Usipokuwa makini Unaweza pata Mikosi, mabalaa na magonjwa Chooni!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,886
USIPOKUWA MAKINI UNAWEZA KUPATA MIKOSI, MABALAA NA MAGONJWA YA AJABU CHOONI!

Anaandika, Robert Heriel

Moja ya dalili ya mtu mwenye akili ni kujua kutofautisha vitu visafi na vichafu, vitakatifu na Najisi.
Ikiwa mtu yoyote atashindwa kutofautisha vitu hivyo basi ni kiashiria kuwa ni Mwendawazimu, mjinga Kama sio Mpumbavu.

Zipo hifadhi za vitu vitakatifu, na zipo hifadhi za vitu najisi/ vichafu. Kuweka vitu sehemu yake huitwa USAFI, UTAKATIFU.

KItu chochote kisichokuwa sehemu yake hutambulika Kama UCHAFU.
Uchafu ni lugha ya Kibaiolojia na kisayansi.
Najisi ni lugha ya Kiimani na kiroho.

Leo tutazungumzia habari ya CHOO ikiwa moja ya sehemu nyeti Kwa Binadamu.

Choo ni sehemu maalum iliyotengwa Kwa ajili ya watu kujihifadhi, kujisaidia, na kuweka uchafu wao humo.
Uchafu Kama Mavi, mikojo, mate, matapishi, na wakati mwingine wanawake hutupa ule uchafu wa desturi zao.

Licha ya kuwa Choo ni sehemu ya kuhifadhi uchafu lakini sehemu yenyewe inapaswa kuwekwa Safi.

Wapo Viumbe Safi na wapo viumbe wasio Safi, yaani viumbe Najisi, wapo viumbe walao vitu Safi na wapo viumbe walao vitu vichafu.

Mfano wa viumbe wenye kuonekana walao vitu vichafu ni pamoja na Nzi, Mende, mafinyofinyo, manyongo ambao Baadhi yao ni Bacteria waluoumbwa katika mfumo wa kukifanya kitu kioze na kuisha.

Kama walivyo viumbe hai waonekanao Kwa macho pia wapo viumbe wasioonekana kwa macho ya nyama ambao nao hupenda kuishi Mazingira machafu, sehemu najisi Kama Chooni hasa Choo kikiwa kichafu Sana, kwenye madampo na majalala, viumbe hao huitwa Pepo wachafu ambao wapo wengi kulingana na Majina na jamii zao.

Katika Viumbe wanaoonekana lakini wenye maumbile madogo yasiyoweza kuonekana Kwa macho isipokuwa utumie vifaa vya kisayansi Kama Microscope ya maabara, viumbe jamii ya Fungi(Kingdom Fungi) ambao huishi katika mwili wa Binadamu hasa kwenye utumbo mpana, au bacteria, ambao wakitoka Kwa njia ya mtu Kujisaidia(Kunya) huweza kuacha vijidudu eneo la tundu la chooni, na endapo mtu mwingine akija kukojoa hasa mwanamke majimaji yakamrukia ukeni na Wale wadudu basi anaweza kupata madhara, pia Mwanamke wakati wakutawadha kama atatawadha bila kufuata utaratibu vile vidudu vilivyokuwa kwenye Mkundu vikiingia kwenye Uke vinaweza kusababisha madhara hasa magonjwa.

Kufikia hapo unaweza kuona chooni kunaweza kuishi viumbe wanamna gani,

Madhara unayoweza kuyapata mtu akiwa Chooni!

1. MAGONJWA
Magonjwa Kama UTI mara nyingi hupatikana katika Mazingira ya chooni, kipindu pindu, na magonjwa ya Fangasi.

Fangasi hasa ya Uke imekuwa ikisumbua wanawake wengi, na wengi wanazipata chooni wakati wakijisaidia.
Nyumba za kupanga zina watu wenye Uelewa tofauti wa mambo ya Usafi na hii inapelekea tatizo la Fangasi na magonjwa ya UTI kuwa tatizo ndani ya jamii.

2. MIKOSI NA MABALAA

Pepo wachafu Kwa Aina na jamii zake, vyoo vikiwa vichafu hugeuka kuwa makazi ya viumbe wasioonekana ambao nao ni wachafu Kama vile uonavyo viumbe wanaoonekana Kama Mende na nzi chooni ndivyo halikadhalika na hao mapepo..

Chooni mtu huweza kupata Roho chafu zinazoweza kumfanya mtu kupata mikosi na mabalaa.

Ndio maana ni ngumu Sana Kwa watu wenye utambuzi na Uelewa wa mambo ya Usafi kuingia katika Choo chochote. Mtu msafi lazima awe mbaguzi na mtu mwenye kuchagua Sana.

Namna ya kuepuka madhara yatokanayo na mambo ya Chooni!

1. Safisha Choo kiwe Safi Kwa sabuni.
Hakikisha unasafisha Choo angalau mara mbili Kwa siku ikiwa Familia ni kubwa kuanzia watu watano.

2. Kama unaishi Nyumba ya kupanga yenye watu wengi. Kabla hujajisaidia Safisha Choo hasa kwenye Karo la Choo, ndipo unye au ukojoe.
Hata kama unakiona Choo ni kisafi Kwa macho yako, safisha ndipo ukitumie, tumia Sabuni ya maji kisha mwagia maji.

