Tabu ni kwamba hapa wengi wanadhan sie tunapinga hvi tunataka hela, ila ukwel tunajaribu kuwaeleza watu wenye tabia hii ni mzigo kwa namna gani, ili mabinti wawe na tahadhari na hlo, mapenzi/ndoa haingalii pesa ila upendo wa dhati, uvumilivu na ustahimilivu wa mambo, unaweza kuwa na mwanaume ambaye anakipato kidogo kabisa lakin akawa ni mtu mwenye anayejal familia, atajitahid kuifanya familia iwe na amani muda tuchukulie mtu anayepoke kima cha chin 180000 akaja nyumbani akatoa hata 80000 tu labda mama mwl anapokea 240000 take home, nikimaanisha labda anamkopo ndio maana akapata 240000 hv hiyo 80000 haita msaidia mama kujiongeza hapo katika bajet yake kulinga na maisha yao? itakuwa sawa na kubwa jinga ambalo linapokea 900000 alafu bado linapiga mizinga? huyu ni mwanaume wa kumvumilia? hebu wakaka kuwen wakwel hapo,hayo ni mahaba nifilisi kama si ujinga, ukwel ni kwamba akina kaka wengi mnamaliza pesa zenu kwenye starehe za kijinga kama pombe, kujifanya mnajua kutumia pesa bar sijui mnataka sifa kwa ma barmeid, Hakuna binadam asiejua kupenda na thaman ya kupendwa lakin lazim kila mmoja ajue wajibu wake hata kwakuchangiana kiduchu, Nyie wanaume mlilalamika kuwa wanawake ni magoli kipa, sie tukajiongeza ili maisha yaende. sasa mmekutwa na yapi hadi kujisahau na kuwa tegemezi tena?
Note: sio wanaume wote ni wale tegemez ndio walengwa