Usiyoyajua kuhusu Che Guevera

kabla sija uwendea huu uzi nakushukuru sana mkuu kuleta huuzi tena inabidi niache hata kula nipae nao[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Na upi ukweli kuhusiana na kugeukana baina ya Che Guevara na Fidel Castro baada ya kushika madaraka ya Cuba...?
Niliisoma sehem ila ilikuwa kifupi mno.
Hakuna aliyemgeuka mwenzake, Che Guevara alimtaka Komredi Fidel Castro awe Kiongozi wa Cuba punde tu baada ya Mapinduzi matukufu ya 1959.

Che Guevara alikuwa na majukumu ya kwenda Nchi nyingine kwa ajili ya kufanya ukombozi. Kazi aliyoifanya Cuba ilimtosha hivyo hakutaka wadhifa wowote.

Ila fitna za madaraka, ziliwagombanisha Komredi Fidel Castro na Mwanamapinduzi mwingine wa Cuba, Huber Matos kiasi cha Fidel Castro kumweka Kizuizini Huber Matos.

Ugomvi wa Fidel Castro na Huber Matos ulisababisha kifo tata cha Mwanamapinduzi mwingine Camilo Cienfuegos ambaye baada ya kutumwa na Castro kwenda kumkamata Huber Matos, ndege aliyopanda Camilo wakati akirejea jijini Havana ilipotea na haikuwahi kuonekana tena licha ya kutafutwa kila kona.

Maneno yalizuka kuwa ndege aliyopanda Camilo Cienfuegos itakuwa imelipuliwa na ndege vita za Cuba kwa amri ya Fidel Castro. Che Guevara alijitokeza kupinga tetesi hizo za kuuwawa kwa Camilo na uwepo wa uhusika wa Castro katika sakata hilo.

Kwa leo niishie hapo!!
 
Daaa..yaani hapo ndo huwa ninakumbuka Maneno ya marehemu Remmy "kifoooo...kifoooo...kifo hakina huruma".

Yaani komando na mpiganaji mahiri kabisa anakuja kuuwawa kizembe zembe tena na "askari chapombe". Inasikitisha sana...we kifo huna adabu kabisa.
 
Daaa..yaani hapo ndo huwa ninakumbuka Maneno ya marehemu Remmy "kifoooo...kifoooo...kifo hakina huruma".

Yaani komando na mpiganaji mahiri kabisa anakuja kuuwawa kizembe zembe tena na "askari chapombe". Inasikitisha sana...we kifo huna adabu kabisa.
Kasome historia yake vizuri mkuu
 
aaaaah mkuuu vipiii[emoji122] [emoji122] unamlambisha mtu asali alafu hapo hapo una mwambia tema mate jamanii [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hiyo familia kumuona che guevara kama gaidi ni haki yao maana viongoz ambao walikua madikteta uchwara walikua ni familia zao pia,

Lakn haibadilishi maana na heshima ya guevara kwa kusaidia kutokomeza ubepari,

Hata leo hii unafikir familia ya mzee wa vijisenti inamuonaje mzee wao....wanamuona yupo safi na akihukumiwa watamlaani aliewahukumu.

Che Guevara was a true leader.
 
Na upi ukweli kuhusiana na kugeukana baina ya Che Guevara na Fidel Castro baada ya kushika madaraka ya Cuba...?
Niliisoma sehem ila ilikuwa kifupi mno.
Yaah Che Guevara walitofautiana misimamo na Fidel Castro kipind fulani wakati Guevara akiwa waziri ktk serikali ya Castro.....

Guevara alikuwa hakubaliani na sera marekanj hivyo aliwachukia sana na Castro alikuwa hana msimamo ya hilo, hvyo Guevara akaomba aache uongozi akaona bora aende kuendelea kusaidia mapinduzi ktk nchi zingine japo Castro alimsihi sana asiondoke....mwisho alimkubalia na kumruhusu.

Kwa ufupi nimejaribu kuelezea.....ukipata kitabu utaelewa zaidi.
 
Hata hi Leo wapo ila sasa kuna mbinu mpya na za kileo mapigano ya waasi Wa congo yanafadhiliwa, Sudan kusini Na kwengineko kwa mbinu mbadala na huo alotumia Che Guevara Wa kupigana bega kwa bega na anaowasaidia, na ya sasa hivi ni mabaya zaidi
WA sasa hivi hawapoganii maisha ya watu wanyonge bali wanafadhiliwa ili wapore mali za nchi na madaraka.
 
Aisee kuna baadhi ya binadamu wanaumea kwa sababu ya maisha duni wanayoishi wengine

kuna watu wanaandika majina yao vizuri kama CHE GUEVARA na wengine wanaandika majina yao vibaya kama HITLER
Mkuu hitler wajerumani na dunia ndio hawataki mwelewa ila ilichangia kwa kiasi kikubwa ecomic reform za ujeruman pamoja na kupunguza kama c kumaliza un employment
 
Hivi siku hizi wapo wanamapinduzi wa aina ya Che? Maana nchi nyingi zimeshaweka kando Ujamaa/Ukomunist!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…