Mtoa mada bado elimu yako ni kidogo sana au inawezekana umesoma ila hujaelemika.
Sio kweli kuwa kila kitu cha kimaendeleo kitakachokuja kitakuja na mazuri tuu. Unatakiwa ujue vipi vizuri as kwa upande wako na inategemea mtu na mtu anaamini vipi kuhusu uzuri wa kitu. Unataka watu waweke picha wakiwa wamevaa mavitenge tuu na mandhari yao ikiwa ni kwa mnyamani au manzese au mbagala? Ili nini kwa mfano? Binadamu wanapenda vitu vizuri tuu nikwambie usipate presha ukiona watu wako sehem nzuri au wana drive, hata kama mtu amepiga picha akiwa ana drive na hata kama gari sio lake sio tabu kwani mtu kuonyesha ana drive ni kitu kizuri, nani asiyependa kudrive? Unataka waweke wakitembea na watu hawapendi kutembea? Zamani wakati sijanunua gari nilikua napiga picha na magari ya wenzangu nadhani iliniongezea ari ya kutaka kununua langu siku moja.