Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,635
- 729,550
Si kitu kigeni kabisa miongoni mwetu na hata baadhi yetu tunazo tumezivaa, zinaitwa Pete za bahati.Kiuhalisia si Pete za bahati ni Pete za kishetani ni Pete za maagano ni za kuzimu,ukivaa ile ni sawa na kupigwa mhuri.
Wengi wanaozivaa haziwasaidii kivile na nyingi hazina nguvu kivile kwakuwa ni za kitapeli zilizo halisi ni very powerful na zinafanya mambo yaliyokusudiwa
Maisha yako Mungu ndie ayajuaye kushindwa kwako kushinda kwako kuna yeye (kwa wale waamini na waaminio )
Maisha yana changamoto nyingi na kuna wakati katika maisha kila kitu huyumba na kupoteza mwelekeo kabisa lakini ukiwa mvumilivu na kusimama na Mungu wako yatapita na utasimama tena.
Kuna kufanyiwa mambo mabaya machafu ya kuharibu future ya mtu mara nyingi ushirikina ukitumika,lakini usitende kinyume na Mungu simama naye usiende kwa waganga wengi ni waongo na matapeli.
Ikifikia uamuzi wa kwenda huko hakikisha unaenda kwa mtu sahihi mwenye tiba sahihi kwasababu haya mambo pia yapo lakini ogopa kubebeshwa maagano na mihuri ya kuzimu kwenye mapete ya bahati ili usije kuwa mtumwa maisha yako yote badala ya kumwamini Mungu unayaamini mapete.
Kuna mengi kwenye hizi Pete ivae ukiwa unajua kwa hakika umevaa kitu gani.