Usipoacha alama Duniani nini kitatokea?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,965
Nimesikia mara nyingi mijadala ya watu na hasa motivational speakers wakisisitiza ni muhimu kuacha alama hapa duniani.

Watu wengine wanapigana kuacha ukoo mkubwa kwa kuhakikisha wanazalisha wanawake wengi iwezekanavyo.

Wengine wanateseka sana kwa kukosa mtoto wa kiume ingawa matajiri huko duniani wana watoto wa kike tu na hawawazi yanayotusumbua.

Watu wengine wanalazimika kuwa wakatili dhidi ya wapenzi wenzi wao wa ndoa kisa mmoja wao amekosa uzazi,na wanalazimika kuvunja viapo vya ndoa ili wakatimize azma yao ya kuujaza ulimwengu na watu wengine.

Je, nini maana na maksudi ya maisha?
Kuna tuzo yoyote kuacha alama hapa duniani?

Kwani ukiishi kwa unyenyekevu pasipo kutafuta makuu na mashindano yasiyo ya msingi,na ukaishi bila kuacha alama nini kiratokea?

Ninaona binadamu anafanya mambo mengi yasiyo na faida na kujilisha upepo tu
 
Back
Top Bottom