Usitolewe 'out' huku ukiwa huna salio mfukoni

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,420
40,405
Usitoke 'out' au sehemu yoyote ya kupata chakula au vinywaji ukiwa na rafiki/marafiki bila kuwa na salio lolote mfukoni na usiagize vinywaji au vyakula vinavyozidi salio ulilonalo mfukoni.

Kuna jamaa mmoja alikutana na rafiki yake wa muda mrefu kiasi, akamwambia bwana kaka wapi tunaweza kupata mlo mzuri na vinywaji? Jamaa akamwambia kuna sehemu fulani pako vizuri sana, basi huyo rafiki yake akamsisitiza hebu twende tukapate huduma.

Jamaa akajua yawezekana rafiki yake amejipanga vizuri, basi akampeleka ingawa yeye hakuchukua salio lolote huku akijua rafiki yake atalipa bill kutoka na msisitizo wa kutaka kwenda.

Baada ya kufika eneo la tukio, wakaagiza vyakula na vinywaji, baada ya muda wakaletewa bill, rafiki wa jamaa akiangalia mfukoni salio halitoshi kulipa bill ya watu wawili, ikabidi amwambie mwenzie achangie. Mbaya zaidi mwenzake hakutembea na salio, kilichofuata wanajua wenyewe.
 
Uwe na wa kumpigia, na awe na uwezo na utayari wa kukusaidia.

Vizuri ni kutokutoka safari ya hiari bila kitu mfukoni, tena ni vema kuhakikisha utumiacho uwe na uwezo wa kukilipia hata kama hutakilipia wewe.

kwa kweli
 
Nisitembee na kila kitu hata pochi nisiwe nayo ila siyo pesa jamani, kuna emergencies za ajabu sana zinaweza kukuaibisha..!
Hata kama unaenda kuonana na mtu una hakika ata take care of everything lakini lazima uwe na kipesa chako tu kibindoni, yaani kwanza unakuwa unajiamini khatari..!!
 
Back
Top Bottom