Kulewa haimaanishi kwamba anayelewa hana akili, kuna kazi ambazo bila kupata kileo haziendi vyema. Naamini unawafaham vyema madaktari waliosomea Urusi walivyo walevi lakini utendaji wao kazi ni mzuri sana. wapo pia ma-engineer ambao ni waevi lakini wanachapa kazi hamna mfano. Na pia wapo watu ambao hawakamati kilaji hatakidogo lakini asubuhi wanaamkia kwenye vijiwe vya kahawa, wakitoka hapo ni kurudi nyumbani kusubiri msosi ulioandaliwa na wake zao wanaojishughulisha na shughuli ndogondogo kama umama ntilie n.k
KICHWA CHINI MIGUU JUU UNAENDESHA GARI.
Ulio andika hayafanani na topic, sisi tunaongelea mtoto kucopy tabia ya wazazi.
Hatuongelei elim ya mtu, au matendo ya mtu na uwezaji wake wa kufanya kazi.
Na vile vile kuna tofauti ya mlevi na mnywaji, we vipi mwenzetu?
Sikubaliani na wewe docta mlevi anaweza kufanya kazi vizuri.
Kuna docta alikuwa analewa halafu kufanya operation na kuua wagonjwa, mwisho raia wakilalamika na mwiso akasimamshwa kazi. Lakini docta mwenyewe aliona anafanya kazi nzuri.
Nilikua na mwalim mlevi, alikuwa hafundishi akingia darasani, wanafunzi wakifeli somo lake, ila yeye mwenyewe akisema akilewa ndio anafundisha vizuri, mwisho akasimamishwa kazi.
Wewe ni punguani, urusi ni nchi ilio corrupt, wamepoteza muelekeo kila wanavofanya sio sahihi, ndio maana hamna amani.
uzuri ni kwamba sio watanzania wote wanarudi home na huwo ujinga wa kucopy vitu vya kujiaribia na kuaribia wengine.
Na kuna docs za ulaya niliona madocta wanao tumia madawa ya kulevya, nini pombe.
copy mazuri hachana na ya kiaribifu, by somoe