Usimpeleke mwanao shule za bweni

Shule za boarding ziko vizuri kiufaulu na kuwa na Walimu bora kuliko za day
 
Nilimsikia akibishana na mkewe kuhusu mtoto wao kwenda boarding. Akamwambia, "sikuona faida yoyote niliyoipata wakati nasoma boarding zaidi ya kujifunza punyeto".
Kwanza watoto wa boarding schools ni mazuzu! Hadi mtoto wa kiume unakuta ana aibu aibu kama wa kike!
 
Mtoa mada unaweza kuwa sahihi, kwa hoja yako ila kwa miaka hii ya karibuni.
Miaka ya nyuma boarding ilikuwa ni nzuri sana. Hasa mimi nimesoma kuanzia std 5 boarding mpk form 6. Zote za masista, sijutii kwa kweli.
Nimejifunza mengi, bila kuwa boarding ningesoma day, ningekuwa mayai kupindukia.

Leo hii nikiangalia nyuma, nashukuru kupitia boarding.
Kwasasa dunia imebadilika, kimaadili boarding si salama tena kwa watoto.
 
Wengi Mambo ya kihuni wanajifunzia huko.
 
Nimewahi kufanya kazi fulani shule hii ya wasichana huko Morogoro, i'm sure wana malezi bora kabisa kwa watoto wa kike kiasi unaweza kumpeleka mwanao hapo.

Ilikuwa ni nyuma kidogo nadhani 2014 natumaini hata sasa wapo hivyo.View attachment 2464596
 
Kwa uandishi huu na wewe ni zao la day school, ingawa sio mbaya.

Unasema mtoto yupi asiende boarding? Na boarding ipi. Kwa hiyo una maanisha Serikali isijenge mabweni na yaliyopo wafugie kuku au una maana gani.

Kwa hiyo mwanao akichaguliwa form 1 kwenda shule za boarding km Bwiru, Tabora nk, utamzuia sababu boarding ataharibika. Vipi akichaguliwa form 5 utamzuia pia au.

Kabla hujaleta mada hakikisha unaeleweka kwa kuweka bayana unacholenga kuzungumzia.

Tuache maneno ya vijiweni kujazana hofu. Wazazi wanalilia hosteli shule za kata kuwaokoa mabinti na mafataki alafu wewe unakuja kuleta stori za mtaani. Mnataka watoto wa kike wawe wanatokea makwao ili muwatafune? Umewahi kumpeleka mwanao boarding ukaona matokeo hasi ya kukukatisha tamaa? Lete ushahidi, vinginevyo tafuta besa.

Huna point wala utofauti na wanaosema English medium ni kupoteza pesa. All of you are sailing in the same boat. Vinginevyo labda ujibu maswali yangu hapo juu.

Sizitaki mbichi hizi!!!!!
 
Shule za boarding ziko vizuri kiufaulu na kuwa na Walimu bora kuliko za day
Mtoto anaweza kufaulu shule yoyote ukimjengea mazingira mazuri ya kufaulu anafaulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…