Mkuu pole.vipi na watoto hajakimbia nao?? wana heshima za kinafiki.
Mkuu
Albosignathus,
Acha nikupe japo trailer kidogo,
Huyu mama nilmvumilia, na kwa taarifa tu mimi ndo nilihama nyumba (yakupanga wakati huo) nilishindwa mkuu, nilivumilia nikasema cha kufia nini, (ndoa ya kikatoliki hiyo).
Siku naondoka hakuwepo nyumbani alirudi usiku kama kawaida yake, akakuta nimeshasepa, nadhani kwanza hakuelewa kilichokuwa kinaendelea, baada ya kama wiki moja alinifuata huko nilikokuwa na kuniporomoshea matusi mazito, akiniita zigo la mavi, nakumbuka the late baba yangu alisha niambia nisithubutu kunyanyua mkono kumpiga mwanamke, kwa hiyo matusi yote hayo niliyapokea kwa iwango cha juu sana cha uvumilivu, nakumbuka alitukana mpaka akachoka bila mimi kunyenyua mdomo wala mkono wangu... akaondoka zake.
Kuna wakati aliwahi kunitukana matusi ya ajabu sana mchana kweupe kituo cha basi mtoto wetu akisikia kila kitu, mkuu sikujibu chochote mpaka anamaliza na kuondoka. wakati huo ni kama mwaka mmoja baada ya kuwa mbali naye na mimi nimeshapata super woman ambaye ninaye mpaka leo, aliyenikubali mimi na watoto wa wangu. Naona aliumia sana kwa sababu pengine alidhani ningebaki single milele, kitendo cha kujua kumbe ninaweza kupendwa kilimvuruga hahaha...
Alikatalia watoto akaondoka nao akawapeleka kwa mama yake, na yeye akaendela na 'uchangu' wake bila kujua watoto wanakula nini wanalala vipi nk.
Ajabu mama yake ambaye alikuwa mnyakyusa pia hakunipa kabisa ushirikiano, alikuwa upande wa mwanae kwa kila kitu, bila kujali kuchunguza tatizo, lakini Mungu si athumani huyo aliyekuwa mke wangu alikuja akamtwanga huyo mama yake mzazi siku moja.
Let me sumarise sifa zingine:
1. Alikuwa anarudi nyumbani hata saa nane usiku na mimi ndio namfungulia mlango, kisa nalinda future ya mtoto asikose mama.
2. Alikuwa anakaa baa tena ya jirani na nyumbani kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane.
3. Aliendelea kwenda baa hata alipokuwa mja mzito, wakati huo tumesha tenganana na alipojifungua alipotea kwa wiki moja tu na kuendelea na baa business.
4. Hakunyonyesha mtoto kwa sababu ya kukosa muda wa kufanya hivyo aliona pombe ni bora zaidi.
5. Watoto wake walikuwa wanamuita aunt, halafu housegirl anaitwa mama, ndiye waliyemjua.
6. Alikuwa mbishi ajabu, hakubali kushauriwa, ukitaka mkae muongeelee tofauti hizo anakuwa mbogo. na mengine mengi tu
7. Mtoto alifundishwa kunichukia, mama mkwe hakuniruhusu kuchukua watoto wangu pamoja na kuwa mama yao hakuishi nao, hata kipindi fulani nilitaka kumchukua mwanangu wakati wa kipindi cha pasaka na niwarudishe baadaye lakini sikuruhusiwa, tuliwahi kugombana nikamwambia aniache na mimi niishi na watoto wangu kama yeye alivyoishi na wake. Kwa kifupi huyo mama naye hakuwa na akili, sorry to say so...
Angalizo: Hapa sielezei tabia za wanyakyusa, ila naelezea tabia alizokuwa nazo mwanamke wa kinyakyusa aliyekuwa mke wangu, nadhani umepata picha mkuu
Albosignathus.
Cc.
Sibonike