Usiuze amali (assets) kabla ya kuwa na mpango mahsusi

Samahani

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
237
Reaction score
355
Maisha yanatupa nafasi ya kufanya maamuzi kila siku. Tunafanya maamuzi juu ya kila kitu kinachotuzunguka. Tunaamua muda wa kuamka na muda wa kulala, nini tufanye na nini tusifanye… Karibu kila wakati tunajikuta tunahitajika kufanya maamuzi. Kwa kiasi kikubwa, tuko jinsi tulivyo ni kutokana na maamuzi tunayoyafanya.

Umewahi kumiliki amali (asset) yoyote na ukalazimika kuiuza kutokana na sababu yoyote? Mfano, unaweza kuwa na kiwanja, nyumba, gari, redio, kitanda, kochi, simu, laptop, jokofu, vyombo vya ndani, nguo au kingine chochote kama hivyo. Wakati Fulani, unaweza kujikuta unalazimika kuuza mojawapo kati ya vitu hivi kwa sababu mbalimbali kama vile kukwama kiuchumi, kuhitaji fedha ya kukabiliana na dharura kubwa (msiba, ugonjwa, sherehe n.k), kuhitaji kubadilisha aina ya amali (kupata iliyo bora Zaidi), kuhamisha makazi, kupunguza idadi ya amali na sababu nyingine nyingi.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi unapouza amali fulani, haiwi rahisi kununua tena amali hiyo!!! Hata pale unapofanikiwa kununua, huenda isiwe tena ya ubora na/au viwango vya amali iliyouzwa awali.

Mathalani, binafsi niliwahi kuuza shamba eneo ambalo sasa ni katikati ya mji kabisa. Wakati nauza eneo lile, nililiuza kwa shilingi milioni nne hivi. Lakini miaka sita baadae, eneo lile lile limekuwa na thamani ya Zaidi ya mara kumi!! Kwa kiasi kile kile ambacho niliuza, leo siwezi kupata hata eneo ambalo liko ndani ya kilometa kumi kutoka mjini lenye ukubwa ule ule!!!

Ni kutokana na sababu hii, nimejifunza juu ya yafuatayo kabla ya kuuza amali yoyote.
  • Usiuze amali ikiwa hujaweka mipango madhubuti inayotekelezeka juu ya kununua amali mbadala ikiwa unaihitaji
  • Usiuze amali kutokana na dharura ambayo unaweza kupata suluhisho mbadala kwa wakati huo. Hii inaweza kukulazimisha kuuza amali yenye thamani kubwa kwa bei ndogo mno.
  • Epuka kutumia mtu wa tatu (kama vile dalali) wakati wa kuuza amali. Hii inaweza kupelekea kukosekana usawa wa bei ya amali unayoiuza.
  • Unapolazimika kuuza amali, jitahidi kujua thamani halisi ya amali unayoiuza kwa wakati huo. Hii itakusaidia kuhakikisha kuwa, unauza amali husika kwa bei halisi au walau inayoakisi uhalisia wa wakati husika
  • Mapato unayoyapata wakati umeuza chochote ulichowahi kukimiliki, hasa kama ni cha kudumu, ni vema ukahakikisha kuwa sehemu yake unaielekeza kwenye ununuzi wa amali nyingine.
  • Penda kushirikisha watu wengine wakati wa kufanya maamuzi ya kuuza amali zako, hasa wale unaowaamini. Hii inaweza kukusaidia kupata msaada wa mawazo na wakati mwingine, unaweza kupata msaada wa kuweka rehani mali husika badala ya kuiuza.
 
Ni muhimu sana kuwa nao makini
 
Unatafuta ugomvi namadalali
Kuwa nao makini sana mkuu... Nimewahi kuona mtu anauza shamba milioni kumi na mbili wakati kwake zinafika tatu tu. Dalali kaweka kilemba cha maana juu, na mwenye mali hajui
 
🤝
 
Mtu uko na shida zimekukaba kooni huoni muda wa kujadili thamani ya kitu unachotaka kuuza unautoa wapi? Muhimu upate mteja akutoe hapo kwanza mambo mengine mbele kwa mbele utajipanga huko.
 
Ila Mimi Niko tofauti kdg,

Ule ujinga WA Nina asset yangu,

afu NMETINGWA nisiiuze kisa naogopa sitoipata tena AU watanionaje.

aisee nishaukataa kitambo.

Nnachoamini Mimi,
KIMFAACHO MTU CHAKE
 
Huu ujinga WA kutouza assets Kwa uoga WA kutopata nyingine unawacost SANA waliokopea mikopo nyumba wanazoishi kwenye mabenki.

Unakuta mtu deni limekaba koo, anaogopa kuuza nyumba yake anayoishi, alipe deni benk, abakize Cha juu aendeleze Mizunguko.

