Usimvue nguo mume wako

Usimvue nguo mume wako

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,700
Reaction score
4,126
*UJUMBE KWA WANANDOA Na wachumba.*

_*"USIMVUE NGUO MUME WAKO"*_

Wakati anafungua zawadi kutoka kwa watu mbalimbali Jane alishika Box kubwa na kuanza kulifungua kwa pupa kwani alikuwa akikumbuka kuwa alipewa na Mama yake siku ya harusi yake na alitaka kujua ni kitu gani Mama yake mpendwa alimpa, Box lilikuwa jepesi sana na alipolifungua alikutana na kikaratasi kidogo kumeandikwa *USIMVUE NGUO MUME WAKO* hakukuwa na maneno mengine.

Alishangaa sana kwani alishaolewa na suala la kumvua nguo mumewe alishafanya katika honeymoon. Siku iliyofuata alienda Kumuona Mama yake na kumuuliza alimaanisha nini? Hapo ndipo Mama yake alianza kumfafanulia kwa kumuambia kuwa "Moja ya kazi kubwa katika ndoa ni *kuficha mapungufu ya mume wako*huo ndiyo msingi wa ndoa na ndiyo kazi yako kama msaidizi wake.

Hakuna mwanadmu aliyekamilika, mwenza wako atakuwa na mapungufu mengi ya kimaumbile na kitabia, jaribu sana kumfichia mapungufu yake. Unapowaambia marafiki zako kuhusu mapungufu ya Mume wako unakuwa unamvua nguo na kumuondolea heshima yake mbele yao. Lakini mlolongo hautaishia hapo kama wewe ulivyoshindwa kuvumilia na kuwaambia kuwa mume wako anatabia kadha wakadha, maumbile yake yako hivi na vile ndivyo nao watashindwa kuvumilia.

Watawaambia marafiki zao wengine, watawambia wanaume zao na wanaume zao wataongea, yatasambaa mtaani na kuingia mpaka ofisini. Kila anapopita watu watamuangalia kwa mapungufu yake na hata akifanya kitu kizuri watu watakipima kwa mapungufu yake na kumdharau".

Anna kwa wasiwasi alimuuliza mama yake "Sasa nitafanyaje kama nikishindwa kuvumilia mapungufu yake?' Mama yake alimjibu "Kama ni mapungufu ya kitabia ongea naye na msaidie kubadilika, kama ni mapungufu ya kimapenzi basi msaidie kubadilika pia ila kama ni mapungufu ya kimaumbile *jifunze namna ya kukaa naye*, usimpe presha kwa kitu ambacho hawezi kukibadilisha, hajajiumba yeye hata wew una kasoro ambazo atalazimika kuzivumilia na hata hao unaowaambia wenza wao wanakasoro pia lakini hawatangazi!

Akamaliza kwa kumuuliza "Hivi kama mume wako ana Mikono midogo ukimuambia shoga yako ndiyo mikono yake itakuwa mikubwa?" Jane akajibu *Hapana*. Mama yake akaendelea "Basi huna haja ya kumtangazia na kuongelea udogo wa mikono yake, mpakulie chakula na mikono hiyo hiyo midogo aliyonayo na mfundishe namna ya kufinya tonge na mikonon kwa hiyo midogo"

Mama akamaliza na Jane akarejea nyumbani kufurahia ndoa yake.

Acha kuwa balozi wa mabaya ya mwenza wako. Kama post hii imekubariki usisahau kushare ili iwabariki na wengine.

N.B Hata kama ilishakuwepo hapa, wacha tuwakumbushe tena dada zetu, moja kati ya makosa makubwa yafanywayo na wanawake wa sasa ni kumvua nguo mmeo.

1480969698078.jpg
 
Hii post inaingia ktk top 3 zangu za wiki ya 1 ya desemba 2016........safi sana
 
Uta wasikia hata anifikishi ila Yule mwendesha bodaboda ndio ana maliza haja zangu
 
Big up kk kwa kuongea vitu vibavyojenga COZ TUMECHOKA NA WATU KULIGEUZA HILI JUKWAA KUWA LA KUNGONOKA YAAN NGONONGONO TU HAKUNA ISHU ZINGINE utackia cjui DUSHELE langu lime........ mwingine utamsikia PAPUCHI yake ili..... mara KIBAMIA kime.... ...
 
