Usista duu haulipi...... Utaumbuka bureeeee

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
Hili ni tukio la kweli lililo tokea last weekend mjini Dar es Salaam pande za Masaki.
Kisa chenyewe kilikuwa hivi, kuna kijana mmoja wa pande za Usukumani alipata msichana kwenye facebook.
Kwenye kutambulishana, msichana akajitambulisha kuwa anaishi Masaki na wazazi wake.
Kijana wa kisukuma akamdondokea kiukweli sister do wa Masaki. Kijana wa Kisukuma alipopata likizo, akafunga safari hadi DsM na kufikia bondeni hotel, Magomeni.
Mawasiliano yakafanyika kati ya sista duu wa Dsm na Msukuma mshamba. Binti akaja hadi Magomeni Bondeni Hotel na kuanza kumgombeza Msukuma kwa nini amefikia Magomeni Hoteli ya hadhi ya chini na hakufikia hoteli kama Golden Tulip, Sea Cliff ama Double Tree Hotel.
Jamaa Msukuma akajitettea kuwa hakuwa na uwezo wa kukaa hoteli kubwa, binti akamfyonya kwa dharau ya hali ya juu.
Msukuma akachuklia poa, na baada ya siku tatu binti mwenyewe "akajiingiza mkenge", akamwambia Msukuma twende Masaki ukamuone baba yangu n na ndugu zangu.
Maandalizi yakfanyika, Msukuma na binti wakaongozana wote pamoja hadi Masaki. Kufika huko wakakuta nyumba imejaa vijana, hakukuwa na mtu wa makamo wa kuweza kuwa baba ama mama wa Sister Duu wa Msukuma.

Jioni Msukuma akiwa mbioni kuondoka akaja mzee mmoja wa Kipemba. Sister doo kwa manjonjo akamuintroduce Msukuma kwa baba wa Kipemba.
Mpemba akafurahi sana, na akauliza umempeleka kwenu Yombo Vituka?
Sisterr doo akakunja uso na kubadilika ghafla, wakati akimsindikiza Msukuma akamwambia sikutaki, baba yangu amekukataa ameona huna vigezo vya kuwa mpenzi na kuanzia leo usinijue tena.
Msukuma akajibu haya, lakini akawa na jibu sahihi kuwa sista duu alikuwa analazimisha kuwa mtoto wa tajiri.
 
sista duu anaendelea kumtumia msukua sms akimponda kuwa sio mvulana wa kisasa na wala hastahili kuwa na msichana kama sista duu wa Masaki
 
hayo ndio matokeo ya mapenzi ya kwenye facebook, Kaka Bujibuji mwambie huyo Msukuma ajfanye anataka kumwoa ila ampeleke kwao Yombo Vituka kwanza
 
Hili ni tukio la kweli lililo tokea last weekend mjini Dar es Salaam pande za Masaki.
Kisa chenyewe kilikuwa hivi, kuna kijana mmoja wa pande za Usukumani alipata msichana kwenye facebook.
Kwenye kutambulishana, msichana akajitambulisha kuwa anaishi Masaki na wazazi wake.
Kijana wa kisukuma akamdondokea kiukweli sister do wa Masaki. Kijana wa Kisukuma alipopata likizo, akafunga safari hadi DsM na kufikia bondeni hotel, Magomeni.
Mawasiliano yakafanyika kati ya sista duu wa Dsm na Msukuma mshamba. Binti akaja hadi Magomeni Bondeni Hotel na kuanza kumgombeza Msukuma kwa nini amefikia Magomeni Hoteli ya hadhi ya chini na hakufikia hoteli kama Golden Tulip, Sea Cliff ama Double Tree Hotel.
Jamaa Msukuma akajitettea kuwa hakuwa na uwezo wa kukaa hoteli kubwa, binti akamfyonya kwa dharau ya hali ya juu.
Msukuma akachuklia poa, na baada ya siku tatu binti mwenyewe "akajiingiza mkenge", akamwambia Msukuma twende Masaki ukamuone baba yangu n na ndugu zangu.
Maandalizi yakfanyika, Msukuma na binti wakaongozana wote pamoja hadi Masaki. Kufika huko wakakuta nyumba imejaa vijana, hakukuwa na mtu wa makamo wa kuweza kuwa baba ama mama wa Sister Duu wa Msukuma.

Jioni Msukuma akiwa mbioni kuondoka akaja mzee mmoja wa Kipemba. Sister doo kwa manjonjo akamuintroduce Msukuma kwa baba wa Kipemba.
Mpemba akafurahi sana, na akauliza umempeleka kwenu Yombo Vituka?
Sisterr doo akakunja uso na kubadilika ghafla, wakati akimsindikiza Msukuma akamwambia sikutaki, baba yangu amekukataa ameona huna vigezo vya kuwa mpenzi na kuanzia leo usinijue tena.
Msukuma akajibu haya, lakini akawa na jibu sahihi kuwa sista duu alikuwa analazimisha kuwa mtoto wa tajiri.

Ahahahaaaaah!!! Bujibuji again...
 
Usista duu kazi kama huna vitendea kazi.............hehehehehehe
 
kwani haya mambo bado yapo siku hizi?

kuna matajiri wengi saana wanaishi manzese au yombo au hata magomeni na ni matajiri kuliko hata hao wa masaki....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom