Usimvue nguo mume wako

Usimvue nguo mume wako

Ujumbe huu si kwa wanandoa tu bali hata mahali pa kazi, si vyema kusema habari za bosi wako au mfanyakazi mwenzako kwa watu wengine. Si vyema kuongea mambo ya mama au baba yako kwa watu wengi, ni dhambi.
 
Hizi ndo mada sasa, sio ananuka chupi, sijui boxer, sijui kikwapa,..... Unawezaje kumvua mwenzako nguo ndani ya mamia ya watu humu jf!!!
 
*UJUMBE KWA WANANDOA Na wachumba.*


_*"USIMVUE NGUO MUME WAKO"*_


Wakati anafungua zawadi kutoka kwa watu mbalimbali Jane alishika Box kubwa na kuanza kulifungua kwa pupa kwani alikuwa akikumbuka kuwa alipewa na Mama yake siku ya harusi yake na alitaka kujua ni kitu gani Mama yake mpendwa alimpa, Box lilikuwa jepesi sana na alipolifungua alikutana na kikaratasi kidogo kumeandikwa *USIMVUE NGUO MUME WAKO* hakukuwa na maneno mengine. Alishangaa sana kwani alishaolewa na suala la kumvua nguo mumewe alishafanya katika honeymoon. Siku iliyofuata alienda Kumuona Mama yake na kumuuliza alimaanisha nini? Hapo ndipo Mama yake alianza kumfafanulia kwa kumuambia kuwa "Moja ya kazi kubwa katika ndoa ni *kuficha mapungufu ya mume wako*huo ndiyo msingi wa ndoa na ndiyo kazi yako kama msaidizi wake.
Hakuna mwanadmu aliyekamilika, mwenza wako atakuwa na mapungufu mengi ya kimaumbile na kitabia, jaribu sana kumfichia mapungufu yake. Unapowaambia marafiki zako kuhusu mapungufu ya Mume wako unakuwa unamvua nguo na kumuondolea heshima yake mbele yao. Lakini mlolongo hautaishia hapo kama wewe ulivyoshindwa kuvumilia na kuwaambia kuwa mume wako anatabia kadha wakadha, maumbile yake yako hivi na vile ndivyo nao watashindwa kuvumilia.
Watawaambia marafiki zao wengine, watawambia wanaume zao na wanaume zao wataongea, yatasambaa mtaani na kuingia mpaka ofisini. Kila anapopita watu watamuangalia kwa mapungufu yake na hata akifanya kitu kizuri watu watakipima kwa mapungufu yake na kumdharau".
Anna kwa wasiwasi alimuuliza mama yake "Sasa nitafanyaje kama nikishindwa kuvumilia mapungufu yake?' Mama yake alimjibu "Kama ni mapungufu ya kitabia ongea naye na msaidie kubadilika, kama ni mapungufu ya kimapenzi basi msaidie kubadilika pia ila kama ni mapungufu ya kimaumbile *jifunze namna ya kukaa naye*, usimpe presha kwa kitu ambacho hawezi kukibadilisha, hajajiumba yeye hata wew una kasoro ambazo atalazimika kuzivumilia na hata hao unaowaambia wenza wao wanakasoro pia lakini hawatangazi!

Akamaliza kwa kumuuliza "Hivi kama mume wako ana Mikono midogo ukimuambia shoga yako ndiyo mikono yake itakuwa mikubwa?" Jane akajibu *Hapana*. Mama yake akaendelea "Basi huna haja ya kumtangazia na kuongelea udogo wa mikono yake, mpakulie chakula na mikono hiyo hiyo midogo aliyonayo na mfundishe namna ya kufinya tonge na mikonon kwa hiyo midogo"

Mama akamaliza na Jane akarejea nyumbani kufurahia ndoa yake.


Acha kuwa balozi wa mabaya ya mwenza wako. Kama post hii imekubariki usisahau kushare ili iwabariki na wengine.


N.B Hata kama ilishakuwepo hapa, wacha tuwakumbushe tena dada zetu, moja kati ya makosa makubwa yafanywayo na wanawake wa sasa ni kumvua nguo mmeo.



View attachment 443048
Ukipata mwanamke wa namna hiyo mshukuru mungu kwa wema huo wa mungu
 
Ahsante kwa ujumbe mzuri wenye mafunzo ndani na umeutoa kwa nyakati ambazo imekuwa ni jambo la kawaida kwa wanaume kutoa siri za wake zao na wanawake pia, hivyo umemlenga kila mtu mwenye hiyo tabia.