Bila shaka wote mpo sawa,kama kuna mgonjwa basi namwombea heri awe sawa.
Ni hivi baada ya kuwaza sana nikafikia uauzi wa kumuacha so kwakutaka Bali kwa kuepuka lawama yakuharibu ndoa yake ingawa nilikuwa tayali kuwa mke wapili,sasa roho inaniuma kiasi kwamba najikuta sijiekewi kama nimefanya jambo sahihi au laaa.
Tulikutana ofisini kwake miaka miwili iliyo pita,Mimi nilifika kuanza kazi pale hakunisemesha chochote,ila ikinilazimu kufanya mawasiliano nae baada ya kupata shida ya kuchelewa kupata mshahara na hapo ndipo tukaanza kuchati na baadae kuanza mahusiano.
Mwanzo kabisa was mahusiano yetu aliniweka wazi kuwa anafamilia na Mimi nilikubaliana na hill kwakuwa nilimpenda,mahusiano yetu yalikuwa ya siri kubwa lakini baada ya mama mmja mahusiàno yetu yalijulikana,hiyo hakiwa shida kwangu maana mkewe àlikuwa mbali kikazi.
Basi maisha yakaendelea,nikapata wazobla biashara nikamwambia kuwa mi nataka infante I has hara Basi akanipa mawazo yake yakanisaidia nikachukua mkopo na kufungua bihashara hiyo ambayo aliniongeza pesa kidogo kunisapoti,nikashukulu.
Mwezi huohuo akapata barua ya uhamisho akahamia alikopangiwa,maisha yakaendelea ikawa nikipata mda naenda na pia alikuwa akija.
Mapenzi yakanogà mpaka tukakubaliana kufunga ndoa,ila ikabidi tuhailishe kutokana na mkewe kupata matatizo kazini ambako ikamlazimu kwenda mbali,ambako aliishi kwa shida istoshena Bali ilivyo ngumu kwa watumishi was serikali huduma kwa familia ikawa haipo kama zamani zile pesa alizokuwa akitumiwa mkewe ikawa zimepungu,hapo ndo shida ilipo anzia,akawa kapewa habari kuwa mmewe anamwanamke alafu kamfungulia bihashara na akawa anamtuhumu kutoitunza familia na kunihonga Mimi jambo ambako so kweli Mimi najitegemea kwakiasi kikubwa kwakuwa na
*UJUMBE KWA WANANDOA Na wachumba.*

_*"USIMVUE NGUO MUME WAKO"*_

Wakati anafungua zawadi kutoka kwa watu mbalimbali Jane alishika Box kubwa na kuanza kulifungua kwa pupa kwani alikuwa akikumbuka kuwa alipewa na Mama yake siku ya harusi yake na alitaka kujua ni kitu gani Mama yake mpendwa alimpa, Box lilikuwa jepesi sana na alipolifungua alikutana na kikaratasi kidogo kumeandikwa *USIMVUE NGUO MUME WAKO* hakukuwa na maneno mengine. Alishangaa sana kwani alishaolewa na suala la kumvua nguo mumewe alishafanya katika honeymoon. Siku iliyofuata alienda Kumuona Mama yake na kumuuliza alimaanisha nini? Hapo ndipo Mama yake alianza kumfafanulia kwa kumuambia kuwa "Moja ya kazi kubwa katika ndoa ni *kuficha mapungufu ya mume wako*huo ndiyo msingi wa ndoa na ndiyo kazi yako kama msaidizi wake.
Hakuna mwanadmu aliyekamilika, mwenza wako atakuwa na mapungufu mengi ya kimaumbile na kitabia, jaribu sana kumfichia mapungufu yake. Unapowaambia marafiki zako kuhusu mapungufu ya Mume wako unakuwa unamvua nguo na kumuondolea heshima yake mbele yao. Lakini mlolongo hautaishia hapo kama wewe ulivyoshindwa kuvumilia na kuwaambia kuwa mume wako anatabia kadha wakadha, maumbile yake yako hivi na vile ndivyo nao watashindwa kuvumilia.
Watawaambia marafiki zao wengine, watawambia wanaume zao na wanaume zao wataongea, yatasambaa mtaani na kuingia mpaka ofisini. Kila anapopita watu watamuangalia kwa mapungufu yake na hata akifanya kitu kizuri watu watakipima kwa mapungufu yake na kumdharau".
Anna kwa wasiwasi alimuuliza mama yake "Sasa nitafanyaje kama nikishindwa kuvumilia mapungufu yake?' Mama yake alimjibu "Kama ni mapungufu ya kitabia ongea naye na msaidie kubadilika, kama ni mapungufu ya kimapenzi basi msaidie kubadilika pia ila kama ni mapungufu ya kimaumbile *jifunze namna ya kukaa naye*, usimpe presha kwa kitu ambacho hawezi kukibadilisha, hajajiumba yeye hata wew una kasoro ambazo atalazimika kuzivumilia na hata hao unaowaambia wenza wao wanakasoro pia lakini hawatangazi!

Akamaliza kwa kumuuliza "Hivi kama mume wako ana Mikono midogo ukimuambia shoga yako ndiyo mikono yake itakuwa mikubwa?" Jane akajibu *Hapana*. Mama yake akaendelea "Basi huna haja ya kumtangazia na kuongelea udogo wa mikono yake, mpakulie chakula na mikono hiyo hiyo midogo aliyonayo na mfundishe namna ya kufinya tonge na mikonon kwa hiyo midogo"

Mama akamaliza na Jane akarejea nyumbani kufurahia ndoa yake.

Acha kuwa balozi wa mabaya ya mwenza wako. Kama post hii imekubariki usisahau kushare ili iwabariki na wengine.

N.B Hata kama ilishakuwepo hapa, wacha tuwakumbushe tena dada zetu, moja kati ya makosa makubwa yafanywayo na wanawake wa sasa ni kumvua nguo mmeo.

View attachment 443048
 
Back
Top Bottom