ile gest haipo self contained, kwa hiyo nilipoamka ilinipasa kwenda toilet kwanza, nilipotoka toilet mwili ulishikwa ganzi nilipomuona mwanaume mwenye miraba minne akiwa na bunduki ya kivita ambayo sikuweza kuitambua kama ni AK 47 au SMG.

Alikuwa akiikagua, aliponiona akahamaki na kuiweka ndani ya mfuko wa gunia huku akisema, ''Dogo nimekuona tangu jana baa unaonekana kiherehere sana, sasa ole wako uropoke Police kuwa eti umeniona na hii kitu, nitakuchinja njiani, we si Unaenda Rwanda? Utaona sasa''.

Siyo siri niliogopa kupindukia, na kweli jana pale baa nilimuona yule njemba wakati nikiwa na wenzangu na wengi pale walijua kuwa tunaenda wapi.

Kwa tabia za Police wa kibongo, siwezi kutoa taarifa, liwalo na liwe.

Bora ulikaa kimya, huwezi jua ananetwork kiasi gani hapo alipo unaenda kurepot anambiwa akukabidhi wewe hiyo silaha inakuwa yako. Kitachofuata ni jela miaka 30.
 
Jana mida ya saa 4 usiku wakati najiandaa kulala nikiwa katika wilaya ya Ngara katika baa moja ambayo pia ina nyumba ya kulala wageni niliingia chumbani kulala (Nipo hapa Kibiashara) saa 11 alfajiri ya leo niliamka ili kuwahi usafiri wa kwenda mpakani mwa Rwanda ambako huwa napeleka mchele kuwauzia wafanyabiashara wa Kigali, ile gest haipo self contained, kwa hiyo nilipoamka ilinipasa kwenda toilet kwanza, nilipotoka toilet mwili ulishikwa ganzi nilipomuona mwanaume mwenye miraba minne akiwa na bunduki ya kivita ambayo sikuweza kuitambua kama ni AK 47 au SMG.

Alikuwa akiikagua, aliponiona akahamaki na kuiweka ndani ya mfuko wa gunia huku akisema, ''Dogo nimekuona tangu jana baa unaonekana kiherehere sana, sasa ole wako uropoke Police kuwa eti umeniona na hii kitu, nitakuchinja njiani, we si Unaenda Rwanda? Utaona sasa''.

Siyo siri niliogopa kupindukia, na kweli jana pale baa nilimuona yule njemba wakati nikiwa na wenzangu na wengi pale walijua kuwa tunaenda wapi.

Kwa tabia za Police wa kibongo, siwezi kutoa taarifa, liwalo na liwe.

kumbe ulitembea na mke wa hyo jambazi(mkurya) temana na hizo mambo mkuu noma,njamaa angekuua!
 
Back
Top Bottom