"Usiondoe mpaka wa mwenzako." Mpaka gani?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,030
50,932
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani mwanasheria.

Maneno haya yamepimwa, yamefanyiwa uchunguzi wa kina, nami nitayawasilisha kwa kadiri niwezavyo yasipungue, kwani hii ndiyo hesabu yake.

Kwa maana kila jambo lina njia na nafasi yake. Na kila njia na nafasi inawakati wake. Na kila kimoja kina matokeo yake, naam ndiyo mwisho wake. Na kila mwisho mmoja ndio mwanzo wa Jambo jingine. Na hayo yote yana kusudi lake. Na wala hakuna Jambo au kitu chochote kisicho na kusudi/sababu mpaka kutokea.

Niite Taikon wa Fasihi, mwanafalsafa kutoka Nyota ya Tibeli, nyota ing'aayo yenye mbawa mbili zenye nguvu, irukayo kutoka Ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Nimekuandikia haya, upate maarifa, hekima, na ufahamu; utakaokusaidia katika mipango yako, malengo yako, mikakati yako, na katika kuishi kwako kwa ujumla. Wala isihesabike nalitaka faida yoyote kwako, basi usome kwa akili kwani andiko hili litahusu mambo yapatanayo na akili.

Tena sitaki nikuburuze na kukufanya uwe mtumwa wangu, bali uwe huru kuiruhusu akili yako kunikosoa kwa akili ikiwa utaona jambo lolote lisilopatana na akili yako. Kwa maana hivyo ndivyo Watibeli tulivyo. Hatuwi watumwa wa watu wengine, tena hatuwi watumwa wa mambo yasiyopatana na akili zetu, hata kama zingekuwa ni akili ndogo.

Mpaka ni nini?
Mpaka ni ukomo au mwisho wa Jambo moja unaotenganisha Jambo jingine. Hakuna Jambo duniani lisilo na mpaka isipokuwa lile lililoumba hiyo mipaka. Yote yaliyobakia yanamipaka yake, yaani yanaukomo na mwisho wake.

Bado hujamwelewa Taikon? Subiri utanielewa.

Aina za mipaka

Zipo Aina nyingi za mipaka, lakini kuu ni kama ifuatavyo;
1. Mipaka wa Kijiografia
2. Mipaka ya Kimahusiano
3. Mipaka ya Kimaumbile
4. Mipaka ya Kisaikolojia

1. Mipaka ya Kijiografia
Hii ndio mipaka ambayo ni maarufu Kwa wengi. Wengi hujua mipaka ya viwanja na mashamba Yao, mipaka ya Nchi zao. Zipo kesi nyingi mahakamani zinazohusu migogoro ya mipaka ya Ardhi. Hata hivyo zipo nchi zinamigogoro ya mipaka ya Nchi zao au kugombea baadhi ya Maeneo Fulani.

Mipaka ya kijiografia ni mipaka inayohusu ukomo unaotenganisha eneo moja na eneo jingine. Kutengenganishwa huko kunatokana na utofauti wa maeneo hayo mawili.

Utofauti unaweza kuwa katika;
i. Utofauti ulioletwa na tabia za nchi kama ujangwa, uikweta, utropiki n.k, ambapo kila tabia inaupekee wake unaotofautiana na tabia ya nchi nyingine. Tabia za nchi hupelekea pia utofauti wa viumbe vinavyopatikana katika maeneo hayo.

ii. Utofauti wa rangi ya udongo. Rangi ya udongo ni moja ya vitu vinavyoashiria mipaka ya kijiografia, tofauti ya miamba asilia ndio huunda utofauti wa udongo. Unaweza fika eneo moja likawa na udongo mwekundu, kwingine udongo mweupe, kwingine udongo mweusi n.k.

iii. Utofauti wa watu na viumbe.
Mipaka ya maeneo pia huangalia utofauti wa viumbe na watu. Mfano, eneo moja utakuta watu wanaongea lugha fulani na wanamionekano fulani huku eneo jingine likiwa na watu wenye lugha nyingine na mionekano mingine.

Kwa mfano, kule kwetu Upareni, hasa Makanya kwetu😊 watu huzungumza kipare, kadiri unavyoondoka kwenda Kusini mpaka unafika mji wa Mombo Kipare kinapotea polepole na kisambaa kinashika haramu.