 
Naamini ni J2 njema.
Naileta kama nilivyoipokea, kwa sababu moja kuu kutukumbusha walio kwenyz ndoa, waendapo kwenye nyumba za ibada wakumbuke hayo yaliyiomo kwenye ujumbe huu, kwa sala na maombi.

"UJUMBE KWA WANANDOA Na wachumba."

Wakati anafungua zawadi kutoka kwa watu mbalimbali Jane alishika Box kubwa na kuanza kulifungua kwa pupa kwani alikuwa akikumbuka kuwa alipewa na Mama yake siku ya harusi yake na alitaka kujua ni kitu gani Mama yake mpendwa alimpa, Box lilikuwa jepesi sana na alipolifungua alikutana na kikaratasi kidogo kumeandikwa [l]"USIMVUE NGUO MUME WAKO"[/I] hakukuwa na maneno mengine.

Alishangaa sana kwani alishaolewa na suala la kumvua nguo mumewe alishafanya katika honeymoon. Siku iliyofuata alienda Kumuona Mama yake na kumuuliza alimaanisha nini? Hapo ndipo Mama yake alianza kumfafanulia kwa kumuambia kuwa "Moja ya kazi kubwa katika ndoa ni kuficha mapungufu ya mume wako huo ndiyo msingi wa ndoa na ndiyo kazi yako kama msaidizi wake.
Hakuna mwanadmu aliyekamilika, mwenza wako atakuwa na mapungufu mengi ya kimaumbile na kitabia, jaribu sana kumfichia mapungufu yake. Unapowaambia marafiki zako kuhusu mapungufu ya Mume wako unakuwa unamvua nguo na kumuondolea heshima yake mbele yao. Lakini mlolongo hautaishia hapo kama wewe ulivyoshindwa kuvumilia na kuwaambia kuwa mume wako anatabia kadha wakadha, maumbile yake yako hivi na vile ndivyo nao watashindwa kuvumilia.
Watawaambia marafiki zao wengine, watawambia wanaume zao na wanaume zao wataongea, yatasambaa mtaani na kuingia mpaka ofisini. Kila anapopita watu watamuangalia kwa mapungufu yake na hata akifanya kitu kizuri watu watakipima kwa mapungufu yake na kumdharau".

Anna kwa wasiwasi alimuuliza mama yake "Sasa nitafanyaje kama nikishindwa kuvumilia mapungufu yake?" Mama yake alimjibu "Kama ni mapungufu ya kitabia ongea naye na msaidie kubadilika, kama ni mapungufu ya kimapenzi basi msaidie kubadilika pia ila kama ni mapungufu ya kimaumbile jifunze namna ya kukaa naye, usimpe presha kwa kitu ambacho hawezi kukibadilisha, hajajiumba yeye hata wewe una kasoro ambazo atalazimika kuzivumilia na hata hao unaowaambia wenza wao wana kasoro pia, lakini hawatangazi!

Akamaliza kwa kumuuliza "Hivi kama mume wako ana Mikono midogo ukimuambia shoga yako ndiyo mikono yake itakuwa mikubwa?" Anna akajibu "Hapana". Mama yake akaendelea "Basi huna haja ya kumtangazia na kuongelea udogo wa mikono yake, mpakulie chakula na mikono hiyo hiyo midogo aliyonayo na mfundishe namna ya kufinya tonge na mikonon kwa hiyo midogo". Mama akamaliza na Anna akarejea nyumbani kufurahia ndoa yake.

Acha kuwa balozi wa mabaya ya mwenza wako.

FAHALISI
Wanandoa Wengi Wanashindwa Mtihani Huu. Tujitahidi kwa Vyovyote Kuenzi Funzo Hili.
 
Watakuelewa...

Tatizo binadamu ni wabishi sana...


Cc: mahondaw
Ubishi mwingi matokeo yake ni ndoa kutokudumu. Hali ya sasa hivi ya uimara wa ndoa ni mbaya sana kwa sababu ya mitandao. Tunaanika mahusiano ya ndani ya chumba kwenye mitandao ya kijamii. Na humu JF kuna bandiko kadhaa zinazohusu hayo mambo ya ndani. Na imefikia hata kuweka picha.

Tuombe maadili mema ili kudumisha furaha ya ndoa na mahusiano
 
Back
Top Bottom