Usilolijua kuhusu Facebook

Usilolijua kuhusu Facebook

1. Ni mahali ambapo watu hukuomba urafiki lakini mkikutana mtaani wanakupotezea kama hawakujui.

2. Ni mahali ambapo kila mahusiano yapo perfect kama ya ndotoni.

3. Ni mara chache kukuta mtu yupo divorced au kaachwa na mpenzi wake asilalamike kama sanduku la maoni.

4. Ni mahali ambapo kila anayedanganya huamini anasema kweli.

5. Ni mahali ambapo maadui zako na wasiokupenda hutembelea profile yako mara nyingi kimyakimya kuliko unavyojua.

6. Ni mahali ambapo ndugu na marafiki zako wa ukweli wana ku-block kama unabisha jaribu kukagua utashangaa.

7. Ni mahali ambapo ukiandika status yoyote au jambo lolote la kukosoa watu wanajua umewakosoa wao au watasema umeachwa kama ni issue ya mapenzi hata kama uliandika mawazo ya kufikirika tu.

8. Ni mahali ambapo kila mwanamke akiweka picha atasifiwa amependeza hata kama hajavaa nguo ataambiwa nguo aliyovaa imemtoa balaa na yeye atasema asante ni kwa neema tu.

9. Ni mahali ambapo kila mtu amesoma mpaka chuo kikuu tena UDSM na anaishi Dar, Mwanza au Arusha na kama ni Dar basi anaishi mbezi beach hata kama anaishi kimara BONYOKWA.

10. Ni mahali ambapo wengi hupiga picha kuonesha anaendesha gari huku hakuna ufunguo na HANDBRAKE ipo juu.

11. Ni mahali ambapo wanawake wengi hujiuza kwa style ya Ku post picha za kuonesha maungo ya miili yao ili kuwavutia wateja wao.

12. Ni mtandao ambao ukiutumia vizuri kwa marafiki ulionao utaweza hata kujenga nyumba hasa ukiwatumia kama rasilimali.

13. Ni mtandao uliojaa matapeli wengi zaidi kuliko mtandao wowote ule.
 
Jamaa unaonekana mtumiaji mzuri sana wa fb, maana uchambuzi wako hakika ni mtumiaji mzuri sana
Upo sahihi, kuna magroup fulani nimejiunga uwa yana nipa habari mubashara.
 
Ni mahali ambapo Majini yanavaa sura ya mtu na kukuomba urafiki
ukikubali tu yanakungia na kuanza kukutesa na kukuhalibia maisha.
Ni mahali wachawi wanatumia kuwanasa watu wanaomkubali kila mtu anayewaomba urafiki
Hii ni kweli tupu.
Usikubali kubali urafiki kwa mtu usiyemjua wala kumfanyia utafiti. ID nyingi zinazotumika ni feki, picha za uongo hutumika kujitambulisha.
Jihadhalini.
 
Ni mahali ambapo kila mtu ni mkurugenzi na vikampuni fake viingiii
 
Sijasema kuko vibaya, ni vizuri mtu kusema ukweli kuliko kudanganya actually nilivutiwa na hilo jina ingeweza kuwa hata Tandale kwa mama zakaria.
Ila hilo jina nalo linafanya mtu adhani ni kama kwa mfuga mbwa au mtogore. Wabadilishe basi hata waite Kimara Magufuli au Kimara Makonda
 
Mtoa mada bado elimu yako ni kidogo sana au inawezekana umesoma ila hujaelemika.
Sio kweli kuwa kila kitu cha kimaendeleo kitakachokuja kitakuja na mazuri tuu. Unatakiwa ujue vipi vizuri as kwa upande wako na inategemea mtu na mtu anaamini vipi kuhusu uzuri wa kitu. Unataka watu waweke picha wakiwa wamevaa mavitenge tuu na mandhari yao ikiwa ni kwa mnyamani au manzese au mbagala? Ili nini kwa mfano? Binadamu wanapenda vitu vizuri tuu nikwambie usipate presha ukiona watu wako sehem nzuri au wana drive, hata kama mtu amepiga picha akiwa ana drive na hata kama gari sio lake sio tabu kwani mtu kuonyesha ana drive ni kitu kizuri, nani asiyependa kudrive? Unataka waweke wakitembea na watu hawapendi kutembea? Zamani wakati sijanunua gari nilikua napiga picha na magari ya wenzangu nadhani iliniongezea ari ya kutaka kununua langu siku moja.
 
Back
Top Bottom