Ingawaje Kisambaa na Kipare kinafanana kwa kiasi kikubwa kutokana na ukaribu wa kimaeneo, lakini kadiri unavyosonga kuliacha eneo la Upareni mfano ukafika mpaka Morogoro kwa Luguru, Kipare kinakufa kabisa, yaani Mluguru akiongea 95% hawezi kueleweka na Mpare. Ila msambaa akiongea Kisambaa basi Mpare atamuelewa kwa 50% ni kutokana wanakaribiana.

Tofauti za kijiografia ndizo huzalisha tofauti za kiutamaduni na kimahusiano, ingawaje viumbe wanaweza kuwa wa asili moja, yaani wote ni wanadamu lakini wakawa na mipaka yao.

Ni kosa kisheria, siyo tuu hizi sheria zetu tulizotunga sisi wanadamu tunazoziita sheria za Serikali, ni kosa kwa sheria za asili kuondoa mipaka ya kijiografia. Ni mtu mjinga pekee na mpumbavu ambaye atafikiri kuondoa mipaka ya kijiografia asijue madhara ya kile akifanyacho.

Madhara ya kuondoa mipaka ya kijiografia siyo tuu kuleta vita na umwagaji wa damu bali pia kuleta machafuko ya kimaadili, kigenetiki, na kiafya.

Biblia inasema;
Kumbukumbu la Torati 19:14
[14] Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki.

"Thou shalt not remove thy neighbour's landmark, which they of old time have set in thine inheritance, which thou shalt inherit in the land that the Lord thy God giveth thee to possess it."

2. Mipaka ya Kimahusiano
Mahusiano ya mume na mke, mzazi na mtoto, mwajiri na mwajiriwa, kiongozi na mwananchi, mahusiano ya Mungu na mwanadamu. Katika mahusiano kuna mipaka, mipaka ya wajibu na majukumu.

i. Mpaka wa Mume na Mke
Ili mahusiano yoyote yadumi na yawe na tija, ni sharti mipaka kuzingatiwa. Usiondoe mpaka wa mume wako ndani ya ndoa, na wala usiondoe mpaka wa mkeo katika familia yako.

Ni kosa kwa sheria za asili kuondoa mpaka wa mwenza wako, na adhabu lazima uipate. Raha ya hukumu na adhabu za nature hutoa hukumu za haki. Na wala hakunaga mijadala. Ukikosea lazima uwajibishwe.

Hata hivyo kwenye mipaka ya kimahusiano kuna kukaimishana, kukodishana wajibu na majukumu kwa muda ili kufanya mambo yaende. Kwa mfano, baba anaouwezo wa kumruhusu mama/mkewe aingie katika mpaka wake(afanye baadhi ya wajibu au majukumu yake, ya baba) kwa muda fulani ikiwa baba anamajukumu mengi mengine.

Au mama akamruhusu mume wake aingilie baadhi ya mipaka yake kwa muda kwa mustakabali mzuri wa mipango ya familia. Hiyo inaruhusiwa kwa sababu ni makubaliano, siyo dhulma.

Ni kama nchi moja kuomba msaada kutoka kwa nchi nyingine. Mfano Msumbiji imeomba msaada wa Jeshi la Rwanda kusaidia kupambana na magaidi. Au Ukraine imeomba msaada wa kijeshi kwa mataifa ya Ulaya kupambana na uvamizi wa Urusi.

Kisheria hairuhusiwi jeshi la nchi moja kufanya kazi katika nchi nyingine. Yaani Jeshi la Kenya lifanye kazi Tanzania. Huko ni kuvuka mipaka. Ila Tanzania inayoruhusa kuomba msaada wa kijeshi kwa nchi nyingine. Na hiyo ni kwa muda Fulani. Hiyo ni mipaka ya mahusiano ya nchi na nchi.

Ndivyo ilivyo hata katika mipaka ya mahusiano ndani ya ndoa. Baba anauwezo WA kuomba msaada Kwa mkewe, na isionekane kuwa Mke kavunja au kuondoa mpaka wa mumewe. Jambo ambalo litaitwa uhaini au uvunjifu wa Amani.

ii. Mpaka wa mzazi na mtoto
Mzazi anaukomo wa mamlaka yake kwa watoto aliowazaa. Mtoto akishafikisha umri wa kujitegemea, akajitegemea na kuanzisha maisha yake, mzazi hana mamlaka yoyote ya kumuingilia mtoto wake kivyovyote.

Tayari mtoto huyo ni taifa huru, anatakiwa kuendesha maisha na familia yake atakavyo, siyo utakavyo wewe, mzazi. Ukifika nyumbani kwa mtoto wako, wewe unabaki kama mgeni tuu usiye na amri wala mamlaka yoyote ndani ya nyumba ya mtoto wako.

