Usioe wala kuolewa kama wewe ni muhuni

Usioe wala kuolewa kama wewe ni muhuni

Wanawake wamefanya wanaume wakatae ndoa
Wahuni ndio wanafanya watu waogope kuingia kwenye NDOA Mkuu.

Kuna wahuni wanawake na wahuni wanaume, wote hawafai kuwa kwenye NDOA.
 
Ndoa sio upendo ila ni kuheshimiana na kuiheshimu ndoa.

Naongea na wanaume wenzangu pamoja na wanawake, kama wewe unahisi huwezi kuiheshimu ndoa basi nakushauri endelea na uhuni wako tu.

Usiolewe wala kuoa kwasababu ya kupewa tendo, pesa n.k bali owa/kuolewa kwasababu ya Mungu wako unaemuamini. Mambo ya kihuni hayapaswi kuletwa kwenye ndoa kwani mnawatisha vijana wadogo mpka wanafikia hatua ya kusema Kataa Ndoa.

Kwa nchi za waislamu ukizini nje ya ndoa kuna hukumu yake nzito, ndio maana ni nadra kuona nchi za Kiislamu/Waarabu watu wakizini nje ya ndoa.

Natamani kungekuwa na hukumu kubwa kwa wahuni/malaya wote wanaoichezea sekta muhimu ya ndoa.

Usichezee Ndoa.

Ndoa ni Taasisi Muhimu.
Mm ndio maana nataka kuoa uarabuni jpo Dini yng mkristo [emoji41]
 
Mm ndio maana nataka kuoa uarabuni jpo Dini yng mkristo [emoji41]
Hilo ni jambo jema Mkuu, ni bora ukaoe sehemu yenye Msingi mzuri wa Ndoa kuliko kuoa sehemu ambayo zinaa sio kosa kufanya.
 
Wanawake sizani kama wataweza kwani wanapenda sana wahuni.
 
Kama unapenda wanaume wahuni, basi ukichitiwa au kuletewa watoto wa nje usilalamike.

Kaa mkimya na Muhuni wako
Kawaida sana,haya mapenz utaweka misimamo yako weee,lakini kama ni wa kuangukia pua utaangukia tu mkuu
 
Back
Top Bottom