Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 54,721
- 102,505
Ni ujinga usio kifani kumpeleka mtoto wa shule ya msingi bweni.Ni upuuzi upuuuziii ban upuuuuuuuziiiiiii!Siko hapa kukupangia namna ya kuishi na familia yako, ila naomba nikushauri kitu;
kumpeleka mwanao akaishi bweni kwanza ni ulimbukeni, kama mtoto ana akili, hata akisoma day atafaulu tu.
wapo wanaosoma wakiwa boarding awali mpaka form4.. na bado wanafeli!
hasara kubwa anayoipata mtoto ni kukosa malezi ya wazazi. Mtu aliesoma katika mazingira hayo, hata ukubwani utamjua tu!
sasahivi tuna vijana mpaka wazee wa hovyo sana lakini cha ajabu ni wasomi (walikosa malezi ya wazazi)
tunawapa wanawake lawama za kila rangi kumbe sio wao bali "walikosa malezi bora ya wazazi": binti wa for4 & std7 alielelewa na wazazi ni bora (anaweza kuwa mke bora) kuliko degree holder aliekulia boarding kipindi chote cha makuzi yake
kuna msemo huu:- "asiyefunzwa na wazazi dunia itamfunza"
umekosa nini mpaka mwanao ukamkabidhi mikononi mwa walimwengu wamfunze?
Kaa karibu na mwanao kwa faida yake, huko mbele kuna hatari.
NB. Nazungumzia watoto under18
Mkuu unautani na mimi sio?Tumia akili mama j
Nakubaliana na wewe kabisaSiko hapa kukupangia namna ya kuishi na familia yako, ila naomba nikushauri kitu;
kumpeleka mwanao akaishi bweni kwanza ni ulimbukeni, kama mtoto ana akili, hata akisoma day atafaulu tu.
wapo wanaosoma wakiwa boarding awali mpaka form4.. na bado wanafeli!
hasara kubwa anayoipata mtoto ni kukosa malezi ya wazazi. Mtu aliesoma katika mazingira hayo, hata ukubwani utamjua tu!
sasahivi tuna vijana mpaka wazee wa hovyo sana lakini cha ajabu ni wasomi (walikosa malezi ya wazazi)
tunawapa wanawake lawama za kila rangi kumbe sio wao bali "walikosa malezi bora ya wazazi": binti wa for4 & std7 alielelewa na wazazi ni bora (anaweza kuwa mke bora) kuliko degree holder aliekulia boarding kipindi chote cha makuzi yake
kuna msemo huu:- "asiyefunzwa na wazazi dunia itamfunza"
umekosa nini mpaka mwanao ukamkabidhi mikononi mwa walimwengu wamfunze?
Kaa karibu na mwanao kwa faida yake, huko mbele kuna hatari.
NB. Nazungumzia watoto under18
Hakuna lolote. Hakuna haja ya mtoto kusoma bweni. Uozo mtupushule za bweni zilizo chini ya kanisa ni bora kuliko hizo zingine binafsi
Kumpeleka mtoto boding shule za msingi ni mbinu ya wazazi kukwepa majukumu ya malezi kwa mtoto. Umri huu (miaka 0-14) mtoto anapaswa kuwa chini ya uangalizi wa wazazi na si mtu mwingine. Kwa level ya sekondari mtoto kukaa bweni si vibaya
Usijidanganje lea mtoto wako mwenyewe hakuna bweni ya kanisa wala ya binafsi zote hazifai kwa malezi ya mtoto.shule za bweni zilizo chini ya kanisa ni bora kuliko hizo zingine binafsi
Hujamuelewa mtoa mada anazungumzia boarding kwa watoto wa primary. Miaka 14 umekuwa tayari.Najivunia kusomea boarding school tena boys tu nikiwa na miaka 14. Hakika nimemiss hekaheka za kutufunza na kutupa malezi yaliyojazia yale ya wazazi. Hakika Popote ulipo Mwalimu Laban Kansimba na timu yako ya Nyakato Sec ya bukoba kongole sana. Ukimpeleka mtoto shule ya boarding kwa mentality ya kuiga ujinga na kufuata mkumbo hakika atauiga kweli. Boarding haina shida shida ni wewe mzazi na huyo mwanao