Utafuata amri, sheria na taratibu za nyumba ya mtoto wako, akiwemo mkwe wako. Masuala ya kusema nimekuzaa, sijui nilikuweka tumboni, hapo hayana maana yoyote.

Mzazi utabaki kama mshauri tuu. Kuingilia mambo ya nyumba ya mtoto wako ni kuondoa mpaka wa jirani yako, hilo ni kosa siyo tu kidini bali pia hata nature haitaruhusu jambo hilo kutokea. Na itakuadhibu vyema.

Mzazi yeyote anayeleta chokochoko na kuingilia sovereignty power ya serikali ya mtoto wako unajitengenezea bomu baya hapo baadaye. Ukitaka watoto wako wakupende, basi heshimu mipaka ya mahusiano yenu. Bali kuwa mzazi na yeye abaki kuwa mtoto, wewe endelea kumshauri na siyo kila mara. Kukushauri mtu mzima jambo lilelile ni kumshinikiza. Ni kuingilia mamlaka yake.

iii. Mpaka wa Mungu na Mwanadamu
Ni kosa kisheria kuondoa mpaka wa Mungu wako kwako. Upo wajibu na majukumu ya Mungu aliyekuumba kwako, na wewe unaowajibu na majukumu uliyopewa kwa Mungu wako. Ni kosa kubwa kuingilia au kuondoa mipaka hiyo.

Mungu kuna mambo hawezi kukuingilia kamwe, anajua unauhuru kwa baadhi ya mambo, lakini hata yeye anauhuru na hataki kuingiliwa anapofanya wajibu na majukumu yake. Ni vyema kujifunza kujua wajibu na majukumu yako kwa Mungu. Kujua wajibu na majukumu ya Mungu kwako.

Ni kosa kisheria za asili kuabudu miungu migeni ilhali Mungu wako aliyekuumba yupo. Kama unavyojihisi maumivu mkeo akichakatwa na kubinuliwa binuliwa na mhuni ndivyo Mungu wako anavyojihisi wivu. Kama unavyojisikia mumeo akilala na wanawake wengine ndivyo Mungu anavyojisikia. Unajua matokeo ya wivu wa mapenzi yalivyo?

Moja ya jukumu na wajibu wa Mungu ni kukusaidia wewe kiumbe wake. Lakini nawe unaowajibu wa kumuabudu.
Kwa nini uende kwa waganga kuomba msaada ilhali Mungu wako yupo?

Embu fikiria umezaa mtoto Aldi mtoto huyo anaenda kwa majirani kuombaomba hovyo, unajisikiaje? Bila Shaka unahisi kudhalilishwa, kuabishiwa. Ndivyo ilivyo kwa Mungu aliyekuumba.

Soma
2 Wafalme 1:16
[16]Akamwambia, Bwana asema hivi, kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, Mungu wa Ekroni, je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

Abudu kwa Mungu aliyekuumba, maisha yasikufanye uvuke mipaka. Ni sawa na kijana anayetafuta maisha akaacha kufanya shughuli halali halafu anafanya shughuli haramu kwa kisingizio cha kutafuta maisha na kupata Pesa. Hilo ni kosa kisheria.

3. Mipaka ya Kisaikolojia
Hii ni mipaka inayohusu akili na tabia za viumbe hasahasa binadamu. Ipo akili na tabia ya kike na ya kiume.
Ipo akili na tabia ya kitoto na mtu mzima au mzee. Kila mtu hapaswi kuondoa mpaka wake au mpaka wa mwenzake.

Mtoto anayohaki ya kufikiri na kutenda kama mtoto. Ila hapaswi kutenda mambo yawapasayo watu wazima. Mfano mtoto mdogo hapaswi kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi kwani mapenzi yanawahusu watu wazima wenye akili iliyokomaa na wenye uwezo wa kukabiliana na matokeo na hekaheka za mapenzi.

Ni kosa kisheria hasa sheria za asili mtoto kutenda mambo ya kikubwa. Mfano mtoto akijiingiza kwenye mapenzi halafu akapata mimba, ni wazi mtoto atakayemzaa hataweza kumhudumia. Na hii itaathiri mwenendo mzima wa maisha yake na wale wanaomzunguka.

Pia mtu mzima hapaswi kutenda au kufikiri kama mtoto mdogo. Hii itaathiri maamuzi na utendaji wake katika majukumu yake kama mtu mzima. Mfano, mwanaume mwenye akili za kitoto huweza athiri familia yake kwa sababu watoto akili zao mara nyingi ni ndogo, fupi, zinafanya jambo pasipo kuangalia matokeo.

Siyo ajabu kijana mwenye akili ya kitoto anaweza kuendesha gari kwa kasi bila kufikiri kuwa ajali mbaya inaweza kutokea halafu naye anafamilia inayomtegemea, yaani ni kama mtoto mdogo asiye na maarifa makubwa. Huko ni kuondoa mpaka wa akili na tabia yako, ni kosa kisheria.

Mwanaume lazima ubaki katika mipaka yako. Fikiri kama mwanaume, kuwa na tabia za mwanaume. Siyo unafikiri na kutenda mambo kama jike. Hilo ni kosa kisheria za asili, na huo huitwa ushoga. Kuwa Mwanaume, kwa wasiyojua maana ya mwanaume ni kuwa na nguvu usiwe legelege kama demu. Hapo unaingilia haki za wanawake.

Wanawake ndiyo wanahaki zote kuwa legelege, lainilaini, warembo, wazuri, wapole, watamu n.k. Sasa mwanaume mzima unataka kulelewa kama mwanamke, huko ni kuvunja sheria za asili na lazima ulipie. Lazima mkeo na watoto wakudharau.

Kuna vijana wasiyo na akili wanasema wanawake wakipata vipato wanakuwa na jeuri. Mwanamke kiasili humdharau mwanaume asiye mwanaume bila kujali unahela au hauna. Kama haujielewi wanawake hawanaga simile, hawanaga kupindisha mambo, watakudharau tuu. Kiufupi wanawake hawanaga kitu inaitwa uvumilivu. Ukiona mwanamke anakuvumilia ujue bado anaona unauanaume ndani yako.

Wanawake hudharauliana, hivyo ukiona mwanamke wako anakudharau ujue anakuona kama mwanamke mwenzake. Unaingilia mipaka yao unataka wakufanyaje, wakuchekee, lazima wakuchukie, wakudharau na watafute namna ya kukukomesha.

Kama sisi wanaume tunavyowachukulia wanawake wanaojifanya wanaume, ndivyo pia wanawake wanavyotuchukulia wanaume tunapovuka mipaka yetu kiutendaji na kitabia na kufanya kama wao.

Kiasili mwanamke hamshindi akili mwanaume. Hilo hata wao wanalijua. Hivyo mwanamke akiona anakuzidi akili moja kwa moja anakutoa kwenye ile listi ya wanaume anakuweka kwenye kundi la wanawake wenzake.

Mwanamke siku zote huishi kwa furaha na mwanaume kamili. Aliyemzidi maarifa, akili, uwezo wa kujitawala kihisia, kiakili, kiroho na kimwili.

Kusema mwanamke anamzidi mwanaume akili ni ujanja wa kuwasifia na kuwapaka mafuta wanawake kwa mbongo wa chupa. Ila ukweli ni kuwa wao wenyewe wanajua uwezo wao wa akili ni mdogo ukilinganisha na wanaume.

Sasa kama huna akili za kutosha kumzidi mwanamke utaweza kweli kumtawala? Kumbuka wanawake wanapenda kutawaliwa haswa.

4. Mipaka ya Kimaumbile

Hii tutaendelea wakati ujao.

Pole na hongera kwa andiko refu. Bila shaka umepata mawili matatu.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Maneno yamepimwa na yamepitishwa.

Je, huwa unapima kuwa maandishi yako tunayaelewa?
 
Hakuna outside the box.
Kila kitu kiko limited
not limited to everything, not to all the people and not to all the time - Ideally kusingekuwa na uvumbuzi wa mambooo kabsaaaa

mara nyingi sana mipaka imewekwa ili kupunguza ugomvi baina ya nchi/watu/taasisi/majirani/marafiki/nduguuu

ni taratibu za jamii ziheshimiwee -
 
Hiyo point kuhusu ukubwa wa akili kati ya me na ke ni sahihi. Nina best yangu hivi mwanamke akawa anasema siku moja hivi

"mchumba ako ana raha maana unajua vitu vingi."

Mkuu mimi ni nani hadi nipinge hili??
 
not limited to everything, not to all the people and not to all the time - Ideally kusingekuwa na uvumbuzi wa mambooo kabsaaaa

mara nyingi sana mipaka imewekwa ili kupunguza ugomvi baina ya nchi/watu/taasisi/majirani/marafiki/nduguuu

ni taratibu za jamii ziheshimiwee -

Outside the box mara nyingi zinamaanisha Kuacha uvivu na uzembe. Na si vinginevyo.

