Usisubiri kujua thamani yake akiondoka

Usisubiri kujua thamani yake akiondoka

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,709
Reaction score
35,712
Watu husema kwamba, "Huwezi kujua thamani ya kitu mpaka ukipoteze". Kwangu mimi hii si kweli.
.
Ukweli ni kwamba, muda wote mtu hufahamu thamani ya kitu alichonacho, sema hua hafikirii kama atakuja kukipoteza.
.
Yule EX wako unafahamu fika kwa namna gani alivyokuwa bora, unafahamu kabisa kwa nafasi yake alijitahidi kwa hali na mali kukupa furaha. Ulimchukulia poa kwa sababu ulifikiri hatakuja kuondoka mikononi mwako.
.
Ile kazi uliyonayo, unafahamu fika ilivyokuwa ya muhimu kwako katika kuendesha maisha yako, lakini uliichukulia poa kwa vile ulijua fika sio rahisi kuipoteza.
.
Chochote ulichonacho leo hii, usisubiri mpaka kikuponyoke ndipo uanze kujuta. Maana, utakapoanza kupay attention ndipo kitakuwa kishakuondoka na hakirudi tena!!
.
Unae mama? Mueleze kuwa unampenda, mthamini na mtunze. Maana, wakati wewe unasheherekea mothers' day, siku hiyo hiyo mtu mwingine anamzika mama yake. Vivyo hivyo hata kwa baba.
.
Unae Mke/Mume/girlfriend/Boyfriend? Mpende, tambua thamani yake katika maisha yako kwa sababu wakati mtu mwingine akisheherekea Valentine day na mpenzi wake, mwingine anamkumbuka mpenzi wake aliempoteza.
.
Ishi maisha yako sasa! Furahia kila sekunde ya uhai uliyopewa na Mwenyezi MUNGU. Pale utakapotizama nyuma isiwe ni majuto, bali iwe ni shukrani kwa hatua kubwa uliyopiga!!!

God bless y'all
2019-02-15%2009.44.03.jpeg
 
Thanks to all MMU members na JF yote.. michango yenu inanielimisha na kuniweka mbali na upweke.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom