Usipunjwe tena nyama buchani

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
5,498
6,630
Me/ Ke!. Ukienda kununua nyama buchani utaona kuna kajiwe kadogo karobo ambako mudawote kapo kwenye mizani.

Kajiwe hako kanawekwa makusudi ili kukufanya usijue kama mizani imeelemea katika upande inapowekwa nyama.

Mwambie akatoe kabla hajaweka nyama kwenye mzani iliuone kama mzani upolevo.

Ukituliatuu ujue umepunjwa nusu ya robo, kwasababu baadhi ya wauzaji wanatabia ya kuchezea mizani.

Mwingine anaejua ujanjaujanja wao tujuzane hapa.
 
Ule upande wa sahai huwa wameweka kitu (mfano sumaku ambayo imenasishwa upande wa chini)
Hilo jambo huwa wanalificha kwa kuweka jiwe la kilo kadhaa upande wa pili wa mzani..!
Sasa wakati anakuuzia nyama au hata bidhaa nyingine kama sukari au mchele, anaweka kabisa hiyo bidhaa kabla ya kuondoa yale mawe uliyoyakuta, akishaweka hiyo bidhaa yako (kwa makadirio) hapo ndio utaona anatoa yale mawe uliyoyakuta kisha anaweka jiwe lenye kilo unazohitaji wewe (mfano kama unataka mchele wa kilo 1 basi hapo ndipo ataweka jiwe la kilo 1), halafu ataanza kubalance kwa kupunguza huo mchele au kuongezea hadi mzani ubalance.

Tafsiri
Hapo maana yake ni kwamba lile jiwe la kilo moja limebalance na uzito wa mchele wako + sumaku aliyoinasisha chini ya sahani.
Let say sumaku ilikuwa ni robo kilo, basi mchele wako ni robo tatu ya kilo.

Hapo atachukua mchele wako atakuwekea kwenye package, utaondoka na robo tatu zako ila ile robo (sumaku yake) utamuachia muuza duka
 
Ukiweza kuwa na mzani nyumbani ni vyema kwani inakusaidia sana kujua ni kwa kiasi gani umepunjwa, kama mteja wako wa kila mara unachukua tahadhari, Mama yangu alikuwa mjanja mjanja vipimo vilikuwepo nyumbani, alikuwa anapenda kupima pima.
 
Licha ya mambo ya Mizani penda kununua nyama mchana badala ya Asubui.....
Mchana na jioni maji maji na damu vinakua vmekauka kwa hiyo unanunua nyama halali....
Halali, how?
 
  • Thanks
Reactions: Oxx
Ukinunua Asubui nyama inakua na maji maji, pia inakua na damu hivyo uzito wake unakua Mkubwa, Ila ikitundikwa inakauka kwa hiyo uzito wake unapungua.......

Kilo moja ya asubui sio kilo moja ya Jioni Mkuu.......!
Ooh, ahsante kwa ufafanuzi aisee. Nitafanya hivyo.
 
Acha waibe, kama mamlaka hazifuatilie sisi tutafanyaje?

Zama hizi bado wanatumia mechanical weigh scales, mbona ipo mizani ya electronic kwanini mamlaka zisitoe agizo ikatumika hiyo au wale wakala wa vipimo wanafanya kazi gani maana unawakuta mtaani na tupa, misumeno ya chuma na vinyumdo....., jukumu lao nini kama siyo kushughulikia wizi wa aina hiyo
 
Zama hizi bado wanatumia mechanical weigh scales, mbona ipo mizani ya electronic kwanini mamlaka zisitoe agizo ikatumika hiyo au wale wakala wa vipimo wanafanya kazi gani maana unawakuta mtaani na tupa, misumeno ya chuma na vinyumdo....., jukumu lao nini kama siyo kushughulikia wizi wa aina hiyo
Hata hao mamlaka ya vipimo nao si wananunua nyama buchani au wao wanaenda na mizani zao?
 
Back
Top Bottom