Kila kitu kina mipaka yake,
Akili ya Mtu inaukomo wake hata hivyo watu wanatofautiana AKILI. Hivyo kila mtu anaukomo wake.

Ukiona mtu anakuambia fikiria outside the box basi fahamu kuwa anakuambia Acha uvivu au uzembe, Jitahidi zaidi kufikiri zaidi ya hapo ulipofikiri kwamba bado haujafikia Limit yako.

Mfano akili yako ni GB 100
Alafu umetumia GB 10 hivyo bado GB 90.
Hapo ndio unaambiwa Fikiri nje ya box yaani malizia hizo GB 90 zilizobakia.

Hauwezi fikiria zaidi ya kipiml au uwezo wa Akili yako hiyo haitokuja kutokea KAMWE.
 
Safi
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani mwanasheria.

Maneno haya yamepimwa, yamefanyiwa uchunguzi wa kina, nami nitayawasilisha kwa kadiri niwezavyo yasipungue, kwani hii ndiyo hesabu yake.

Kwa maana kila jambo lina njia na nafasi yake. Na kila njia na nafasi inawakati wake. Na kila kimoja kina matokeo yake, naam ndiyo mwisho wake. Na kila mwisho mmoja ndio mwanzo wa Jambo jingine. Na hayo yote yana kusudi lake. Na wala hakuna Jambo au kitu chochote kisicho na kusudi/sababu mpaka kutokea.

Niite Taikon wa Fasihi, mwanafalsafa kutoka Nyota ya Tibeli, nyota ing'aayo yenye mbawa mbili zenye nguvu, irukayo kutoka Ulimwengu huu mpaka ulimwengu mwingine.

Nimekuandikia haya, upate maarifa, hekima, na ufahamu; utakaokusaidia katika mipango yako, malengo yako, mikakati yako, na katika kuishi kwako kwa ujumla. Wala isihesabike nalitaka faida yoyote kwako, basi usome kwa akili kwani andiko hili litahusu mambo yapatanayo na akili.

Tena sitaki nikuburuze na kukufanya uwe mtumwa wangu, bali uwe huru kuiruhusu akili yako kunikosoa kwa akili ikiwa utaona jambo lolote lisilopatana na akili yako. Kwa maana hivyo ndivyo Watibeli tulivyo. Hatuwi watumwa wa watu wengine, tena hatuwi watumwa wa mambo yasiyopatana na akili zetu, hata kama zingekuwa ni akili ndogo.

Mpaka ni nini?
Mpaka ni ukomo au mwisho wa Jambo moja unaotenganisha Jambo jingine. Hakuna Jambo duniani lisilo na mpaka isipokuwa lile lililoumba hiyo mipaka. Yote yaliyobakia yanamipaka yake, yaani yanaukomo na mwisho wake.

Bado hujamwelewa Taikon? Subiri utanielewa.

Aina za mipaka

Zipo Aina nyingi za mipaka, lakini kuu ni kama ifuatavyo;
1. Mipaka wa Kijiografia
2. Mipaka ya Kimahusiano
3. Mipaka ya Kimaumbile
4. Mipaka ya Kisaikolojia

1. Mipaka ya Kijiografia
Hii ndio mipaka ambayo ni maarufu Kwa wengi. Wengi hujua mipaka ya viwanja na mashamba Yao, mipaka ya Nchi zao. Zipo kesi nyingi mahakamani zinazohusu migogoro ya mipaka ya Ardhi. Hata hivyo zipo nchi zinamigogoro ya mipaka ya Nchi zao au kugombea baadhi ya Maeneo Fulani.

Mipaka ya kijiografia ni mipaka inayohusu ukomo unaotenganisha eneo moja na eneo jingine. Kutengenganishwa huko kunatokana na utofauti wa maeneo hayo mawili.

