Usimkopeshe hela mtu

Mm kuna rafik yangu alinikopa 5,000/=mpaka leo anitafuti tena.
 
Mimi nimepoteza ndugu watatu. Mmoja Ni mtoto wa mjomba, kanikopa kwa shida zake mwaka wa tatu huu. Juzi nikikuambia asinijue na nisimjue na namba zake nikazifutilia mbali. Wengine wawili Ni watoto wa baba yangu, nao vivyo hivyo hata tulikutana popote kila mtu na hamsini zake. Ni Bora kua na marafiki WACHACHE kuliko utitiri wa ndugu mbwa.
 
Kwakweli Binafsi nimedhukumiwa laki sita na jamaa yangu mmoja, tena yeye niilmpa kadi ya benk kabisa akachukue aliomba laki tano badae napata message kachukua laki sita tangu 2015 daah!

Ila na mimi nadaiwa na jamaa zangu wawili mmoja ananidai laki mmoja mwingine 60,000/= mmoja kanipigia sana jana sijapokea maana sina hela namwambiaje sasa
ila nitalipa tu.
 
Rafiki yangu nilimkopesha pesa mwaka jana, siku zimeenda kafilisika kibiashara na sioni dalili ya. Kupata hiyo pesa yangu, roho yaniuma sana
Pole sana mkuu. Kaka yangu mmoja alinieleza "siku ukimkopesha rafiki yako, ni mwanzo wa urafiki kufa" Sikumuelewa mpaka siku yaliponikuta ya kunikuta. Unamkopesha mtu na hana hata aibu ya kusema alipe deni. 🤬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…