Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Kwanza nikupe pole kwa mtihani uliokumbana nao, nina hakika yataisha na maisha yataendelea kama kawaida, hakuna changamoto isiyokuwa na ufumbuzi, na natumaini kwamba hili litakapokwisha nawe utakuwa umejifunza kitu. Kama hujajifunza ni kwamba USIFANYE NGONO NA MWANAMKE BILA KUTUMIA KINGA HASA KAMA BADO HUNA HAKIKA KAMA MAHUSIANO YENU NI YA DHATI. Ukiendelea kufanya ngono bila kinga maana yake utaendelea kuzaa watoto bila mpangilio lakini utakuwa unawakwanza wanawake hao unaokutana nao, licha ya hatari unayojitengenezea ya kupata magonjwa.
 
Wewe ulimsaliti sasa yeye kukusaliti hasira unaitoa wap kiongozi, ndege wafananao huruka pamoja
 
Duuu...we jamaa una gundu!

But aliyekutuma kushika simu ya mkeo huyo tena usiyempenda ni nani? Sasa ulitarajia akae tu bila kuwa na mtu? Mbona we una mwanamke tena ana mimba ako???

Wee una majanga tayari bado unaongezea mengine! Utakuja kujiua ww wee endekeza wanawake na mambo yao
 
Witnessj ndugu yangu,bora ningeona ana-date na mtu mmoja,ningejua ndo ukame wakati mimi sipo,sasa wanaume 4 na bado unamtetea,eboooo!!!
 
Aisee somo la leo wanaume tuache kuchovya chovya ovyo raha ya siku moja inaweza leta shida ya mwaka mzima
 
Ni kweli,nauchukua ushauri wako,japo nikianzisha mahusiano yakikaa kuanzia miezi 3,matumizi ya kondom kwa kweli yanapungua automatically!!!

Ila kwa hali hii nadhani nitajitahidi sana kuji-control,awali nilikuwa naamini mwanamke hawezi kushika mimba tu pasipo makubaliano,hasa watu wazima na wasomi!

Sasa msomi mzima anajishikia tu mimba pasipo kukubaliana,sio sawa kabisa!
 
Ujanja uliuanza wewe sasa unalia lia
Ushauri muombe msamaha mke wako uanza maisha mapya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…