Utofauti unaweza kuwa katika;
i. Utofauti ulioletwa na tabia za nchi kama ujangwa, uikweta, utropiki n.k, ambapo kila tabia inaupekee wake unaotofautiana na tabia ya nchi nyingine. Tabia za nchi hupelekea pia utofauti wa viumbe vinavyopatikana katika maeneo hayo.

ii. Utofauti wa rangi ya udongo. Rangi ya udongo ni moja ya vitu vinavyoashiria mipaka ya kijiografia, tofauti ya miamba asilia ndio huunda utofauti wa udongo. Unaweza fika eneo moja likawa na udongo mwekundu, kwingine udongo mweupe, kwingine udongo mweusi n.k.

iii. Utofauti wa watu na viumbe.
Mipaka ya maeneo pia huangalia utofauti wa viumbe na watu. Mfano, eneo moja utakuta watu wanaongea lugha fulani na wanamionekano fulani huku eneo jingine likiwa na watu wenye lugha nyingine na mionekano mingine.

Kwa mfano, kule kwetu Upareni, hasa Makanya kwetu😊 watu huzungumza kipare, kadiri unavyoondoka kwenda Kusini mpaka unafika mji wa Mombo Kipare kinapotea polepole na kisambaa kinashika haramu.

Ingawaje Kisambaa na Kipare kinafanana kwa kiasi kikubwa kutokana na ukaribu wa kimaeneo, lakini kadiri unavyosonga kuliacha eneo la Upareni mfano ukafika mpaka Morogoro kwa Luguru, Kipare kinakufa kabisa, yaani Mluguru akiongea 95% hawezi kueleweka na Mpare. Ila msambaa akiongea Kisambaa basi Mpare atamuelewa kwa 50% ni kutokana wanakaribiana.

Tofauti za kijiografia ndizo huzalisha tofauti za kiutamaduni na kimahusiano, ingawaje viumbe wanaweza kuwa wa asili moja, yaani wote ni wanadamu lakini wakawa na mipaka yao.

Ni kosa kisheria, siyo tuu hizi sheria zetu tulizotunga sisi wanadamu tunazoziita sheria za Serikali, ni kosa kwa sheria za asili kuondoa mipaka ya kijiografia. Ni mtu mjinga pekee na mpumbavu ambaye atafikiri kuondoa mipaka ya kijiografia asijue madhara ya kile akifanyacho.

Madhara ya kuondoa mipaka ya kijiografia siyo tuu kuleta vita na umwagaji wa damu bali pia kuleta machafuko ya kimaadili, kigenetiki, na kiafya.

Biblia inasema;
Kumbukumbu la Torati 19:14
[14] Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo Bwana, Mungu wako, uimiliki.

"Thou shalt not remove thy neighbour's landmark, which they of old time have set in thine inheritance, which thou shalt inherit in the land that the Lord thy God giveth thee to possess it."

2. Mipaka ya Kimahusiano
Mahusiano ya mume na mke, mzazi na mtoto, mwajiri na mwajiriwa, kiongozi na mwananchi, mahusiano ya Mungu na mwanadamu. Katika mahusiano kuna mipaka, mipaka ya wajibu na majukumu.

i. Mpaka wa Mume na Mke
Ili mahusiano yoyote yadumi na yawe na tija, ni sharti mipaka kuzingatiwa. Usiondoe mpaka wa mume wako ndani ya ndoa, na wala usiondoe mpaka wa mkeo katika familia yako.

Ni kosa kwa sheria za asili kuondoa mpaka wa mwenza wako, na adhabu lazima uipate. Raha ya hukumu na adhabu za nature hutoa hukumu za haki. Na wala hakunaga mijadala. Ukikosea lazima uwajibishwe.

Hata hivyo kwenye mipaka ya kimahusiano kuna kukaimishana, kukodishana wajibu na majukumu kwa muda ili kufanya mambo yaende. Kwa mfano, baba anaouwezo wa kumruhusu mama/mkewe aingie katika mpaka wake(afanye baadhi ya wajibu au majukumu yake, ya baba) kwa muda fulani ikiwa baba anamajukumu mengi mengine.

Au mama akamruhusu mume wake aingilie baadhi ya mipaka yake kwa muda kwa mustakabali mzuri wa mipango ya familia. Hiyo inaruhusiwa kwa sababu ni makubaliano, siyo dhulma.

Ni kama nchi moja kuomba msaada kutoka kwa nchi nyingine. Mfano Msumbiji imeomba msaada wa Jeshi la Rwanda kusaidia kupambana na magaidi. Au Ukraine imeomba msaada wa kijeshi kwa mataifa ya Ulaya kupambana na uvamizi wa Urusi.

Kisheria hairuhusiwi jeshi la nchi moja kufanya kazi katika nchi nyingine. Yaani Jeshi la Kenya lifanye kazi Tanzania. Huko ni kuvuka mipaka. Ila Tanzania inayoruhusa kuomba msaada wa kijeshi kwa nchi nyingine. Na hiyo ni kwa muda Fulani. Hiyo ni mipaka ya mahusiano ya nchi na nchi.