3. Kabla hujaingia omba Mungu akulinde na Pepo wachafu au roho wachafu ikiwa unajisaidia Choo cha mbali (kisicho cha Nyumba yako) au ikiwa mpo wapangaji wengi.

4. Mwanamke ukitawadha, jisafishe Kwa kwenda nyuma. Usisafishe kuja mbele kwenye uke, utaleta uchafu wa haja kubwa kuja Ukeni, na bacteria wa Mkunduni huweza kuwa hatari wakiingia katika Mazingira Mapya ya Ukeni. Na ndio hayo mambo ya UTI.

5. Ikiwa upo safarini ukapatwa na haja, basi tembea na Sabuni ya Maji iwe ya kununua au yakutengeneza hasa Kwa wanawake, mwagia hiyo sabuni kwenye Choo kisha umwagie maji kisha ndio ujisaidie. Kisha uwe na Tishu, Kwa Usalama usitumie Tishu za Choo usichokitambua.
Kwa wanaume Kama ni kukojoa wao hawana matatizo Sana. Labda wapige tuu Sala, pia wanawake mpige pia sala.

6. Mwanamke usitupe Uchafu wa desturi zako, pedi, au kitambaa au kifaa chochote utakachotumia kwenye Hedhi, usitupe chooni.
Kusanya kisha nenda sehemu ya kutupia takataka au kwenye pipa la kuchomea taka, miminia Mafuta ya taa kwenye huo uchafu uliotokana na desturi yako, kisha choma.

7. Mwanaume kojoa Kwa kulengesha Tundu, usikojolee pembeni.
Ikiwa unamwanaume mlevi asiyejielewa na asiye na akili za mambo hayo, basi itakupasa kila wakati Mtoto hasa wadogo akienda chooni, ukasafishe kidogo ndipo ajisaidie.

8. Baada ya kukojoa au Kunya Osha Choo Kwa kumwagia maji kuhakikisha mavi na Mkojo umeenda, kisha chukua sabuni ya maji mwagia kwenye Karo la Tundu la Choo. Kisha sugua kidogo alafu mwagia maji.

9. Safisha mikono Kwa maji na sabuni,

10. Usitumie Ndoo za wapangaji wengine hasa za kuogea, wengi huzikojolea, ni chafu.
Usijesema utazisafisha.

11. Usitumie Sabuni au Brashi au taulo la mtu mwingine.
Ikiwa unaishi Nyumba ya. Kupanga usitumie sabuni au Brashi utakalolikuta bafuni.

12. Usiache Mswaki au dawa ya Meno Bafuni au chooni. Hii ni Kwa wanaoishi kwenye Nyumba zao hasa zenye watu wengi, na Wale mliopangisha Nyumba mnaoishi wapangaji wengi

13. Sabuni au Brashi ikianguka bafuni au chooni unapooga usiikote, hasa wanaoishi Nyumba za kupangisha.
Pia tafuta kitu chakuwekea sabuni au brashi(kibebeo) usiweke Brashi au sabuni sehemu wanaoweka watu wengine.
Wengi wamepata Mba na magonjwa ya ajabu ya ngozi Kwa namna hii.

14. Usitumie bafu au Choo ambalo ni chafu au lenye maji maji, wengi wameteleza na kuanguka na kuvunjika bafuni. Iwe Kwa utelezi wa kawaida(hawa ni wengi zaidi) au kuanguka Kwa kuangushwa na mapepo wachafu (hawa ni wachache)

15. Usitumie kopo la chooni na wapangaji wengine au ndoo. Kuwa na ndoo yako na kopo lako. Vitu hivyo vihifadhi sehemu ambayo wewe pekee unaweza kuifikia.

Andiko hili linawahusu waamini na wasioamini mambo ya viumbe wasioonekana.
Niishie hapa.
Na nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
, Mkuu SEMA/QOUTE HAPA bas hiyo Dua na sisi tusio waislam tuitumie au inawasiadia waislam pekee?.

Lkn pia hujasema tunao gegeda mikosi vepe Kwa sababu hata kugegedana Kuna sababisha ikiwa umekutana na Mtu ambaye sio partner wako..mweny kisrani. Ukataabika wewe maisha yako yote.. ukamaliza waganga, na waganga wakakutwisha mikosi mingine Mkuu ukatembea mtaani Bora kichaa kuliko wewe
 
Wapo Viumbe Safi na wapo viumbe wasio Safi, yaani viumbe Najisi, wapo viumbe walao vitu Safi na wapo viumbe walao vitu vichafu.

Mfano wa viumbe wenye kuonekana walao vitu vichafu ni pamoja na Nzi, Mende, mafinyofinyo, manyongo ambao Baadhi yao ni Bacteria waluoumbwa katika mfumo wa kukifanya kitu kioze na kuisha.
Mtaalamu wetu tuambie tunajifunza nini kutoka kwa fungofungo ambaye lazima akagonge mhuri eneo lilelile aliloanzia hata kama ni Km 100 atajiziba na vigunzi
 
Back
Top Bottom