Usiombe yakukute jamani, daah!!!

Ni kweli ni mzazi mwenzangu,na nampenda japo anajenga mazingira ya mimi kuipoteza familia yangu,kwa maana nyingine nyingine nisiende kuqatembelea familia yangu!!!(hapo ndo kitendawili,nawezaje kutelekeza familia yangu!!?)
Yaani na wewe unataka kabisa kuingia kwenye mtego wa hivyo wa kuiacha familia yako kizembe namna hiyo acha masihara basi kuwa greatman kweli Fanya maamuzi kwa ajili ya future ya yule unaetambua maisha yake, unatambulika kwao, wanamtambua kwenu

Kofia uliyo vaa ya u-greatman inaanza kupwaya kama utaendelea na maamuzi dhaifu kwenye issue serious ya maisha yako
 
Kitu ambacho ni maajabu kw wanaume wengi " ile ni familia yangu kiukweli ila mwanamke yule simpendi sina hisia naye kali" unawezaje kufanya kwarudiarudia na mtu usompenda kisha kumuoa kabisa?
 
Usijutie sana kilichotokea na maamuzi yako, nachokushauri kama wewe ni mtumishi hama huko Tanga, mwachie vitu vya ndani ya nyumba/Chumba chako. Kaishi na Mkeo wa Singida, yule wa Tanga akigundua hivyo hapo baadaye hatoweza kukusumbua maana alifanya anachokijua wakati wanawake huwa wanawaza matukio ya mbali sana
 
Sasa anajichinja mkono, si angechinja koromelo kabisa kama anataka kufa kweli?

Ila wanawake bana tuna taabu sana, yaani akaona ajibebee mimba na yeye ili akumiliki mazima!! Hapo anajua ukimuacha wewe kuja kupata mwanaume wa kumuoa ni majaaliwa maana hiyo idadi ya watoto tu haitamwacha mwanaume salama atakimbia tu
 
Natamani kuwa mwenyewe kabisaaa!!!
Naomba nipe shule hiyo ndugu yangu,niepukane na haya majanga!
Naogopa zaidi kesho yangu kuliko niliyoyashuhudia!
 
Ahsante mkuu,ila ni fundisho kubwa sana kwetu wanaume,bora angekuwa si mfanyakazi mwenzangu,lakini kwa hali ilivyo ni janga,kila siku ofisini tunakutana na wakati mwingine tunapangiwa majukumu ya pamoja!
 
Mkuu naogopa sana VVU,ndiyo maana nakuwa na vipimo vya kutosha,kabla sijaingia kwenye mahusiano ni lazima nicheck kwanza afya ya mhusika,lakini kwa hili nimekwama kabisa!
 
Kitu ambacho ni maajabu kw wanaume wengi " ile ni familia yangu kiukweli ila mwanamke yule simpendi sina hisia naye kali" unawezaje kufanya kwarudiarudia na mtu usompenda kisha kumuoa kabisa?
UKiwa na uwezo mdogo wa kuchanganua mambo. ... Utashangaa hilo ..ila kwa wenye akili ........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…