Usista duu haulipi...... Utaumbuka bureeeee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usista duu haulipi...... Utaumbuka bureeeee

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Sep 20, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  Hili ni tukio la kweli lililo tokea last weekend mjini Dar es Salaam pande za Masaki.
  Kisa chenyewe kilikuwa hivi, kuna kijana mmoja wa pande za Usukumani alipata msichana kwenye facebook.
  Kwenye kutambulishana, msichana akajitambulisha kuwa anaishi Masaki na wazazi wake.
  Kijana wa kisukuma akamdondokea kiukweli sister do wa Masaki. Kijana wa Kisukuma alipopata likizo, akafunga safari hadi DsM na kufikia bondeni hotel, Magomeni.
  Mawasiliano yakafanyika kati ya sista duu wa Dsm na Msukuma mshamba. Binti akaja hadi Magomeni Bondeni Hotel na kuanza kumgombeza Msukuma kwa nini amefikia Magomeni Hoteli ya hadhi ya chini na hakufikia hoteli kama Golden Tulip, Sea Cliff ama Double Tree Hotel.
  Jamaa Msukuma akajitettea kuwa hakuwa na uwezo wa kukaa hoteli kubwa, binti akamfyonya kwa dharau ya hali ya juu.
  Msukuma akachuklia poa, na baada ya siku tatu binti mwenyewe "akajiingiza mkenge", akamwambia Msukuma twende Masaki ukamuone baba yangu n na ndugu zangu.
  Maandalizi yakfanyika, Msukuma na binti wakaongozana wote pamoja hadi Masaki. Kufika huko wakakuta nyumba imejaa vijana, hakukuwa na mtu wa makamo wa kuweza kuwa baba ama mama wa Sister Duu wa Msukuma.

  Jioni Msukuma akiwa mbioni kuondoka akaja mzee mmoja wa Kipemba. Sister doo kwa manjonjo akamuintroduce Msukuma kwa baba wa Kipemba.
  Mpemba akafurahi sana, na akauliza umempeleka kwenu Yombo Vituka?
  Sisterr doo akakunja uso na kubadilika ghafla, wakati akimsindikiza Msukuma akamwambia sikutaki, baba yangu amekukataa ameona huna vigezo vya kuwa mpenzi na kuanzia leo usinijue tena.
  Msukuma akajibu haya, lakini akawa na jibu sahihi kuwa sista duu alikuwa analazimisha kuwa mtoto wa tajiri.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  sista duu anaendelea kumtumia msukua sms akimponda kuwa sio mvulana wa kisasa na wala hastahili kuwa na msichana kama sista duu wa Masaki
   
 3. Bright Smart

  Bright Smart JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 644
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  huyo sista duu wa masaki alikua beki tatu nini!!!???
   
 4. K

  Kyeli Lula Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ndio matokeo ya mapenzi ya kwenye facebook, Kaka Bujibuji mwambie huyo Msukuma ajfanye anataka kumwoa ila ampeleke kwao Yombo Vituka kwanza
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,132
  Trophy Points: 280
  Inawezekana...
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,132
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaaaah!!! Bujibuji again...
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Usista duu kazi kama huna vitendea kazi.............hehehehehehe
   
 8. M

  MyTz JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wadada wa kibongo wanapenda sana kuigiza maisha!!wameshindwa kabisa kuishi maisha yao halisi...
  inawezekana ni kweli bek3/mtu wa chini sana kimaisha...
   
 9. M

  MyTz JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  heheheheheh...
  hapo umenena, nenda ukatete nao wenye hako katabia!!!i&i
   
 10. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Bujibuji hii hadith ina2fundsha nin mkuu?
   
 11. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  hamna kitu hapo..ni hadithi tu kama za 'kumbi na kumbinga".
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mmmh!
  .
   
 13. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  Masaki ndo nini? Au wapi?
   
 14. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  shangaa,cjui wanao kaa brooklyn au manhattan wao wasemeje.
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwani haya mambo bado yapo siku hizi?

  kuna matajiri wengi saana wanaishi manzese au yombo au hata magomeni na ni matajiri kuliko hata hao wa masaki....
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  wengine wanadhani eti ukizaliwa tu Dsm una degreee. Halafu kusoma na kuandika hujui
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  Unakufahamu Manzese Midizini, Mbagala kwa Nyoka na Tandale Kona ya Ta'ko? Basi Masaki ipo jirani na maeneo hayo
   
 18. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duuh,usister du mwingine ni adhabu 2..kwan wanaokaa masaki wanapokufa hawaozi?
   
 19. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  nahisi nahitaji ramani mpya ya jiji la DSM
   
 20. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,160
  Trophy Points: 280
  dada yako akiwa house girl imekula kwako
   
Loading...