Usiseme nitampenda Kesho

Usiseme nitampenda Kesho

Habari zenu Great
Thinkers
Leo nimekuja naomba niwausie kitu ndugu zangu.

Katika mahusiano ya kimapenzi,kirafiki au kifamilia kupishana au
kukosana ni jambo la kawaida lakini tusipende kuendekeza ugomvi na
ukorofi usiokuwa na maana, nitawapa kidogo hii inanihusu mimi mwenyewe.

Ni kwamba katika familia yetu tulizaliwa wengi kidogo....kuna kaka yetu
mmoja aliondoka nyumbani mimi nikiwa sina ufahamu. I mean nilikuwa
nimezaliwa lakini nilikuwa mdogo sana nadhani nilikuwa bado nanyonya.

Kwa maana hiyo nilikuwa simfahamu huyo kaka yangu zaidi ya kumuona
kwenye picha.

Alirudi nyumbani baada ya miaka kama kumi japo hakukaa sana nilipata
wasaa wa kukaa nae na kipindi hicho hata hatukukaa sana.

Baadae alirudi akakaa kwa kipindi kirefu kidogo na mimi wakati huo
nlikuwa mkubwa kidogo.

Nakiri wazi katika kipindi kifupi nilichokaa nae ni mara chache sana
tulifurahi pamoja muda mwingine ilikuwa ni kukosana tu.

Alikuwa ni mkubwa kwangu kwa hiyo alistahili kupewa heshima na upendo
kama kaka japo alikuwa ni mtata sana nilitakiwa kujishusha maana mimi
ndo mdogo lakini mara nyingi sikufanya hivyo ulikuwa ni utoto mi sijui
kwa kweli.

Nilijipa matumaini kwamba ipo siku mimi na kaka tutakaa kwa amani kabisa
na upendo, niliamini ni upepo tu utapita na yote yatakwisha kumbe
nilikuwa nakosea sana pumzi ya mwanadamu iko mikononi mwa Mungu. Hakuwa
na afya njema sana but I never thought he would go that soon.

Nakumbuka mara ya mwisho alikuwa ameondoka nyumbani akaenda huko
alikokuwa akiishi kwa ahadi ya kurudi baada ya wiki moja lakini
zikakatika wiki mbili siku moja kanipigia simu nikamwambia 'kaka wiki
moja haiishi'?

Akaniambia nitarudi j3 sikuamini hiyo j3 napokea taarifa za msiba.

Akarudi jumatatu kweli akiwa ndani ya jeneza..!! Nikikumbuka huwa nalia
sana.

Ninachotaka kusema ni kwamba tujitahidi kuishi vizuri na wale
tuwapendao, kama kuna tofauti zirekebishwe haraka hakuna sababu ya
kuwekeza utakapokuja kugutuka itakuwa too late.

Mimi yametokea hivi lakini kwa mwingine inaweza kutokea tofauti
yawezekana katika mahusiano yako unaishi kwa kugombana ovyo ovyo au
kumkwaza mwenzio kila mara pasipo sababu za msingi.

Siku utagutuka na kuanza kubadilika utagundua it's too late mwenzio
hayupo kwako tena.

kuna binadamu wagumu kubadilika
 
Back
Top Bottom