Usiuze amali (assets) kabla ya kuwa na mpango mahsusi

Usiuze amali (assets) kabla ya kuwa na mpango mahsusi

Maisha yanatupa nafasi ya kufanya maamuzi kila siku. Tunafanya maamuzi juu ya kila kitu kinachotuzunguka. Tunaamua muda wa kuamka na muda wa kulala, nini tufanye na nini tusifanye… Karibu kila wakati tunajikuta tunahitajika kufanya maamuzi. Kwa kiasi kikubwa, tuko jinsi tulivyo ni kutokana na maamuzi tunayoyafanya.

Umewahi kumiliki amali (asset) yoyote na ukalazimika kuiuza kutokana na sababu yoyote? Mfano, unaweza kuwa na kiwanja, nyumba, gari, redio, kitanda, kochi, simu, laptop, jokofu, vyombo vya ndani, nguo au kingine chochote kama hivyo. Wakati Fulani, unaweza kujikuta unalazimika kuuza mojawapo kati ya vitu hivi kwa sababu mbalimbali kama vile kukwama kiuchumi, kuhitaji fedha ya kukabiliana na dharura kubwa (msiba, ugonjwa, sherehe n.k), kuhitaji kubadilisha aina ya amali (kupata iliyo bora Zaidi), kuhamisha makazi, kupunguza idadi ya amali na sababu nyingine nyingi.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi unapouza amali fulani, haiwi rahisi kununua tena amali hiyo!!! Hata pale unapofanikiwa kununua, huenda isiwe tena ya ubora na/au viwango vya amali iliyouzwa awali.

Mathalani, binafsi niliwahi kuuza shamba eneo ambalo sasa ni katikati ya mji kabisa. Wakati nauza eneo lile, nililiuza kwa shilingi milioni nne hivi. Lakini miaka sita baadae, eneo lile lile limekuwa na thamani ya Zaidi ya mara kumi!! Kwa kiasi kile kile ambacho niliuza, leo siwezi kupata hata eneo ambalo liko ndani ya kilometa kumi kutoka mjini lenye ukubwa ule ule!!!

Ni kutokana na sababu hii, nimejifunza juu ya yafuatayo kabla ya kuuza amali yoyote.
  • Usiuze amali ikiwa hujaweka mipango madhubuti inayotekelezeka juu ya kununua amali mbadala ikiwa unaihitaji
  • Usiuze amali kutokana na dharura ambayo unaweza kupata suluhisho mbadala kwa wakati huo. Hii inaweza kukulazimisha kuuza amali yenye thamani kubwa kwa bei ndogo mno.
  • Epuka kutumia mtu wa tatu (kama vile dalali) wakati wa kuuza amali. Hii inaweza kupelekea kukosekana usawa wa bei ya amali unayoiuza.
  • Unapolazimika kuuza amali, jitahidi kujua thamani halisi ya amali unayoiuza kwa wakati huo. Hii itakusaidia kuhakikisha kuwa, unauza amali husika kwa bei halisi au walau inayoakisi uhalisia wa wakati husika
  • Mapato unayoyapata wakati umeuza chochote ulichowahi kukimiliki, hasa kama ni cha kudumu, ni vema ukahakikisha kuwa sehemu yake unaielekeza kwenye ununuzi wa amali nyingine.
  • Penda kushirikisha watu wengine wakati wa kufanya maamuzi ya kuuza amali zako, hasa wale unaowaamini. Hii inaweza kukusaidia kupata msaada wa mawazo na wakati mwingine, unaweza kupata msaada wa kuweka rehani mali husika badala ya kuiuza.
Nimeshuhudia watu waliouza nyumba zao kariakoo aise wana hali mbaya sana hata ukijiuliza hela zimeenda wapi hupati jibu na wapo usweken huko
 
Uko sahihi.. Na hapa ndio tatizo kubwa lilipo. Shida mara zote inakufumba macho, masikio na zaidi sana, AKILI. Mwenye shida yuko tayari kuuza utu na thamani yake, sio tu amali. Biblia inatukumbusha kuwa, Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kisa dengu tu... Njaa ilikuwa inakaribia kumuua!!
-
Ni hapo ndipo msisitizo wangu ulipo. Nyakati za shida zinapita, lakini zinaweza kupita zikakuacha ukiwa na shida kubwa kuliko ya awali. Fikiri unauza nyumba ili upambane na kesi mahakamani. Kwa bahati mbaya, unashindwa kesi na nyumba ulishaiuza. Au unashinda, unakuwa umetatua tatizo moja na kutengeneza lingine kubwa zaidi!!
-
Nyakati ngumu zinahitaji akili ngumu zaidi. Ni nyakati hizo zinazotulazimisha kuwaza zaidi juu ya maamuzi ya kuchukua. Kumbe, badala ya kuuza amali fulani, ni afadhali kuiweka rehani kwa mtu unayemuamini na ukatatua matatizo, kisha katika utulivu, hata utakapoamua kuiuza, unaiuza ukiwa na utulivu na sio msukumo mkubwa unaotokana na shida.
Mkuu ulishawai kupata changamoto yoyote iliyosababisha ukauza kitu chako kama nyumba.
 
Mkuu ulishawai kupata changamoto yoyote iliyosababisha ukauza kitu chako kama nyumba.
Bila shaka mkuu. Soma andiko langu nimetoa uzoefu hapo juu. Niliuza kiwanja mwaka 2014, eneo ambalo mpaka sasa imekuwa ni sehemu ya majuto makubwa na maumivu yasiyoisha moyoni. Nilipata shida ya kuuguza na kimbilio likawa kuuza eneo. Sitasahau kabisa!!
 
Nimeshuhudia watu waliouza nyumba zao kariakoo aise wana hali mbaya sana hata ukijiuliza hela zimeenda wapi hupati jibu na wapo usweken huko
Naam. Na hapo kuna cha kujiuliza. Fikiri thamani ya nyumba pale kariakoo. Mtu anaiuza kwa kuwa na shida, na unakuta anapewa thamani ambayo hata kununua kiwanja Vigwaza au Chanika hawezi. Anapata pesa ambayo hata akiamua kurudi kijijini hawezi kujenga kibanda cha kujisitiri na kuanzisha mradi. Mbaya zaidi, unakuta ni mzaliwa wa jiji la Dar, hivyo hawezi kwenda mbali na Dar na kufanya maisha mengine. Anauza kariakoo anaenda kupanga Mazense na baada ya mwaka mmoja, pesa inakuwa imeisha anatamani akaanze kuleta vurugu alikouza
 
Naam. Na hapo kuna cha kujiuliza. Fikiri thamani ya nyumba pale kariakoo. Mtu anaiuza kwa kuwa na shida, na unakuta anapewa thamani ambayo hata kununua kiwanja Vigwaza au Chanika hawezi. Anapata pesa ambayo hata akiamua kurudi kijijini hawezi kujenga kibanda cha kujisitiri na kuanzisha mradi. Mbaya zaidi, unakuta ni mzaliwa wa jiji la Dar, hivyo hawezi kwenda mbali na Dar na kufanya maisha mengine. Anauza kariakoo anaenda kupanga Mazense na baada ya mwaka mmoja, pesa inakuwa imeisha anatamani akaanze kuleta vurugu alikouza
Uuze asset upewe bln 4 kama una akili si utapiga hatua

Ova
 
Mtu anauza jokofu lenye thamani ya laki tano kwa shilingi laki tatu na nusu ili alipe deni la shilingi laki tatu. Elfu hamsini inayobaki anaenda kujipooza moyo kwa kula nyama choma na bia baridi. Kumbe angetuliza kichwa kidogo tu, angeomba muda kidogo wa kujipanga, akaanzisha mradi rahisi wa kuuza Ice Cream, ndani ya mwezi mmoja akawa walau amelipa nusu ya deni au kumaliza deni na akabaki na jokofu lake likiendelea kufanya biashara na matumizi mengine ya nyumbani
Hizo ice cream mzee sio kila sehemu zinatoka alafu pressure ya wadai sio ya mchezo.
 
Mali nyingi sahv za mirathi zinauzwa

Ova
Ingawa wengi kati ya hawa wanaouza tumewaona wakiwa na majuto baada ya muda. Hawajuti kwa kuwa waliziuza, wengi wanajuta kwa kuwa waliziuza bila kufikiri sawasawa, au waliziuza kutokana na migogoro, na zaidi sana, baada tu ya kuziuza, hawakufanya maamuzi wachukue hatua inayofuata.
 
Hizo ice cream mzee sio kila sehemu zinatoka alafu pressure ya wadai sio ya mchezo.
Ni sahihi. Unajua hata wanaotudai mara nyingi sana tunajikuta tunawakwaza kwa mienendo na matendo yetu. Mtu anakudai halafu unaleta njia za kupinda pinda. Nikijuacho, ikiwa unadaiwa, unapaswa kunyoosha sana maneno na matendo yako. Deni halifungi.
 
Back
Top Bottom