Usipoweka kitunguu kwenye mchuzi nini kitatokea?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,526
3,801
Mara nyingi nimekiona kina mama wakipika mchuzi ikosekana carrot au hoho wala hawana shida lakini kikikosekana kitunguu watatafuta popote pale.

Umuhimu katika mchuzi ni upi? na kama kikikosekana nini kitatokea?
 
Ladha ya kitunguu haitokuwepo!
 
Kitunguu huwa sikipendi sana, nikiwa nakula lazima nikitoe kama kipo kwenye mboga, na nikila kwa bahati mbaya ulimi wangu upo sensitive sana lazima kitoke, utata unakuja nikienda ugenini
 
Hata mm siku nilijaribu lengo kutaka kujua itakuwaje lakini sikuweza kula huo mchuzi nilihisi kutapika tu.kiunguu ni kiungo muhimu sana kwenye mchuzi...yahni bora ukate nyanya pekee na chUmvi utakula kuliko upike mchuzi bila kitunguu matokeo mawili ukaumwage au ule utapike....
 
Hata kisipokuwepo hakuna shida,kuna watu wana allergy na vitunguu na ukipika wanakula na wengine wasiokuw ana allergy wanakula bila kujua hamna vitunguu.
 
Nenda shule ya bweni ya serikali iliyo karibu yako vizia wakat wa chakula cha mchana uone nini hua kinatokea.
 
Kitunguu huwa sikipendi sana, nikiwa nakula lazima nikitoe kama kipo kwenye mboga, na nikila kwa bahati mbaya ulimi wangu upo sensitive sana lazima kitoke, utata unakuja nikienda ugenini
Mie napenda sana kitunguu. Nikipika nayaweka mapande mapande ili nipate niyatafune vizuri. Tena hupenda kuvikaanga kdg tu ili visipotee ladha.
 
Mie napenda sana kitunguu. Nikipika nayaweka mapande mapande ili nipate niyatafune vizuri. Tena hupenda kuvikaanga kdg tu ili visipotee ladha.
Daaah kweli tuna tofautiana, mimi tangu utotoni walikuwa wananiforce kula vitunguu nikila natapika, ila kwenye kachumba(l)ri nakula (vibichi)
 
Back
Top Bottom