Usilolijua kuhusu Facebook

Boloyoung

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
682
652
1. Ni mahali ambapo watu hukuomba urafiki lakini mkikutana mtaani wanakupotezea kama hawakujui.

2. Ni mahali ambapo kila mahusiano yapo perfect kama ya ndotoni.

3. Ni mara chache kukuta mtu yupo divorced au kaachwa na mpenzi wake asilalamike kama sanduku la maoni.

4. Ni mahali ambapo kila anayedanganya huamini anasema kweli.

5. Ni mahali ambapo maadui zako na wasiokupenda hutembelea profile yako mara nyingi kimyakimya kuliko unavyojua.

6. Ni mahali ambapo ndugu na marafiki zako wa ukweli wana ku-block kama unabisha jaribu kukagua utashangaa.

7. Ni mahali ambapo ukiandika status yoyote au jambo lolote la kukosoa watu wanajua umewakosoa wao au watasema umeachwa kama ni issue ya mapenzi hata kama uliandika mawazo ya kufikirika tu.

8. Ni mahali ambapo kila mwanamke akiweka picha atasifiwa amependeza hata kama hajavaa nguo ataambiwa nguo aliyovaa imemtoa balaa na yeye atasema asante ni kwa neema tu.

9. Ni mahali ambapo kila mtu amesoma mpaka chuo kikuu tena UDSM na anaishi Dar, Mwanza au Arusha na kama ni Dar basi anaishi mbezi beach hata kama anaishi kimara BONYOKWA.

10. Ni mahali ambapo wengi hupiga picha kuonesha anaendesha gari huku hakuna ufunguo na HANDBRAKE ipo juu.

11. Ni mahali ambapo wanawake wengi hujiuza kwa style ya Ku post picha za kuonesha maungo ya miili yao ili kuwavutia wateja wao.

12. Ni mtandao ambao ukiutumia vizuri kwa marafiki ulionao utaweza hata kujenga nyumba hasa ukiwatumia kama rasilimali.

13. Ni mtandao uliojaa matapeli wengi zaidi kuliko mtandao wowote ule.
 
Yote nakuunga mkono lakini kimara bonyokwa pako vizuri kuliko uzaniavyo na watu wa bonyokwa wengi wana maisha ya kati.
 
Yote nakuunga mkono lakini kimara bonyokwa pako vizuri kuliko uzaniavyo na watu wa bonyokwa wengi wana maisha ya kati.
Sijasema kuko vibaya, ni vizuri mtu kusema ukweli kuliko kudanganya actually nilivutiwa na hilo jina ingeweza kuwa hata Tandale kwa mama zakaria.
 
Mi nautumia kupata taarifa za ndugu, marafiki na jamaa
Matharani msiba, harusi nk.

Nilishaachaga kupost coz ukionekana una life bovu upati like wala mention ila ukiigiza maisha bongo move utapata like hata kwa wasiokufahamu
 
Jamaa unaonekana mtumiaji mzuri sana wa fb, maana uchambuzi wako hakika ni mtumiaji mzuri sana
 
Back
Top Bottom