Usiombee kukosa hela

Hela mbaya sana kuna mzee mmoja alimtia kibendi demu nilitaka kuoa. Ikabidi nibadili gia angani nikaoa mwingine chap.Yule mzee hamuhudumii kabisa yule demu na mwanae.Kuna mizee yenye hela ina waharibia vijana.
 
Mwanaume unashindwa kukaa na njaa siku moja,aiseeeee
 
Ss hata kufunga hii ramadhan utaweza kweli?
 
Hizi ndio style ambazo sitakagi,ndio maana kama sinaga kitu najiambiaga kabisa moyo tulia,nakua nipo busy na mambo yangu
 
Hahahaha kwahiyo ungemuelewa saiv ungekuwa muke yake dciiiiii
hatuwezi kuwakubalia wote isitoshe wanawake tunaangukiaga kwa watu wenye speed ya kufukuzia walio slow huwa tunahisi wanajaribu au wanna kambi nyingi
Na hapo ndipo mnapo lose point
 
Kuna mtu nimemtumia amenijibu hela ndogo hata asante sijapata, japo sisaidii kupata shukrani, bora ningekupa mwenye uhitaji ningepata baraka
Humu wapo watu wa kila aina mkuu
,so hata huyu ungeweza kumtumia na akakutusi tuuu
 
hongera mkuu, sisi bado tunapambana hata nauli ya kutoka Moro hadi dar nichangamoto ila tunakomaa, ni dhambi kukata tamaa

Kaka acha tu. Kwenye maisha kila mtu ana yake Moyoni aliyopitia. Nimepitia Magumu. Nishatokaga Kariakoo mpaka Kinondoni A kwa Miguu. Kariakoo nilifuata Mchongo wa kazi lakini sikumkuta alieniahidi. Nikaunga Kinondoni nako nikapewa Kisomo tu.
Nikarudi home Magomeni nipo hoi.
Niliacha Vitumbua Geto nikachemsha Chai na Vitumbua nikanywa nikalala.
Kuna muda huwa nikimfikiria Mungu we acha tu. Nipo First World, eti na mimi sasa hivi nikija Africa Nadinya wanawake wenye hadhi zao, wenye kazi nzuri, wenye kipato, Dah!! Maisha yana siri nyingi sana Kwa sisi Maskini.
Yote Kwa yote kwenye maisha ni marufuku kukata tamaa.
 
Maisha haya jamani, enzi hizo kuna siku nimeamka nina buku 3 tu halafu naona kila kitu kimeisha ndani. Kichwa kinawaka moto kwamba hiyo buku 3 naibajeti vipi inisogeze sogeze. Natoka home nakutana na mama ananililia shida yuko na katoto kadogo hawajala kitu tangu jana yake. Ikabidi tu nimpe ile buku3 nipambane na hali yangu. Kama bahati jioni inaingia msg ya mpesa ndio ikawa afadhali yangu.
 
-unahamisha madeni unakopa ili ukalipe pengine
-Yani wewe kwenye maisha yako ukishika tu hela basi kama hutaumwa kuna jambo lingine la kuifanya ile hela isikae ilimradi tu ukae mtupu uishi kwa majuto saa zote.
-Kuna kipindi unajiuliza hivi Mungu yupo ama kaenda likizo? kama yupo likizo basi aanze kazi leo
 
Bora ukose hata tshs ila uwe na mwenza aka mke understanding... ila kama ni kisirani akijua huna ndio anakuja na list ya vitu ... mara maji ya kunywa yameisha, mara gesi inakaribia kuisha, mara watoto wanatumwa kwenda kuangalia units za umeme zimebakia ngapi , ... hatari tupu
 
Maisha yana changamoto nyingi ila bado tunapambana nashukuru Mungu umri bado unaruhusu nitajitahidi nikimbane na muda
 
kuna ule usemi unasema "moyo kichaka" kuna siku nilimuambia jamaa yangu mmoja hivi ukiona siku nimekufa halafu kifo changu cha mashaka msijali wala msiogope maana nina mengi moyoni...
 
Yaani wewe unaongea lugha tunayoongea wengi, sis kina mama tunapitia kipindi kigumu sana.

Wanaume mnaondoka sis na watoto wanaojua chakula lazima kiwepo.....

Wakati mwingine najiona kwa nn maisha yanakuwa hata siendani na hali hii?? Na kusoma kwangu, shahada za juu kuweka akiba naidokoa, siku kahela ukikapata hata mil2 ndg akipata shida Roho inanituma nitoe. Natoa

Nilikosaga 100 ndani na watoto mume wkt huo nae hana kitu. Natafuta nyumba nzima wkt mwingine napata pesa zilizosahaulika, na pale ninapotupiatupia miamia napo hakuna, nakwenda dukani mangi naye, anaonekana kunichoka...natembea nikitamani kuokota hata elfu 10.

bodaboda ya mradi nayoe analia biashara ngumu wateja hakuna, bajaji inadai natengenezo....

Biashara hazikipi ni maisha maisha hayaeleweki je huu ndio uchumi wa kati kweli au unetukamata
 
Hela mbaya sana kuna mzee mmoja alimtia kibendi demu nilitaka kuoa. Ikabidi nibadili gia angani nikaoa mwingine chap.Yule mzee hamuhudumii kabisa yule demu na mwanae.Kuna mizee yenye hela ina waharibia vijana.
Hivo vizee vipo na mara nyingi kwao kuhonga laki 2/3 au kodi ya nyumba sio issue sasa wewe mtoto akikwambia nina birthday kesho unatoa elfu 10 tena kwa mawazo sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…