Usipende kuwa wa kwanza "ku-update" simu au acha kabisa!

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
6,661
20,995
Nimetumia neno UPDATE kwenye heading sababu wengi ndio tumelizoea, lakini hasa nitazungumzia UPGRADE.

Japokua vyote vinalenga katika kuleta mabadiliko kwenye kifaa chako(hapa nitazungumzia simu tu) ila ni vitu viwili tofauti ambavyo utofauti huo hutokana na aina ya hayo mabadiliko.

UPDATE
Hili neno sio geni, update hufanyika mara kwa mara kwenye simu na mda mwingi hua inaweza ikajiendesha in background.

Update inahusisha maboresho madogo madogo yaliyopo kwenye software, application au OS iliyopo, mfano security breach, malware, errors fix, ku support drivers, new hardware n.k,

Chukua mfano hacker ametengneza kirusi cha kimtandao, ambacho ukifungua tuu kinaharibu ufanisi wa simu, wizi wa data n.k,
Sasa wenye app, OS au software wakigundua wanashusha update mpya ili kukikwepa na kutengeneza security mpya kuepuka mashambulizi mengine ya kimtandao.

Hapa ndio unakuja kuona kazi ya update ni kufanya repairing/kuboresha mfumo unavyofanya kazi ila si kubadilisha, ndio maana inahitaji software/OS iliyopo ili iweze kufanya hio kazi(update), Mfano wa update ya android version ni kutoka OS 8.0 kwenda 8.1.
Mfano wa update ya app Ni Jf version 8.8.50 kwenda 8.8.60.

UPGRADE
Haya ni mabadiliko makubwa kwenye Operating system ya simu mfano kutoka android 8.0 kwenda 9.0, hapa unabadilisha android version ya simu. Hapa sio repairing tena ni changes, kupata new features, enhanced functionality (edition), na hii haihitaji mfumo uliopo ili ku upgrade.

Chukulia mfano wewe kila siku unakaza nati na kuweka oil kwenye engine hii ni update, halafu mwingine akabadilisha engine kabisa hii ni upgrade.

Au hii...
Ukiwa una pesa ili ziendelee kukua kutokana na challenges inahitaji uboreshe mbinu(UPDATE)

Ukiwa Huna pesa unahitajika kubadilisha mfumo wako wa maisha ili uzipate(UPGRADE)

Nimetumia muda mwingi hapo kwenye differences ili kufanya lengo la uzi kua fupi.

Kwa nini nakuambia kama hakuna ulazima usi UPGRADE.

Ipo wazi lengo la update & upgrade ni zuri, kama nilivyokwishasema hapo juu.

Na Update/upgrade yoyote inapokuja anakupa na hints kabisa
"Whats new"

Wengi wetu hatusomi, tunakimbilia ku upgrade/update tu,

Inapaswa usome na kuelewa ni kitu gani kipya utapata baada ya upgrade...

Kama kuna kitu unaona ulikua unakikosa na sasa kipo basi ni chaguo lako, kama unaona kila kitu kilichopo hakina effect yoyote kwenye matumizi yako basi nakushauri achana na hio update kwanza,

Ninachoweza kushauri wote hawa wawili ni kujipa mda kidogo kupata reviews sio kutaka kua wa kwanza ku upgrade/update...

Naandika hivi kwakua, baada ya update kua released ma developers wenyewe wataipitia kwa undani hasa kuchunguza kama inafanya kazi kama ilinavyotakiwa? kama sivyo wataweka tangazo la kuleta update mpya ili kuiboresha au kuondoa tatizo lililojitokeza, lakini pia jaribu kupitia user reviews za sites tofauti tofauti kama Gsmarena, Gadgets now n.k kule utakuta mirejesho ya watu waliokwisha upgrade.

Matatizo na malalamiko makubwa utakayokutana nayo ambayo hapo kabla hayakuwepo ni...

1. Simu kuisha battery haraka
2. Simu kupata joto sana,
3. Simu ku stack na kua slow
4. Simu kujizima,
5. Shida kwenye kamera,
7. Kusumbuliwa na matangazo mara mwa mara.
8. Kupoteza network,
9. Kuchukua storage kubwa.

Na mambo mengine mengi, ambayo mwanzo hujawahi yaona kwenye simu yako na hapa wengi ni mashahidi.

Ndio tunajua moja ya Lengo la update/upgrade ni kutatua matatizo kama security issues, crushing and lagging etc, lakini ikiwa wamefanikiwa ku fix hayo, kuna uwezekano mkubwa kulifanyika makosa katikaa uundwaji na hatimaye wanakuletea na shida kama hizo hapo juu.

Wakigundua wao wenyewe au kutokana na malalamiko ya watumiaji basi haraka wanashusha update ili kurekebisha, hapo napo kuna mawili, either kweli watatue hilo tatizo(kwa baadhi ya issues hua wanashindwa kabisa) au ndio yaongezeke mengine..

