Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,291
- 14,782
Fb ni ya watoto wanaojifunza kutumia simu
Na unaweza kukuta wewe ni Member mzuri sana kule, ila umeamua kufuata mkumbo kwa wale waliotangulia na kusema Facebook ni watoto.
Jamiiforums wana ukurasa kule, nao ni watoto wanajifunza kutumia?
Watu wengi maarufu wana kurasa zao kule na wanatumia kama majukwaa ya kusemea maoni yao.
Facebook utaiona ni ya watoto endapo umejaza marafiki watoto ambao post zao ni za Salamu "Jamani usiku mwema, Jamani karibu tule, jamani naumwa mniombee, Jamani niko safarini maombi yenu na ujinga meingi unaofanana na huo" na ume like Kurasa za kina Shilawadu lazima utaiona Facebook kama ni ya kitoto.
Ila kama umezungukwa na marafiki ambao Post zao zinakuhamasisha na ume Like Page za maana ambazo zinafundisha na kuhabarisha Facebook hutaiona ya kipuuzi.
Utaiona Facebook ya hovyo endapo umechagua kupata taarifa za namna gani.
Aliyoyasema mtoa mada yote yapo, na hii kwasababu kila mtu anapenda aonekane(kama ilivyo kwa hulka ya wabongo)
Lakini tutakupima kwa Comments zako na Post zako. Mtu aliyesoma kweli na anayejua matumizi sahihi ya mitandao hawezi akapost eti 'Jamani usiku mwema nalala' hizi ni Private zako wewe.
Aliyesoma kweli tunategemea atupe mawazo firikishi.

