Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 59,468
- 119,622
Habari zenu Great Thinkers
Leo nimekuja naomba niwausie kitu ndugu zangu.
Katika mahusiano ya kimapenzi,kirafiki au kifamilia kupishana au kukosana ni jambo la kawaida lakini tusipende kuendekeza ugomvi na ukorofi usiokuwa na maana, nitawapa kidogo hii inanihusu mimi mwenyewe.
Ni kwamba katika familia yetu tulizaliwa wengi kidogo....kuna kaka yetu mmoja aliondoka nyumbani mimi nikiwa sina ufahamu. I mean nilikuwa nimezaliwa lakini nilikuwa mdogo sana nadhani nilikuwa bado nanyonya.
Kwa maana hiyo nilikuwa simfahamu huyo kaka yangu zaidi ya kumuona kwenye picha.
Alirudi nyumbani baada ya miaka kama kumi japo hakukaa sana nilipata wasaa wa kukaa nae na kipindi hicho hata hatukukaa sana.
Baadae alirudi akakaa kwa kipindi kirefu kidogo na mimi wakati huo nlikuwa mkubwa kidogo.
Nakiri wazi katika kipindi kifupi nilichokaa nae ni mara chache sana tulifurahi pamoja muda mwingine ilikuwa ni kukosana tu.
Alikuwa ni mkubwa kwangu kwa hiyo alistahili kupewa heshima na upendo kama kaka japo alikuwa ni mtata sana nilitakiwa kujishusha maana mimi ndo mdogo lakini mara nyingi sikufanya hivyo ulikuwa ni utoto mi sijui kwa kweli.
Nilijipa matumaini kwamba ipo siku mimi na kaka tutakaa kwa amani kabisa na upendo, niliamini ni upepo tu utapita na yote yatakwisha kumbe nilikuwa nakosea sana pumzi ya mwanadamu iko mikononi mwa Mungu. Hakuwa na afya njema sana but I never thought he would go that soon.
Nakumbuka mara ya mwisho alikuwa ameondoka nyumbani akaenda huko alikokuwa akiishi kwa ahadi ya kurudi baada ya wiki moja lakini zikakatika wiki mbili siku moja kanipigia simu nikamwambia 'kaka wiki moja haiishi'?
Akaniambia nitarudi j3 sikuamini hiyo j3 napokea taarifa za msiba.
Akarudi jumatatu kweli akiwa ndani ya jeneza..!! Nikikumbuka huwa nalia sana.
Ninachotaka kusema ni kwamba tujitahidi kuishi vizuri na wale tuwapendao, kama kuna tofauti zirekebishwe haraka hakuna sababu ya kuwekeza utakapokuja kugutuka itakuwa too late.
Mimi yametokea hivi lakini kwa mwingine inaweza kutokea tofauti yawezekana katika mahusiano yako unaishi kwa kugombana ovyo ovyo au kumkwaza mwenzio kila mara pasipo sababu za msingi.
Siku utagutuka na kuanza kubadilika utagundua it's too late mwenzio hayupo kwako tena.