Anabaki kujipa matumaini uchwara atalilipa tu na penalty za benki zinamuandama, deni linakua kubwa.

mwisho wa SIKU benki wanakuja kuuza wenyewe na haambulii Hata mia mbovu
 
Uko sahihi.. Na hapa ndio tatizo kubwa lilipo. Shida mara zote inakufumba macho, masikio na zaidi sana, AKILI. Mwenye shida yuko tayari kuuza utu na thamani yake, sio tu amali. Biblia inatukumbusha kuwa, Esau aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kisa dengu tu... Njaa ilikuwa inakaribia kumuua!!
-
Ni hapo ndipo msisitizo wangu ulipo. Nyakati za shida zinapita, lakini zinaweza kupita zikakuacha ukiwa na shida kubwa kuliko ya awali. Fikiri unauza nyumba ili upambane na kesi mahakamani. Kwa bahati mbaya, unashindwa kesi na nyumba ulishaiuza. Au unashinda, unakuwa umetatua tatizo moja na kutengeneza lingine kubwa zaidi!!
-
Nyakati ngumu zinahitaji akili ngumu zaidi. Ni nyakati hizo zinazotulazimisha kuwaza zaidi juu ya maamuzi ya kuchukua. Kumbe, badala ya kuuza amali fulani, ni afadhali kuiweka rehani kwa mtu unayemuamini na ukatatua matatizo, kisha katika utulivu, hata utakapoamua kuiuza, unaiuza ukiwa na utulivu na sio msukumo mkubwa unaotokana na shida.
 
Ila Mimi Niko tofauti kdg,

Ule ujinga WA Nina asset yangu,

afu NMETINGWA nisiiuze kisa naogopa sitoipata tena AU watanionaje.

aisee nishaukataa kitambo.

Nnachoamini Mimi,
KIMFAACHO MTU CHAKE
Sahihi. Na kuwa kuwa kimfaacho mtu chake, si vema kikimletea majuto yanayoweza kuepukika. Tunanunua amali ili zitufae. Sihamasishi mtu mwenye amali yake asiiuze, kuna nyakati tunazinunua ili baadae tuziuze maisha yaendelee. Swali kuu hapa ni, JE, Unauza amali yako wakati gani na kwenye mazingira gani?"
-

Umeshafikiri mara kadhaa juu ya kuiuza wakati huu na sio wakati mwingine?
Unaiuza kwa thamani halisi inayokubalika katika soko la amali ile?
Una mpango wa kupata amali nyingine inayoweza kuwa mbadala wa unayoiuza kutokana na umuhimu wake? (Mfano, unauza nyumba unayoishi. Je, una makazi mengine? Au kwa pesa unayoipata, unaweza kupata makazi mengine?
Je, kuuza amali hiyo ndilo wazo pekee linaloweza kuwa msaada kwako kwasasa?
Je, hakuna msukumo hasi unaokusukuma kuuza amali hiyo sasa, na baadae msukumo huo ukiisha ukajuta? (Msukumo unaweza kuwa shida za kawaida kwenye maisha, madeni, ulevi, hasira, kisasi, n.k)
 
Maisha yanatupa nafasi ya kufanya maamuzi kila siku. Tunafanya maamuzi juu ya kila kitu kinachotuzunguka. Tunaamua muda wa kuamka na muda wa kulala, nini tufanye na nini tusifanye… Karibu kila wakati tunajikuta tunahitajika kufanya maamuzi. Kwa kiasi kikubwa, tuko jinsi tulivyo ni kutokana na maamuzi tunayoyafanya.

Umewahi kumiliki amali (asset) yoyote na ukalazimika kuiuza kutokana na sababu yoyote? Mfano, unaweza kuwa na kiwanja, nyumba, gari, redio, kitanda, kochi, simu, laptop, jokofu, vyombo vya ndani, nguo au kingine chochote kama hivyo. Wakati Fulani, unaweza kujikuta unalazimika kuuza mojawapo kati ya vitu hivi kwa sababu mbalimbali kama vile kukwama kiuchumi, kuhitaji fedha ya kukabiliana na dharura kubwa (msiba, ugonjwa, sherehe n.k), kuhitaji kubadilisha aina ya amali (kupata iliyo bora Zaidi), kuhamisha makazi, kupunguza idadi ya amali na sababu nyingine nyingi.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kuwa, mara nyingi unapouza amali fulani, haiwi rahisi kununua tena amali hiyo!!! Hata pale unapofanikiwa kununua, huenda isiwe tena ya ubora na/au viwango vya amali iliyouzwa awali.

Mathalani, binafsi niliwahi kuuza shamba eneo ambalo sasa ni katikati ya mji kabisa. Wakati nauza eneo lile, nililiuza kwa shilingi milioni nne hivi. Lakini miaka sita baadae, eneo lile lile limekuwa na thamani ya Zaidi ya mara kumi!! Kwa kiasi kile kile ambacho niliuza, leo siwezi kupata hata eneo ambalo liko ndani ya kilometa kumi kutoka mjini lenye ukubwa ule ule!!!

