Usiwaze sana kuhusu kesho yako

Mosalah_

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
314
720
Habari wana JF,

Naimani mpo poa sana kama haupo poa basi mungu akutie nguvu urudi kwenye ubora wako.

Ujumbe huu nawatumia wote Wana-JF iwe Mwanasiasa, Daktari, Muuza Mkaa, tajiri na masikini na watu wa hali ya kati.

Watu tuna pressure sana ya maisha mambo ni mengi sana, huyu anawaza kupandishwa cheo kazini, huyu anawaza apone ugonjwa unao msumbua kwa muda mrefu, huku ana haso kununua I phone 15, uyu anawaza kujenga nyumba, uyu anawaza kuwapeleka watoto wake wakasome nje, huyu anataka kuolewa.

Yote hayo ni mazuri sana ila mpangaji wa kila kitu ni mungu, kwenye kila jambo unalofanya tegemea matokeo mawili kufanikiwa au kutofanikiwa namaana fanya vitu kwa uwezo wako wote lakini usipo fanikiwa elewa ni sehemu ya matokeo.

Hii kanuni itakufanya kutokuwa na vinyongo au makunyanzi kwenye moyo wako kabisa , utakuwa mwepesi kuwapigia makofi walio fanikiwa na kuwa na upendo kwa wanao kuzunguka.

Hivyo ndugu yangu usiwaze sana kuhusu kesho yako fanya kwa uwezo wako ikishindikana sawa ikiwezekana alhamdulillah.

Uwe na siku njema mwana JF.
 
Mungu huyo ndio anafanya watu wasifanikiwe?

Yeye si ni mpangaji wa kila kitu.

Kwa hiyo mtu asipo fanikiwa ni mipango ya Mungu?

Basi huyo Mungu ana mipango dhaifu ya kufelisha watu.
 
Back
Top Bottom