Usioe Mwanamke asiyekupenda

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
865
1,204
Jana nilikutana na fundisho kubwa sana kwenye maisha yangu baada ya kukutana na mzee wa bodaboda aliyenipa ushauri mzito utasema alitumwa na Mungu juu yangu.

Mwakyoma: Mzee umemuona yule dada aliye nisindikiza vizuri

Mzee wa boda: Ndio nimemuona , vipi ndio mkeo

Mwakyoma: Hapana , ni mtoto wa mwenye nyumba hapo nilipopanga , kiukweli ni mwanamke mwenye kila kitu chema ila najiuliza sana kivipi huyo mwanaume wake aliamua kumuacha na kumsusa mtoto wao

Mzee wa boda: Ha ha ha, wewe ina maana hujui mpaka leo siri ya ndoa

Mwakyoma: Inawezekana sijui

Mzee wa boda : Mwanamke anaweza kua na tabia zote nzuri na utu kwa asilimia mia, wewe ukatokea kumpenda sana ila kumbuka na yeye anahisia kama wewe za kumpenda mtu ukitoa tabia zote nzuri unamuona nazo

Mwakyoma : Mmmmh , sijaelewa vizuri hapo

Mzee wa boda: Mwanamke anaweza akampenda mwanaume kwa roho yake yote, na wakati huo anajua kabisa huyo mwanaume kamwe hawezi kumfanya yeye kuwa mke wake wala kufanya maisha pamoja nae lakini bado akampenda hivyo hivyo.

Mwakyoma: Sasa kwa nini wanafanya hivyo

Mzee wa boda: Kwasababu hayo ndio mapenzi , kumpenda mtu bila sababu yoyote yani unajikuta unampenda tu lakini hayo yote hubadilika pindi anapotokea mtu kama wewe ambae anavutiwa na tabia za binti na kutangaza ndoa

Mwakyoma: Kwaio wanao tangazaga ndoa wengi wao wanakosea

Mzee wa boda: Ndio , wengi wao wanakosea hata mimi nilikosea angalia vidole vyangu siunaona nimevaa pete kidole cha kati hiyo ni pete ya ndoa ambayo imenifanya mpaka leo nimekua dereva bodaboda na umri wangu huu

Mwakyoma: Mzee pole sana nini kilitokea

Mzee wa boda: Nilikua kijana wa rika lako kipindi hicho nina mali za urithi na biashara zikienda poa huko mkoani , nikavutiwa na mwanamke mwenye tabia nzuri kama hizi ulizolua unasifia yule dada niliekukuta nae, nikamueleza lengo langu la kutaka kumuoa na akaniambia nisubilie jibu baada ya kama mwezi alikuja kukubali na nikamuoa

Mwakyoma: Aise! Mzee ulipenda

Mzee wa boda: Ndio nilipenda sana , mwanzoni tuliishi vizuri sana , yeye akiwa mwajiliwa wa serikali mimi nikiwa na biashara zangu mengine nimazito nikikuelezea mwanangu lakini nilishindwa kuvumilia niliyokua nafanyiwa siku moja nikaamua kukaa pembeni naapa !! Siku chukua mwezi maduka yangu ya kumla na store ziliwaka moto mala magari ya nock engine nk

Mwakyoma: duuuu! Sasa nani alikua anafanya hivyo

Mzee wa boda: Hahahaha , ni yeye mwanangu mwanamke asiyekupenda ni sumu hata kama anatabia nzuri hizo tabia ni kwajili ya watu wote lakini mapenzi ni kwa mtu special ampendae kama wewe si huyo ampendae ni bora utulie tu kamwe hutamuona mbaya.

Mwakyoma: Kwaio inawezekana huko kwa mwanaume wake alizingua ndio maana karudi pale kwao na mwanake

Mzee wa boda: Haha siwezi jua lakini nakwambia hili asikudanganye mtu kama unataka kuona dunia nzuri oa mwanamke anaekupenda na usiniulize utajuaje kama anakupenda , mwanamke anayekupenda hato tafuta kigezo cha kukupenda ni atakupenda tu!! Uwe na ulemavu ,mfupi, kichaaa, masikini choka, tajiri ,uwe na elimu uwe hauna yani hakuna kigezo atakiangalia ili akupende kila siku atakua anakuona mpya mala zote

Mwakyoma : Mzee nashuka hapo kwenye kibanda daaa! Asante kwa kuniosha macho mkuu

Mzee wa boda: Usiwaze sana ,ila maneno yangu yakumbuke sana maana huwa mimi sio muongeaji sana ila leo sijui nini Mungu kanipa nikwambie.

Wakuu naomba kuwasilisha 🙏🏿
 
Mnh! Moyo umebeba mengi, utajuaje kama anakupenda weng wao wanajua kuigiza s haba 😊.

Muhimu n kumuomba Mungu(Allah) kwa imani yako akupe unayestahili, kwa macho ya kawaida huweza tambua. Utasema kwa vtendo wengne n mabngwa wa kuigza looh!

Ingawa sjasoma, nmeona n ndefu 🤪🤪
 
Mnh! Moyo umebeba mengi, utajuaje kama anakupenda weng wao wanajua kuigiza s haba 😊.

Muhimu n kumuomba Mungu(Allah) kwa imani yako akupe unayestahili, kwa macho ya kawaida huweza tambua. Utasema kwa vtendo wengne n mabngwa wa kuigza looh!

Ingawa sjasoma, nmeona n ndefu 🤪🤪
Mwanamke anayekupenda hatumiagi akili yake hata kwa 1% anaitegemea yako by 100% vile uonavyo sahihi na kwake ni sahihi pia. Anausikiliza moyo wake kuliko chochote.

Ukiona mwanamke anaweka criteria's tu mbele yako ama conditions flani ziwe met ndio akupende jua sio wako huyo! Utatumia nguvu kumshawishi ila ataishia kukutumia tu.
 
Mwanamke anayekupenda hatumiagi akili yake hata kwa 1% anaitegemea yako by 100% vile uonavyo sahihi na kwake ni sahihi pia. Anausikiliza moyo wake kuliko chochote.

Ukiona mwanamke anaweka criteria's tu mbele yako ama conditions flani ziwe met ndio akupende jua sio wako huyo! Utatumia nguvu kumshawishi ila ataishia kukutumia tu.
Unaishi kwa mashaka.......
 
Back
Top Bottom