Ndivyo ilivyo hata katika mipaka ya mahusiano ndani ya ndoa. Baba anauwezo WA kuomba msaada Kwa mkewe, na isionekane kuwa Mke kavunja au kuondoa mpaka wa mumewe. Jambo ambalo litaitwa uhaini au uvunjifu wa Amani.

ii. Mpaka wa mzazi na mtoto
Mzazi anaukomo wa mamlaka yake kwa watoto aliowazaa. Mtoto akishafikisha umri wa kujitegemea, akajitegemea na kuanzisha maisha yake, mzazi hana mamlaka yoyote ya kumuingilia mtoto wake kivyovyote.

Tayari mtoto huyo ni taifa huru, anatakiwa kuendesha maisha na familia yake atakavyo, siyo utakavyo wewe, mzazi. Ukifika nyumbani kwa mtoto wako, wewe unabaki kama mgeni tuu usiye na amri wala mamlaka yoyote ndani ya nyumba ya mtoto wako.

Utafuata amri, sheria na taratibu za nyumba ya mtoto wako, akiwemo mkwe wako. Masuala ya kusema nimekuzaa, sijui nilikuweka tumboni, hapo hayana maana yoyote.

Mzazi utabaki kama mshauri tuu. Kuingilia mambo ya nyumba ya mtoto wako ni kuondoa mpaka wa jirani yako, hilo ni kosa siyo tu kidini bali pia hata nature haitaruhusu jambo hilo kutokea. Na itakuadhibu vyema.

Mzazi yeyote anayeleta chokochoko na kuingilia sovereignty power ya serikali ya mtoto wako unajitengenezea bomu baya hapo baadaye. Ukitaka watoto wako wakupende, basi heshimu mipaka ya mahusiano yenu. Bali kuwa mzazi na yeye abaki kuwa mtoto, wewe endelea kumshauri na siyo kila mara. Kukushauri mtu mzima jambo lilelile ni kumshinikiza. Ni kuingilia mamlaka yake.

iii. Mpaka wa Mungu na Mwanadamu
Ni kosa kisheria kuondoa mpaka wa Mungu wako kwako. Upo wajibu na majukumu ya Mungu aliyekuumba kwako, na wewe unaowajibu na majukumu uliyopewa kwa Mungu wako. Ni kosa kubwa kuingilia au kuondoa mipaka hiyo.

Mungu kuna mambo hawezi kukuingilia kamwe, anajua unauhuru kwa baadhi ya mambo, lakini hata yeye anauhuru na hataki kuingiliwa anapofanya wajibu na majukumu yake. Ni vyema kujifunza kujua wajibu na majukumu yako kwa Mungu. Kujua wajibu na majukumu ya Mungu kwako.

Ni kosa kisheria za asili kuabudu miungu migeni ilhali Mungu wako aliyekuumba yupo. Kama unavyojihisi maumivu mkeo akichakatwa na kubinuliwa binuliwa na mhuni ndivyo Mungu wako anavyojihisi wivu. Kama unavyojisikia mumeo akilala na wanawake wengine ndivyo Mungu anavyojisikia. Unajua matokeo ya wivu wa mapenzi yalivyo?

Moja ya jukumu na wajibu wa Mungu ni kukusaidia wewe kiumbe wake. Lakini nawe unaowajibu wa kumuabudu.
Kwa nini uende kwa waganga kuomba msaada ilhali Mungu wako yupo?

Embu fikiria umezaa mtoto Aldi mtoto huyo anaenda kwa majirani kuombaomba hovyo, unajisikiaje? Bila Shaka unahisi kudhalilishwa, kuabishiwa. Ndivyo ilivyo kwa Mungu aliyekuumba.

Soma
2 Wafalme 1:16
[16]Akamwambia, Bwana asema hivi, kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, Mungu wa Ekroni, je, ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.

Abudu kwa Mungu aliyekuumba, maisha yasikufanye uvuke mipaka. Ni sawa na kijana anayetafuta maisha akaacha kufanya shughuli halali halafu anafanya shughuli haramu kwa kisingizio cha kutafuta maisha na kupata Pesa. Hilo ni kosa kisheria.

3. Mipaka ya Kisaikolojia
Hii ni mipaka inayohusu akili na tabia za viumbe hasahasa binadamu. Ipo akili na tabia ya kike na ya kiume.
Ipo akili na tabia ya kitoto na mtu mzima au mzee. Kila mtu hapaswi kuondoa mpaka wake au mpaka wa mwenzake.

