kila mtanzania anaweza kujenga nyumba ya kuishi mwenyewe iwapo kama una nia yakufanya hivyo. Nunua kitu kimoja kimoja pindi unapopata hela kidogo. kuna watu wanapanga nyumba kwa mamilion ya shilingi kwa kuwa nyumba hiyo ina hadhi anayoipenda. na wala atarajii kuhama mji huo. wakati hela hiyo angeweza kununulia eneo, na baadae kupata ushauri wa wataalam. na baada ya miaka michache sana utakuwa na nyumba nzuri 'yako' Yenye thamani kubwa, ambayo husingelipata hela hiyo 'in cash' think about it.
Hasante kwa hushauli
Nafikiri kiswahili fahasa ni :Usiogope na si Husiogope
Hivi kaka msingi wa ile kitu nliyoku-PM last time inaweza kwenda kwa ngapi?
Sioni kama kuna kosa kutumia mamilioni ya shilingi kupanga nyumba yenye hadhi anayopenda mtu...na unaposema kuwa atumie hayo mamilioni ya kodiya nyumba kununua eneo, in the mean time akijenga/akisubiri kujenga alale porini?
Ugumu wa waTanzania kuwa na nyumba inatokana na kutokuwa na mfumo wa mortgage utakaokuwezesha kuwa na nyumba ukahamia huku ukilipa taratibu kwa muda mrefeu, kama ambavyo ungesave na kujenga! Hata nchi zilizoendelea hawadundulizi ili kujenga nyumba....wana mortgage au kwa wenye hela wananunua nyumba kabisa.
Wakati unajenga lazima maisha yaendelee, na hili linajumuisha kuishi mahali/kwenye nyumba nzuri kwa afya na usalama wako na pia familia yako...sioni kosa kupanga nyumba nzuri kwa ghara kubwa lakini unaafford!
umenena mkuu, big up!Hii post yako ina ushauri usiho sahihi hata kidogo.
Kwa vile inaweza kumshawishi mtu mwenye mawazo mazuri akapotea, nitachangia kidogo.
Unapoput blame on mortgage system unakuwa umesahau kuwa jukumu la kila mmoja wetu ni kutafuta njia za kusurvive katika environment yake. Huwezi kuishi Tanzania kwa kutegemea system ya Marekani, hivyo basi kama uko Bongo unapaswa kujifunza kujenga kutokana na uhalisia. Mortgage system siyo kama haipo Tanzania, ipo ila coverage yake ni ndogo.
Yule anayeamini kuwa maisha "lazima yaendelee" anajidanganya kuwa yule anayesave kwa kujenga maisha yake yamesimama, la hasha. Check him/her out after 4-5 years he will be happier and more secure than yule anayepanga.
Unaposema ni sahihi mtu kutumia pesa yake yote kulipia nyumba huku akilaumu mfumo wa mortgage wa Tanzania, kumbuka kuwa Tanzania pia haina mfumo mzuri wa pension ambao unawahakikishia wananchi makazi na services nyingine mara wanapostaafu au kushindwa kufanya kazi kwa sababu nyingine. Hapo jiulize, security ya huyu aliyekuwa anakodi nyumba ya gharama kubwa inatoka wapi akistaafu au kupata disability?
Hivyo basi, ushauri sahihi kwa watanzania ni kwamba iwapo kipato chako kinaruhusu saving basi fanya hivyo kwa malengo ya kujenga nyumba ASAP. Ukishakuwa na mahali pa kuishi, it is easier kudeal na changamoto nyingine za chakula, ada, matibabu n.k