Usimsingizie Shetani, maana mbinu zake zote unazijua.

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,029
5,259
Neno la Mungu linasema kuwa tusishindwe na shetani kwa kuwa mbinu zake shetani, tunazijua.

Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.
2 Kor 2:11 SUV

Ni kweli kuwa kila mara mtu anapotaka kufanya dhambi, hujua kabisa kuwa hii niifanyayo ni dhambi na huridhia mwenyewe kuifanya, Shetani alicho nacho ni mbinu tu napo hazitumii kwako bali anakushawishi, muamuzi ni wewe mwenyewe.
 
Kuzijua mbinu za shetani sio kuzishinda...

Shetani ana mbinu na ushawishi mkubwa...
 
Kuzijua mbinu za shetani sio kuzishinda...

Shetani ana mbinu na ushawishi mkubwa...
Mungu na Shetani huwa hawaingilii free will ya mwanadamu. Kumshinda shetani ni maamuzi ya mtu na wala sio kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa shetani, maana tayari unajua kuwa shetani ni mshawishi.

Unapotaka kuchepuka, unakwenda loji ya mtaa wa mbali na unapoishi, unatafuta gari ya tinted, unamwambia mchepuke asiongozane nawe nk, hizi zote sio mbinu za shetani, ni maamuzi yako baada ya kushawishiwa.
 
Kumshinda shetani ni kuwa na Mungu pekee...

Shetani ni Roho na Mungu ni Roho

Ila mwanadamu ana mwili wa nyama, amabao unamapungufu mengi, hivyo kwa akili zake hawezi...
 
Kumshinda shetani ni kuwa na Mungu pekee...

Shetani ni Roho na Mungu ni Roho

Ila mwanadamu ana mwili wa nyama, amabao unamapungufu mengi, hivyo kwa akili zake hawezi...
Imeandikwa mtii Mungu na umpinge Shetani.

Pamoja na kuwa mwanadamu ni dhaifu, lakini kuwa na Mungu pekee haitoshi, ni lazima kwa kinywa chako na kwa matendo yako, umpinge na kumkataa shetani na kazi zake.

Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Yak 4:7 SUV
 
Back
Top Bottom