Hua wengi wanatamani kurudi tena nyuma(downgrade) ila tatizo ni kwamba hio huduma haipo official,
Kuna njia za kimtaani ila ni risk.

Hapa sasa ndio utaanza kuichukia simu yako, na ndio unapokuja ushauri ya kua kama huna unachokikosa kwenye simu yako, basi achana na masuala ya update, au basi jipe mda kwanza kupata mirejesho.

NOTE : Sio mara zote unaweza kukutana na hizo shida kila unapo update, na pia kuna baadhi ya update zina athili aina flani tuu za simu.

Update/upgrade moja kwa moja inaingilia mfumo wa utendaji kazi wa simu, ambao huongozwa na vitu kama Processor na RAM ambavyo kwa vyovyote vile vitaathirika hasa kwenye speed na Space,
Kwa kujua ya kua kuna simu zitashindwa ku copy with new features ndio maana hua wanaandika kabisa update/upgrade ni kwa matoleo gani,
Sasa ikatokea katika yale matoleo yaliyo orodheshwa lako ndio la mwisho katika quantification za kupata update basi uwezekano wa kusumbuka ni mkubwa, sababu uwezo wa processor na ram yako ni mdogo, kuendana na new features.
Na shida ya kwanza ni simu kua slow, ku stack kupata joto etc.
 
Kuna updates ni must have, features zake zinashawishi, mfano Android 6, 8 na hii 12 kwangu ni worth it kwa mtu aki update mapema,

Ila hii android 11 ilikuwa ni majanga, hasa kwa power users, ngoja tuone 12 itakuaje ila so far inaonekana itakuwa nzuri sana.
 
Kuna updates ni must have, features zake zinashawishi, mfano Android 6, 8 na hii 12 kwangu ni worth it kwa mtu aki update mapema,

Ila hii android 11 ilikuwa ni majanga, hasa kwa power users, ngoja tuone 12 itakuaje ila so far inaonekana itakuwa nzuri sana.
Yaps, kuna baadhi ya upgrade zinakua major changes, ila nyingine ni uongo tuu..

Android 5 & 11 ni moja ya android versions za hovyo kabisa kuwahi kutoka.
 
Vipi Sisi wa Tecno huu Uzi unatuhusu?
Tecno updates zake ni malware, simu yako nzima uki update wanakujazia matangazo na spyware


Tena walivyo wajanja Wana target Africa kabisa sababu sisi tunasubiria mpaka mzungu aje Africa akishika simu akiona malware aka report vyombo vya Habari.
 
Yaps, kuna baadhi ya upgrade zinakua major changes, ila nyingine ni uongo tuu..

Android 5 & 11 ni moja ya android versions za hovyo kabisa kuwahi kutoka.
Kwa hiyo mkuu unashauri nini hapo.. Tusinunue simu ambazo zinatumia android version ya 11.maana mimi natafuta simu mpya.. Au nichukue iPhone?
 
Niliupdate A50 yangu toka Android 9 kwenda 10 ikapoteza uwezo wa kurecord calls automatic hadi leo, betri ndo usiseme, zile updates ndogondogo ndio zikairejesha angalau.
Nilipoipeleka Android 11 ikaanza kusumbua network yaan inazidiwa na nokia tochi simu nmenunua laki 6 inankera kweli.
Bora waruhusu hiyo downgrade iwe official asee ningerudi zangu nyuma.
 
Tecno updates zake ni malware, simu yako nzima uki update wanakujazia matangazo na spyware


Tena walivyo wajanja Wana target Africa kabisa sababu sisi tunasubiria mpaka mzungu aje Africa akishika simu akiona malware aka report vyombo vya Habari.
Naona umewapiga watu na kitu kizito kwenye utosi
 
Infinix will launch smartphone periscope camera and 160W fast-charging Infinix will launch smartphone periscope camera and 160W fast-charging
Tayari USB association wameshatangaza version Mpya ya USB type C inasupport watts 240,

Source hii

Baada ya kutangaza ndio unaona manufacture mbalimbali na wao wanajitapa na hizi charger alianza Xiaomi na 200w, hao kina Infinix etc.

Hivyo hii ni tech mpya inakuja kwenye simu, laptop, na vifaa vyote vya type C USB zake zitapokea umeme mpaka hizo watts 240.
 
Tayari USB association wameshatangaza version Mpya ya USB type C inasupport watts 240,

Source hii

Baada ya kutangaza ndio unaona manufacture mbalimbali na wao wanajitapa na hizi charger alianza Xiaomi na 200w, hao kina Infinix etc.

Hivyo hii ni tech mpya inakuja kwenye simu, laptop, na vifaa vyote vya type C USB zake zitapokea umeme mpaka hizo watts 240.
Tutakuwa tuna charge simu kwa dakika 5 tu 0-100
 
Back
Top Bottom