Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
1.
Masaa kumi na mbili, toka jua la utosi,
Tena upate kandili, sidhani utusitusi,
Kiza chake si kalili, nyakati za wasiwasi,
Chukua udhu uswali, kwa mola wako Qudusi.
Usiku wa manane, ni usiku wa shari.
2.
Nyakati yake zohali, visoke hupanda rasi,
Wanga hufanya shughuli, kutia watu nuhusi,
Usiku una makali, nadhani kama makasi,
Niwache nifanye fali, kwalo niite farisi,
Usiku wa manane, ni usiku wa shari.
3.
Jambazi huiba mali, wakiipata nafasi,
Usingizini u mbali, ati wapiga gambusi,
Kumbe umelala chali, waibiwa kirahisi,
Lala yako afadhali, upone yake risasi,
Usiku wa manane, ni usiku wa shari.
Dotto Chamchua Rangimoto(Njano5)
0762845394/0784845394
Mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania