Usipunjwe tena nyama buchani

Usipunjwe tena nyama buchani

Mizani madukani na mabuchani wezi weziiiii sana jamani..
 
Me/ Ke!. Ukienda kununua nyama buchani utaona kuna kajiwe kadogo karobo ambako mudawote kapo kwenye mizani.

Kajiwe hako kanawekwa makusudi ili kukufanya usijue kama mizani imeelemea katika upande inapowekwa nyama.

Mwambie akatoe kabla hajaweka nyama kwenye mzani iliuone kama mzani upolevo.

Ukituliatuu ujue umepunjwa nusu ya robo, kwasababu baadhi ya wauzaji wanatabia ya kuchezea mizani.

Mwingine anaejua ujanjaujanja wao tujuzane hapa.
Hilo baki, wengine hutumia ncha ya kisu.pia uliza jiwe la mhuri utaona anainama chini sakafuni na kuchukuwa la ukweli.
 
Ikiwa upo Dar nunua nyama Kawe jeshini nje madukani opposite Makongo pale hakuna masihara. Nyama nzuri na mzani mzuri. Michele ikiwa unaweza bora nunua Nakumatt ama supermarket zingine. Umepimwa vizuri na kilo zimetosha.


Hapo ndio nn unanunua kilo moja kwenye calibration ya kilo 10. ???
 
unakuta yale maye yanachanganywa na metali nyepesi kama aluminium. yanakuwa siyo 1kg. mafundi chuma hupiga hii kazi.
 
Siku hizi wamepewa mashine za kukata mifupa kwaiyo kwenye nyama lazima wakupe mfupa kwaiyo unakuta mfupa unakilo zake na nyama zinakilo zake kwaiyo siku hizi wanatupiga kupitia mifupa

Sasa Wewe hutaki Mfupa kwani yeye alichinja Ng'ombe asie na Mfupa au Mfupa akamuuzie Nani?
 
Sipati picha safari ya mbagala kawe kununua nusu na robo ya nyama....

Mie nilikaa huko na kuwa mteja hapo. Nilipohama na kwenda mbali nikienda nanunua kilo 6 hivi nasahau muda. Pia kuku wa kienyeji wapo shs. 15000 tu mkubwa wa kiasi. Wengine walikuwa Uchumi pale Nyerere Road bei ilikuwa kubwa lakini mzani safi na nyama safi. Walifunga mwaka juzi. Inawezekana hata Mbagala, Kijichi kukawa na wauzaji bucha waungwana fanya utafiti. Maisha ni kuhangaika upate kilicho bora.Jitahidi.
 
Hapo ndio nn unanunua kilo moja kwenye calibration ya kilo 10. ???

Nadhani wako vizuri wewe mjeshi umkate panga? Pia mizani yao ni tofauti na hizi zetu za Mawe imekaa kidigitali hivi. Jaribu kuwatembelea.
 
Pia hata mawe yenyewe hata kwenye maduka ya mangi inua halafu geuza kwa chini utaona limechimbika makusudi ili iwe faida kwao. Jihadharini
 
Ukinunua Asubui nyama inakua na maji maji, pia inakua na damu hivyo uzito wake unakua Mkubwa, Ila ikitundikwa inakauka kwa hiyo uzito wake unapungua.......

Kilo moja ya asubui sio kilo moja ya Jioni Mkuu.......!
Na kama mnyama amechinjwa mchana???
 
Ha ha ha msiogope akigizeni nyama bomba ya kongwa kutoka Dodoma kwa oda maalum,,,nyama nyama kwel,ukiichemsha unasikia harufu ya nyama sio nyama unachemsha unasikia km unachemsha dagaaa

Hapo nakubaliana na wewe. Mie huwa napenda kununuia hiyo inakuwa nzur na nyingi.
 
wengine wanapunguza ukubwa wa mawe kwa hiyo huwezi hata kuhisi, labda utoke hapo ukahakiki kwenye mzani mwingine
 
Ule upande wa sahai huwa wameweka kitu (mfano sumaku ambayo imenasishwa upande wa chini)
Hilo jambo huwa wanalificha kwa kuweka jiwe la kilo kadhaa upande wa pili wa mzani..!
Sasa wakati anakuuzia nyama au hata bidhaa nyingine kama sukari au mchele, anaweka kabisa hiyo bidhaa kabla ya kuondoa yale mawe uliyoyakuta, akishaweka hiyo bidhaa yako (kwa makadirio) hapo ndio utaona anatoa yale mawe uliyoyakuta kisha anaweka jiwe lenye kilo unazohitaji wewe (mfano kama unataka mchele wa kilo 1 basi hapo ndipo ataweka jiwe la kilo 1), halafu ataanza kubalance kwa kupunguza huo mchele au kuongezea hadi mzani ubalance.

Tafsiri
Hapo maana yake ni kwamba lile jiwe la kilo moja limebalance na uzito wa mchele wako + sumaku aliyoinasisha chini ya sahani.
Let say sumaku ilikuwa ni robo kilo, basi mchele wako ni robo tatu ya kilo.

Hapo atachukua mchele wako atakuwekea kwenye package, utaondoka na robo tatu zako ila ile robo (sumaku yake) utamuachia muuza duka
Zile mizani za electonic wengine badala kya kuiseit 0.00 inakuwa 0.08. kwa kuwa mamndishi ya 0 na 8 kwenye hizi mizani yanakaribiana wengi hawajui.
 
Back
Top Bottom