Ni kutokana na sababu hii, nimejifunza juu ya yafuatayo kabla ya kuuza amali yoyote.
  • Usiuze amali ikiwa hujaweka mipango madhubuti inayotekelezeka juu ya kununua amali mbadala ikiwa unaihitaji
  • Usiuze amali kutokana na dharura ambayo unaweza kupata suluhisho mbadala kwa wakati huo. Hii inaweza kukulazimisha kuuza amali yenye thamani kubwa kwa bei ndogo mno.
  • Epuka kutumia mtu wa tatu (kama vile dalali) wakati wa kuuza amali. Hii inaweza kupelekea kukosekana usawa wa bei ya amali unayoiuza.
  • Unapolazimika kuuza amali, jitahidi kujua thamani halisi ya amali unayoiuza kwa wakati huo. Hii itakusaidia kuhakikisha kuwa, unauza amali husika kwa bei halisi au walau inayoakisi uhalisia wa wakati husika
  • Mapato unayoyapata wakati umeuza chochote ulichowahi kukimiliki, hasa kama ni cha kudumu, ni vema ukahakikisha kuwa sehemu yake unaielekeza kwenye ununuzi wa amali nyingine.
  • Penda kushirikisha watu wengine wakati wa kufanya maamuzi ya kuuza amali zako, hasa wale unaowaamini. Hii inaweza kukusaidia kupata msaada wa mawazo na wakati mwingine, unaweza kupata msaada wa kuweka rehani mali husika badala ya kuiuza.
Aise upo sahihi ukiuza asset kuirudisha ni ngumu sana na matatizo huwa hayaishi
 
Huu ujinga WA kutouza assets Kwa uoga WA kutopata nyingine unawacost SANA waliokopea mikopo nyumba wanazoishi kwenye mabenki.

Unakuta mtu deni limekaba koo, anaogopa kuuza nyumba yake anayoishi, alipe deni benk, abakize Cha juu aendeleze Mizunguko.

Anabaki kujipa matumaini uchwara atalilipa tu na penalty za benki zinamuandama, deni linakua kubwa.

mwisho wa SIKU benki wanakuja kuuza wenyewe na haambulii Hata mia mbovu

Hili umeliweka vizuri sana. Nitaandika kwa kirefu katika thread nyingine juu ya maamuzi ya kukopa katika taasisi za pesa.

Hakuna sehemu nimeshauri mtu asiuze asset. Umeeleza vizuri sehemu kuwa, kimfaacho mtu chake. Inapotokea umefanyaa tathmini ya kina juu ya kuuza amali yako, ni wazi kuwa utajikita kuangalia jinsi utakavyonufaika kwa muda mfupi na muda mrefu pia. Katika tathmini yako ni wazi kuwa utakuja na maamuzi sahihi. Kama ni nyumba, utapata muda wa kutosha kuipa thamani, kujua bei halisi ya eneo na jengo kwa wakati huo na hata utakapoiuza, pesa utakayoipata utakuwa umeshafanya maamuzi bora juu ya namna ya kuiwekeza ili ikupe matumaini mapya.
-
Kinyume chake, kuna nyakati tunauza assets kutokana na hasira, kuwakomoa wengine (hasa kwenye mahusiano na ndoa), tunapokuwa na madeni (mengine yasiyo na tija), hali ya ulevi au uraibu wa madawa, kufuata mkumbo, kuwa na matarajio fulani makubwa (mtu anauza nyumba ili aende mgodini kwenda kuokota madini awe bilionea kama Laizer) na sababu nyingine kama hizo.
-
Zipo nyakati pia tunashindwa kuweka vema mipango yetu ya kawaida ya maisha. Tunaingia kwenye madeni yasiyo na tija. Umesikia jinsi ambavyo watu wanaumizwa na vicoba, upatu, madeni ya nguo, pombe, michango ya sherehe na mengine kama hayo. Je, katika madeni kama haya, unapouza asset yako, una matumaini kweli ya kuirudisha?
 
Aise upo sahihi ukiuza asset kuirudisha ni ngumu sana na matatizo huwa hayaishi
Mtu anauza jokofu lenye thamani ya laki tano kwa shilingi laki tatu na nusu ili alipe deni la shilingi laki tatu. Elfu hamsini inayobaki anaenda kujipooza moyo kwa kula nyama choma na bia baridi. Kumbe angetuliza kichwa kidogo tu, angeomba muda kidogo wa kujipanga, akaanzisha mradi rahisi wa kuuza Ice Cream, ndani ya mwezi mmoja akawa walau amelipa nusu ya deni au kumaliza deni na akabaki na jokofu lake likiendelea kufanya biashara na matumizi mengine ya nyumbani
 
Back
Top Bottom