Mtoto anayohaki ya kufikiri na kutenda kama mtoto. Ila hapaswi kutenda mambo yawapasayo watu wazima. Mfano mtoto mdogo hapaswi kujiingiza kwenye masuala ya mapenzi kwani mapenzi yanawahusu watu wazima wenye akili iliyokomaa na wenye uwezo wa kukabiliana na matokeo na hekaheka za mapenzi.

Ni kosa kisheria hasa sheria za asili mtoto kutenda mambo ya kikubwa. Mfano mtoto akijiingiza kwenye mapenzi halafu akapata mimba, ni wazi mtoto atakayemzaa hataweza kumhudumia. Na hii itaathiri mwenendo mzima wa maisha yake na wale wanaomzunguka.

Pia mtu mzima hapaswi kutenda au kufikiri kama mtoto mdogo. Hii itaathiri maamuzi na utendaji wake katika majukumu yake kama mtu mzima. Mfano, mwanaume mwenye akili za kitoto huweza athiri familia yake kwa sababu watoto akili zao mara nyingi ni ndogo, fupi, zinafanya jambo pasipo kuangalia matokeo.

Siyo ajabu kijana mwenye akili ya kitoto anaweza kuendesha gari kwa kasi bila kufikiri kuwa ajali mbaya inaweza kutokea halafu naye anafamilia inayomtegemea, yaani ni kama mtoto mdogo asiye na maarifa makubwa. Huko ni kuondoa mpaka wa akili na tabia yako, ni kosa kisheria.

Mwanaume lazima ubaki katika mipaka yako. Fikiri kama mwanaume, kuwa na tabia za mwanaume. Siyo unafikiri na kutenda mambo kama jike. Hilo ni kosa kisheria za asili, na huo huitwa ushoga. Kuwa Mwanaume, kwa wasiyojua maana ya mwanaume ni kuwa na nguvu usiwe legelege kama demu. Hapo unaingilia haki za wanawake.

Wanawake ndiyo wanahaki zote kuwa legelege, lainilaini, warembo, wazuri, wapole, watamu n.k. Sasa mwanaume mzima unataka kulelewa kama mwanamke, huko ni kuvunja sheria za asili na lazima ulipie. Lazima mkeo na watoto wakudharau.

Kuna vijana wasiyo na akili wanasema wanawake wakipata vipato wanakuwa na jeuri. Mwanamke kiasili humdharau mwanaume asiye mwanaume bila kujali unahela au hauna. Kama haujielewi wanawake hawanaga simile, hawanaga kupindisha mambo, watakudharau tuu. Kiufupi wanawake hawanaga kitu inaitwa uvumilivu. Ukiona mwanamke anakuvumilia ujue bado anaona unauanaume ndani yako.

Wanawake hudharauliana, hivyo ukiona mwanamke wako anakudharau ujue anakuona kama mwanamke mwenzake. Unaingilia mipaka yao unataka wakufanyaje, wakuchekee, lazima wakuchukie, wakudharau na watafute namna ya kukukomesha.

Kama sisi wanaume tunavyowachukulia wanawake wanaojifanya wanaume, ndivyo pia wanawake wanavyotuchukulia wanaume tunapovuka mipaka yetu kiutendaji na kitabia na kufanya kama wao.

Kiasili mwanamke hamshindi akili mwanaume. Hilo hata wao wanalijua. Hivyo mwanamke akiona anakuzidi akili moja kwa moja anakutoa kwenye ile listi ya wanaume anakuweka kwenye kundi la wanawake wenzake.

Mwanamke siku zote huishi kwa furaha na mwanaume kamili. Aliyemzidi maarifa, akili, uwezo wa kujitawala kihisia, kiakili, kiroho na kimwili.

Kusema mwanamke anamzidi mwanaume akili ni ujanja wa kuwasifia na kuwapaka mafuta wanawake kwa mbongo wa chupa. Ila ukweli ni kuwa wao wenyewe wanajua uwezo wao wa akili ni mdogo ukilinganisha na wanaume.

Sasa kama huna akili za kutosha kumzidi mwanamke utaweza kweli kumtawala? Kumbuka wanawake wanapenda kutawaliwa haswa.

4. Mipaka ya Kimaumbile

Hii tutaendelea wakati ujao.

Pole na hongera kwa andiko refu. Bila shaka umepata mawili matatu.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom