Usiogope wanavyomshangilia

Sema basi kuwa hata wewe ulikuwa huko wakati huo! Kisha ushuhudie humu ulichokiona au kujifunza kwenye utawala ule. Onyo:- usiwe biased tafadhali!
Kuwa biased ndio nini. Unataka niongee kama mabavicha yanavyoongopa ndio uridhike?
 
Unajuaje kama hakuwa akila nyama za watu? Wewe unajua kuwa kama dude lile lazima uwe shirikina? Unajua mipaka ya ushirikina? Ongea na Mayunga (marehemu), "Mti Mkavu", aku narratie maisha halisi ya Idi amini tangu wakiwa wote jeshini!
Hakuna kitu kama hicho ndugu, Major General Mayunga au Kamanda Mti Mkavu ambaye alikua jemedari hasa wa vita na ninamuheshimu sana aliwahi kumuelezea huyu mtu sababu walisoma wote kwenye chuo cha jeshi Kenya. Kubwa alilosema ni kwamba Amin alikua mtu matata na akipenda sana presence yake iwe noticed popote atakapokua, na atafanya hivo kwa kufanya vitu vya kibabe(aliwahi kua bondia). Mambo mengine kama ukatili na kuua sikatai kua alifanya kama ambavyo viongozi/watawala wengi tu wa Afrika walifanya kwa maadui zao kisiasa kwa wazi au kimyakimya.
Kama ambavyo na wewe huwezi kunithibitishia kama alikua anakula nyama za watu na mimi siwezi kukuthibitishia kinyume chake. Kwamba General Mayunga RIP aliwahi kusema hivo ni propaganda tu za vita, vinginevyo tuamini pia eti wakati flani alikua akibadilika na kua joka kubwa, maana na hilo nalo tuliambiwa!
Idd Amin alikua ni dictator, mtawala katili na mwenye vituko lakini kuna mengine meengi alizushiwa kama mbinu na hamasa za kivita. Uliza kwa Waganda walio iishi historia yake na wasio biased wakueleze
 
Sivibaya ukayataja japo kwa uchache hayo mazuri na Mabaya....halafu haimaanishi Dikteta... atakuwa anakula
peke yake wapo vibaraka nk unataka kuniambia hata watoto wake watachukuia utawala wake?...kuwa kiongozi ww ni wawote Sasa Angalia kwa mfano hapa kwetu Mtu kama dab ataanzaje kumlaumu mtukufu! lkn wapo watu Wengi wanalia juu ya utawala huu Kwahiyo kwa IDD AMINI pamoja na Mabaya mengi aliyowatendea watu wake kuna watu pia
walinufuika nae Lazima wamtukuze!
 
Kuwepo na waganda walioshika Historia ya Mazuri Idd Amini haimaanishi hakuwa mtu wa hovyo!
Maana walinufaika nae...mfano mzuri ni huyu wahapa na DAB unataka kuniambia mtu Kama hugo atasemaje!
 
Mkuu hiyo ni kawaida sana, hakuna binadamu anayeweza kuwa mbaya kwa watu wote. Wale waliokuwa wananufaika na uwepo wake wanawezaje kumchukia? Shatani pia ana wafuasi wake tena wengi tu!!
 
Raisi mstaafu wa Afrika ya Kusini aliwaji kusema"Matatizo mengi ya Afrika na Waafrika yanatokana na umasikini wa kujiletea au kuletewa na viongozi ili tutawalike watakavyo". Kiongozi anaingia madarakani leo na anaanza kuwaambia mkae kimya yeye anafahamu yote mnayotaka! Bado kwa kauli hiyo hamjashtuka tu? Yaani kila kitu mfanyiwr,hata mahesabu msiulize. Duu,kweli Thabo Mbeki aliona mbali
 
well said
 
kama ulivyo vile...

sometimes fanya busara pita tu! hakuna aliyekuomba usome
Lissu alivyoiita kamati ya rais Magufuli kuhusu madini rubbish, mlishangilia na kupiga vigeregere.
This report to me is a rubbish!, over!
 
1. Serikali hii ya JK Ni dhaifu, nchi inahitaji Raisi dikteta ili isonge mbele - Mnyika

2. Nchi inahitaji Raisi anayeweza kufanya maamuzi magumu bila woga- Mbowe

3. Tunamuhitaji rais mwenye uwezo wa kukemea wasaidizi wake Na wakamtii- Lema


Sasa mnalalamika nini??
 
Unajua hata kuua ni maamuzi?
 
Mkuu hiyo ni kawaida sana, hakuna binadamu anayeweza kuwa mbaya kwa watu wote. Wale waliokuwa wananufaika na uwepo wake wanawezaje kumchukia? Shatani pia ana wafuasi wake tena wengi tu!!
Nakubaliana na mengi yanayosemwa. Ni kweli Amin hakua kiongozi mzuri na alikua ni dictator mbaya(kama kuna dictator nzuri). Makosa mengine ya kiuchumi inaweza kua ni sabotage kutoka nje kama anavofanyiwa Mugabe au pia poor governance kutokana na Sera mbovu kama ambavyo inaweza kutokea kwa kiongozi wa 'kidemokrasia'. Na namba ya watu(waganda) wanaomkumbuka kwa mazuri sio ndogo kusema you can neglect. Ukweli ni kwamba kuna mazuri ya ndani ya nchi yake aliyafanya mambo ambayo mimi Mtanzania hayanihusu. Na pia exaggerations za kula nyama za watu ni unfounded
 

Hukuwahi kuongea na Mayunga privately. Yeye mwenyewe alikuwa mtata pamoja na kwamba alikuwa kamanda wangu mzuri sana kwenye uhamasishaji. Na hili nakubaliana na wewe kwamba wakati wa vita kama vile wakati mwingine wowote wa shughuli ngumu, kuna slogans lazima zitumike katika kufairji na kutia hamasa. Joka kuu is something else kama nduli etc zenye lengo la kutukana kwa lengo lakuondoa nyongo chungu mioyoni mwa watu.

Lakini, ulishawahi kusikia kuna watu wanakula nyama za binadamu katika ulimwengu huu huu, tabia ambayo si ya kawaida lakini inafanyika kutokaa na vichocheo vya nguvu?

Vitani yanatokea mengi, sitaki kuyasema kwanza ni muda mrefu. Unaweze kuamini kuna mahala watu wanamkamata mateka wanawambia akate nyama yake kutoka paja lake mwenyewe atengeneze nyama choma yake mwenyewe?

Watu wana hulka nyingi. Huwezi kukataa tu kwa sababu unakataa pale mtu katili anaposemekana kufanay ukatili usiouwazia wewe? Unaweza kukanusha kwamba kwenye jokofu la idi amini kulikuwa vichwa vya binadamu? Tabia hii haifanywi na mtu wa kawaida. Na kama anaweza kufnya hili, bila shaka anauwezo usiompaka wa kufanya ushetani mwingie wowote. Sikuwepo akila nyama za watu lakini mazingira yanatengeneza mwelekeo chanya kwenye hizi allegations. Or else wewe ulikuwa miongoni mwa kikosi chamauaji cha huyu jamaa ambaye unajua alikuwa akifanya nini na miili ya watu wale walikuwa wakipotea mysteriously. La sivyo huwezi kukanusha kwa kuwa hujui.
 
Unajuaje kama hakuwa akila nyama za watu? Wewe unajua kuwa kama dude lile lazima uwe shirikina? Unajua mipaka ya ushirikina? Ongea na Mayunga (marehemu), "Mti Mkavu", aku narratie maisha halisi ya Idi amini tangu wakiwa wote jeshini!
Wanaokula nyama za watu wapo na hasa baadhi ya mkoa wa kagera na uganda (wachawi)
 
wewe bwana mwongo nchi za magharibi hazikumchukia Amin mana zilimwona ndiye haswaa angeweza kupambana na Nyerere mcomunisti na ndo maana Uingereza ilimsaidia pia wakati wa vita ya Kagera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…